Umuhimu wa michezo katika makuzi ya mtoto

Umuhimu wa michezo katika makuzi ya mtoto

Anita Kajembe

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2021
Posts
215
Reaction score
487
Michezo humfunza mtoto ubunifu, kujenga ushirikiano na wenzake, mawasiliano nk. Hivi vyote ni muhimu katka maisha ya baadae ya mtoto. Katika michezo watoto wanapata nafasi ya kupanga sheria na taratibu ili wote washiriki. Hijifunza kushirikiana katika vifaa vyao vya michezo.

Watoto wanapocheza ni muhimu mkubwa kuwepo kuangalia tu ulinzi na usalama. Mengine ni vizuri kuwaachia watoto wafanye maamuzi yao. Usimuingilie mtoto katika mchezo kabla hajaukinahi. Mtoto akisha kinahi mchezo anauacha. Hapa kitaalamu wanasema mtoto amefikia play cue. Kumkatisha mtoto mchezo kabla hajafikia play cue ni sawa na kukatishwa kunywa maji kabla hujakata kiu.

Michezo haina lugha, weka mtoto wa Kichina, Kiswahili, Kifaransa pamoja. Utawakuta wanacheza na kupanga sheria za mchezo bila kuwasiliana kwa lugha yeyote zaidi ya lugha ya mchezo.

Nchi za Scandinavia zimewekeza sana katika michezo ya watoto kama sehemu ya elimu ya awali. Scandnavia mtoto anaanza elimu ya darasani (formal education)skiwa na miaka mitano. Kuanzia miaka miwili anaanza kuhudhuria play groups, play grounda ect.

Hili la kuwaachia watoto wacheze na kujifunza kutokana na michezo wana sayansi wanasema limesaidia kupunguza idadi ya watoto wenye Attention deficit hyperactivity disorder (ADHD) kulinganisha na sehemu nyingine za dunia ambako formal education huanza mapema.

Michezo kwa watoto ikiandaliwa sehemu salama na mtu mwenye ujuzi wa kuwasimamia husaidia kuinua uchumi wa jamii. Wamama wenye watoto kuanzia miaka miwili wakipata sehemu ya kuwaacha watoto wao asubuhi mpaka saa nane mchana. Itawasaidia kufanya shughuli zao za uzalishaji.
 
Back
Top Bottom