UN imetahadharisha Tanzania kuepuka mazingira ya ukandamizaji hasa kipindi hiki cha Uchaguzi Mkuu

Quinine

Platinum Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
25,848
Reaction score
63,306
Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet ameeleza kuwa, nchini Tanzania kumekuwepo hali ya "kuongezeka kwa ukandamizaji wa kidemokrasia na haki za raia, hali ambayo inazidi kufanya mazingira ya haki za binadamu kuwa duni". Ameeleza hasa mabadiliko ya sheria mbalimbali hususani (Na. 3) ya 2020, ambayo amesema kuwa inazuia uwajibikaji wa serikali kwa ukiukaji wa haki za binadamu nchini Tanzania.

Amesema wakati uchaguzi ukitarajiwa kufanyika mwezi ujao nchini Tanzania, ''tumekuwa tukipokea ripoti kuhusu ukamataji holela na kushikiliwa kwa wanaharakati, waandishi wa habari na wapinzani.

"Kati ya sheria nyingi ambazo zimezuia haki ya raia mitandaoni na nje ya mtandao katika miaka ya hivi karibuni, Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 3) ya 2020 inaminya wigo wa kufungua kesi za ukandamizwaji wa haki za binaadamu... kubinywa zaidi kwa haki za binadamu kunaweza kusababisha athari mbaya, na amehimiza hatua za haraka na endelevu kuzuia hali hii," ameeleza Bi Bechelet.

Bechelet ametoa wito kwa Serikali kusimamia haki za wakimbizi wote, na kuhakikisha kuwa kurudi kwa wakimbizi kunasimamiwa kwa usalama, kwa heshima na kwa hiari.

Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 3) ya 2020 ulipitishwa na Bunge la Tanzania mwezi Juni na baadaye kusainiwa kuwa sheria na rais John Magufuli. ikiwemo kuwapa kinga ya viongozi wakuu akiwemo rais dhidi ya kushtakiwa kwa madai ya kuvunja katiba na sheria.

Kati ya mabadiliko hayo yaliyopitishwa, maeneo mawili yalizua mjadala na kupingwa vikali na wanaharakati wa haki za binaadamu na vyama vya upinzani.

Eneo la kwanza ni la viongozi wakuu wa mihimili ya dola, ambao ni Rais, Makamu wa Rais, Jaji Mkuu, Spika na Naibu Spika kushtakiwa kwa kuvunja sheria na katiba wakiwa madarakani. Kwa mujibu wa sheria hiyo, sasa atakayeshtakiwa kwa niaba ya viongozi wote hao ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Eneo la pili ni kuminywa kwa wigo wa kufungua kesi za kikatiba, kabla ya sheria hiyo kupitishwa, mtu yeyote alikuw na uhuru wa kwenda mahakamani na kufungua kesi ya kikatiba pale anapoona jambo fulani hususani la ukiukwaji wa haki za binaadamu linafanyika kwa mujibu wa sheria. Hivi sasa, inahitajika mtu kuwa na maslahi ya moja kwa moja ama kuathirika moja kwa moja na sheria husika kabla ya kufungua kesi.

Hoja za serikali ya Tanzania.

Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Palamagamba Kabudi ameiambia BBC kwamba wamepokea ripoti hiyo kwa mshangao mkubwa na kuongeza kwamba kamishena huyo angelikuwa Tanzania hangeliandika maneno kama hayo au kutoa tathmini aliyoitoa.

''Kwanza tumechukua hatua ya leo kwamba balozi wa Tanzani katika Umoja wa Mataifa katika ofisi ya Genive anawasilisha majibu yetu rasmi kuhusu taarifa hiyo aliyoitoa'' alisema Bwana Kabudi.

Pia aliongeza kuwa hali halisi nchini Tanzania ni tofauti na yale aliyosema Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet akiangazia hali ya siasa kipindi hiki cha uchaguzi.

''Sasa tuko katika uchaguzi mkuu tunao wagombea nafsi ya urais 17 na wote wanafanya mikutano yao nchi nzima kila sehemu na hakuna aliyezuiliwa kufanya mikutano ''anasema'' kweli kwa wengine ni mshangao''.

Awali akizungumza wakati muswada wa sheria hiyo ukipitishwa Bungeni, Mwanasheria Mkuu wa Tanzania, Profesa Adelardus Kilangi alisema mabadiliko hayo hayataondoa dhana ya kupata suluhu.

"Lengo la kufungua kesi hizi ni kupata suluhu, hivyo hata akishtakiwa mwanasheria mkuu bado suluhu itapatikana mahakamani kisheria."

Kwa mujibu wa Profesa Kilangi, hata sasa kwenye kesi zote ambazo serikali inashtakiwa ama hata kesi za ubunge bado mwanasheria mkuu anasimama mahakamani.

"Lengo la marekebisho haya pia ni kuwa na maudhui ya dhana ya kinga dhidi ya Rais ambayo ni kulinda hadhi ya Rais na nafasi yake," amesema pia Profesa Kilangi.

Kuhusu haki ya mtu yoyote kufungua mashtaka ya haki za ukiukwaji wa haki za binadamu, amesema kuwa Katiba inaelekeza kuwa kutakuwa na utaratibu wa kufuatwa utakaowekwa kisheria.

"Hapa hatukiuki katiba, tunaweka utaratibu wa kisheria…hili suala la nani ahusike katika kufungua mashtaka haya (locus standi) ni mjadala mpana.

Tunasema yule ambaye mwenye maslahi ya moja kwa moja ndiyo afungue mashtaka. Hata Mahakama ya Haki za Binadamu ya Ulaya imeweka wazi msimamo wake kuwa lazima uwe umeathirika moja kwa moja ndiyo ufungue mashtaka katika mahakama hiyo."
 
Wasitusumbue hawa ma mbuzi ni nchi gani inawaruhusu wahuni watukane viongozi na kuganya uhani.
 
Wasitusumbue hawa ma mbuzi ni nchi gani inawaruhusu wahuni watukane viongozi na kuganya uhani

Wewe heshimu uhuru na haki za kila raia wa TZ

watu wanahitaji heshima, utu na haki zao za msingi.
 
Waambie tumewasikia na uchaguzi huu utakuwa huru na haki huku Lisu akipata si zaidi ya asilimia 20
 
Ccm wanajifanya wao ni watetezi wa wanyonge kumbe wao ndio wanatufanya sisi tuonekane wanyonge
 
Ripoti zingine ni za kijinga Sana, na huenda shirika hili limekosa watu wenye weledi, ripoti ya kiujumla Sana hii, haisemi ni kina Nani wamewekwa ndani Wakati huu WA Kampeni na Kwa kusingiziwa makosa yepi

Hizi ripoti za kijinga namna hii nimeanza kuziona Wakati huu huu WA Korona, huwenda wazungu uelewa wao umefyekwa na viruses hawa,. pumbavu kabisa!!
 
Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet ameeleza kuwa, nchini Tanzania kumekuwepo hali ya "kuongezeka kwa ukandamizaji wa kidemokrasia na haki za raia, hali ambayo inazidi kufanya mazingira ya haki za binadamu kuwa duni". Ameeleza hasa mabadiliko ya sheria mbalimbali hususani (Na. 3) ya 2020, ambayo amesema kuwa inazuia uwajibikaji wa serikali kwa ukiukaji wa haki za binadamu nchini Tanzania.

Amesema wakati uchaguzi ukitarajiwa kufanyika mwezi ujao nchini Tanzania, ''tumekuwa tukipokea ripoti kuhusu ukamataji holela na kushikiliwa kwa wanaharakati, waandishi wa habari na wapinzani.

"Kati ya sheria nyingi ambazo zimezuia haki ya raia mitandaoni na nje ya mtandao katika miaka ya hivi karibuni, Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 3) ya 2020 inaminya wigo wa kufungua kesi za ukandamizwaji wa haki za binaadamu... kubinywa zaidi kwa haki za binadamu kunaweza kusababisha athari mbaya, na amehimiza hatua za haraka na endelevu kuzuia hali hii," ameeleza Bi Bechelet.

Bechelet ametoa wito kwa Serikali kusimamia haki za wakimbizi wote, na kuhakikisha kuwa kurudi kwa wakimbizi kunasimamiwa kwa usalama, kwa heshima na kwa hiari.

Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 3) ya 2020 ulipitishwa na Bunge la Tanzania mwezi Juni na baadaye kusainiwa kuwa sheria na rais John Magufuli. ikiwemo kuwapa kinga ya viongozi wakuu akiwemo rais dhidi ya kushtakiwa kwa madai ya kuvunja katiba na sheria.

Kati ya mabadiliko hayo yaliyopitishwa, maeneo mawili yalizua mjadala na kupingwa vikali na wanaharakati wa haki za binaadamu na vyama vya upinzani.

Eneo la kwanza ni la viongozi wakuu wa mihimili ya dola, ambao ni Rais, Makamu wa Rais, Jaji Mkuu, Spika na Naibu Spika kushtakiwa kwa kuvunja sheria na katiba wakiwa madarakani. Kwa mujibu wa sheria hiyo, sasa atakayeshtakiwa kwa niaba ya viongozi wote hao ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Eneo la pili ni kuminywa kwa wigo wa kufungua kesi za kikatiba, kabla ya sheria hiyo kupitishwa, mtu yeyote alikuw na uhuru wa kwenda mahakamani na kufungua kesi ya kikatiba pale anapoona jambo fulani hususani la ukiukwaji wa haki za binaadamu linafanyika kwa mujibu wa sheria. Hivi sasa, inahitajika mtu kuwa na maslahi ya moja kwa moja ama kuathirika moja kwa moja na sheria husika kabla ya kufungua kesi.

Hoja za serikali ya Tanzania.

Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Palamagamba Kabudi ameiambia BBC kwamba wamepokea ripoti hiyo kwa mshangao mkubwa na kuongeza kwamba kamishena huyo angelikuwa Tanzania hangeliandika maneno kama hayo au kutoa tathmini aliyoitoa.

''Kwanza tumechukua hatua ya leo kwamba balozi wa Tanzani katika Umoja wa Mataifa katika ofisi ya Genive anawasilisha majibu yetu rasmi kuhusu taarifa hiyo aliyoitoa'' alisema Bwana Kabudi.

Pia aliongeza kuwa hali halisi nchini Tanzania ni tofauti na yale aliyosema Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet akiangazia hali ya siasa kipindi hiki cha uchaguzi.

''Sasa tuko katika uchaguzi mkuu tunao wagombea nafsi ya urais 17 na wote wanafanya mikutano yao nchi nzima kila sehemu na hakuna aliyezuiliwa kufanya mikutano ''anasema'' kweli kwa wengine ni mshangao''.

Awali akizungumza wakati muswada wa sheria hiyo ukipitishwa Bungeni, Mwanasheria Mkuu wa Tanzania, Profesa Adelardus Kilangi alisema mabadiliko hayo hayataondoa dhana ya kupata suluhu.

"Lengo la kufungua kesi hizi ni kupata suluhu, hivyo hata akishtakiwa mwanasheria mkuu bado suluhu itapatikana mahakamani kisheria."

Kwa mujibu wa Profesa Kilangi, hata sasa kwenye kesi zote ambazo serikali inashtakiwa ama hata kesi za ubunge bado mwanasheria mkuu anasimama mahakamani.

"Lengo la marekebisho haya pia ni kuwa na maudhui ya dhana ya kinga dhidi ya Rais ambayo ni kulinda hadhi ya Rais na nafasi yake," amesema pia Profesa Kilangi.

Kuhusu haki ya mtu yoyote kufungua mashtaka ya haki za ukiukwaji wa haki za binadamu, amesema kuwa Katiba inaelekeza kuwa kutakuwa na utaratibu wa kufuatwa utakaowekwa kisheria.

"Hapa hatukiuki katiba, tunaweka utaratibu wa kisheria…hili suala la nani ahusike katika kufungua mashtaka haya (locus standi) ni mjadala mpana.

Tunasema yule ambaye mwenye maslahi ya moja kwa moja ndiyo afungue mashtaka. Hata Mahakama ya Haki za Binadamu ya Ulaya imeweka wazi msimamo wake kuwa lazima uwe umeathirika moja kwa moja ndiyo ufungue mashtaka katika mahakama hiyo."
UN ndio iliyosaidia Tanzania kuupata Uhuru wake kutoka kwa wakoloni, hivyo haiwezekani kuwa UN inadanganya na kukurupuka tu kama tunavyotaka kuiambia UN. Kudhani hivyo ni kulitakia Taifa mabaya bila sababu za msingi. Mfano, inakuwaje wagombea wa upinzani tu Bara na Zanzibar ndio tu waliongenguliwa kugombea? duniani hakuna bahati mbaya ya hivi. Hii ni moja kwa moja kuna munipulation.
 
Back
Top Bottom