Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Mitandao kutumika vibaya kwenye taarifa nyeti kunatokana na yafuatayoUmoja wa Mataifa(UN) umesema taarifa zisizo sahihi kuhusu chanjo ya #COVID19 kunarefusha muda ambao ungetumika kudhibiti maambukizi ya Corona.
UN wametoa wito kwa raia kuhakiki taarifa kabla ya kusambaza taarifa hizo kwa wengine ambazo zinaathiri mapambano dhidi ya Corona.
Wamesema taarifa za mtandaoni husambaa kwa kasi ya moto wa nyikani, taarifa ndogo ya kupotosha huweza kuleta madhara makubwa.
View attachment 1885972
Ni kweli kabisa, mitandao inatumika vibaya sana, kuasi cha kuathiri malengo,
Sasa tuje kwa ambao tumeshachanja,
Tunaomba tupatiwe uthibitisho kwa kuwa kuna baadhi ya miji tukienda kwenye ofisi zao huhitaji huo uthibitisho au upime ndio uingie, sasa hili ni tatizo kwa ambao tumepata jab tayari na ni waaafiri wa mara kwa mara