Ndio maana nilikuambia kwamba unakariri tu kwa chuki zako, huna 'facts'. Eti Kenya haijafanikisha operation hata moja Somalia? Sasa hivi kusini mwa Somalia kuna amani, kisa vikosi vya Kenya. Kenya ilifanikiwa kuuteka mji wa Kismayu, mji ambao haukuwa umedhibitiwa na vikosi vyovyote vya kigeni, tangia enzi za wazee wa Ndemi na Mathati.
Leo hii eneo la Jubaland, nchini Somalia, limeanza kunawiri na kupata maendeleo ya kweli, kwasababu ya vikosi vya kijeshi vya Kenya. Kuhusu hizo mission zingine ulizozitaja sidhani kama kuna nchi nyingine ukanda huu, ambayo imekuwa na ufanisi mkubwa zaidi ya Kenya. Kumbuka kwamba Kenya sasa hivi ina vikosi vyake DRC, kabla ya hiyo S.Sudan. Ndio hii orodha ya mission zote ambazo vikosi vya Kenya vimehusika. Kutoka Bosnia, East Timor hadi Cambodia.