Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Michezo inasaidia watoto kuwachangamsha, kuwapa ubunifu na kuwafikirisha. Katika duniani ya mtoto mwana sesere si tu kifaa cha michezo bali anaweza kuwa pacha wake kimawazo, atataka ale nae na alale nae.
Wazazi wengi kutokana na ugumu wa maisha au kutokujua hawaoni umuhimu wa kununua vifaa vya michezo kwa watoto wao. Hata huku kwetu Kwamtogole wale watoto wenye vifaa maalumu vya kuchezea wengi wanaishi kwenye nyumba za mageti.
Udogo wangu sehemu nilitokulia hakukua hata na shule ya chekechea. Alitokea mama mmoja aliekua na passion ya kulea watoto na alipewa banda la gari na kiongozi wa serikali ambae hakulitumia banda lile. Lilisafishwa na kutandikwa mikeka. Tulipata nafasi ya kujifunza kuimba, kucheza na kuhesabu.
Hakukua na michezo mingi, ila kulikua na Hospitali moja ya watawa walikua na michezo waliyoiweka kwenye clinic ya mama na mtoto. Wale wa mama wanaopeleka watoto clinic kulikua na kona ya watoto kucheza na walikuwepo wasaidizi wa kuwaangalia watoto. Hii iliwasaidia wakinamama kutokukosa clinic kwa shida ya ulezi. Watoto walipenda kwenda clinic kwasababu ya michezo. Hata kama anaepimwa ni yule wa mikononi.
Siku ya Ijumaa hakukua na clinic ya mama na mtoto hivyo wale watawa kwa kuelewa umuhimu wa vifaa vya michezo kwa watoto, walileta mabox ya michezo shuleni kwetu. Walitupa masaa mawili na walihesabu na kusafisha vifaa vyao kabla hawajaondoka . Wavulana walipewa mipira, magari na wanyama . Wasichana tu kupata wanasesere , nguo zao, jiko la kupikia pamoja na sufuria zake.
Nimeona clinic zetu zinazojengwa huwa hazitoi nafasi kama hizi. Ingewezekana hili kufanyika lingeboresha huduma za Afya. Wale wanaokwenda hospitali binafsi mmeshaona kona ya watoto kucheza. Kwa kweli michezo ya watoto ni sehemu ya utoto tusiwanyime utoto bora.