UN - Tusidanganyane, kama Taifa Tulipwaya

Tanzania ilishapoteza ushawishi iliyokuwa nayo enzi hizo, siku hizi imebaki tu "One of those shithole countries with no any international influence famous only for human rights abuses".

Kutambua tulipo na kufahamu tulipoangukia ni hatua njema sana ya kujinasua.

Eeh mola wetu utufukuzilie mbali pepo wetu huyu mbaya wa kujidanganya anayetufumba macho na masikio tusione wala kusikia maonyo hata ya binadamu wenzetu waliotutangulia mno:

Tutayasikia ya manabii wako kweli?
 
Nakubaliana na mleta uzi. Naomba muitafute hotuba ya mama Waziri Mkuu wa Barbados muone mfano halisi wa tulichotakiwa kufanya na sisi.
 
Ya Adamoo, Kingai, Mahita na mwenzao tumeyasikia:

View attachment 1952725

Fikiria nchi inayofanya komando wake aliyeipigania hivi.

Abuse of human rights, lack of democracy, use of iron fists to suppress dissenting opinions, rigging of elections, etc qualify a country - a Shit hole.

Shit holes are real, neither mindsets nor illusions.
Halafu kiongozi wa hii nchi anajisifu kutoa hotuba UN akidhani anao wahutubia hawajui kumbe wanamchora tu, ndio maana VP wa US naskia amegoma kuonana nae
 
Kuna haja ya kuambiana ukweli. Kama taifa UN hatukufurukuta.

Siyo siri, madhumuni ya mkutano ule ilikuwa ni kwa mataifa kuweka wazi sera zao za nje zenye kuelezea maingiliano baina ya nchi na nchi.

Mkutano ule haukuwa wakutafutia wawekezaji, kutangazia utalii wala kuhusiana na mambo ya ndani ya nchi.

Badala yake tukatumia muda kujielekeza kwenye mambo ya kijinsia. Kwani tulivisahau vyuma vilivyo tikisa dunia hii wakiwamo akina Angel Merkel, Thatcher, Indira Gandhi, Golda Meir, nk?

Usawa wa kijinsia katika mataifa nje ya Africa si agenda za kupeleka UN labda AU. Huko waungwana walikwisha toka zamani. Mama Clinton alikuwa achukue urais wa dunia na wala si kwa kudra za Mola.

Taarifa za Corona tulizosoma ni za WHO ambayo ni agency tanzu ya UN yenyewe.

Kwamba tuna ushauri kuhusu chanjo ya Corona ambayo aghalabu tungetaka hata copyright kwenye chanjo isiwepo wakati tunapewa bure?

Hatuna neno lolote kuhusu nyungu, maombi, mikaratusi, michai chai, malimao au hata na matango pori mengine?

Hatuna neno lolote kuhusiana na vita vya kiuchumi hasa hasa mabeberu dhidi ya Tanzania?

Hatuna neno kumhusu beberu yeyote na upigaji wake kwenye chanjo, barakoa, PPE au kuhusu Corona kwa ujumla?!

Kwani dunia haikupata kutusikia na misimamo yetu na shujaa wetu wanayeshuku Corona haikumnusuru?

Kwani zile takwimu za ugonjwa wa Corona ambazo dunia imekuwa ikituasa kuzitoa tumewahi kuzitoa?

Tupitieni hotuba za wengine kulinganisha na ya kwetu.

Ama kwa hakika hatukufua dafu!

Sera yetu ya mambo ya nje HAIJABADILIKA SANA......

Yako maeneo tumeamua KUGEUKA....mfano kufungua BALOZI nchi ambazo tulikuwa kinyume nazo mfano Israel.....

Dunia imebadilika sana....hatuwezi kung'ang'ania misimamo ya kizamani.....

Mathalani tumeona Marekani ikiwaachia nchi Taliban pamoja na kupigana nao miaka 20...pamoja na Taliban kutoendana na DEMOKRASIA YA MAGHARIBI.....

Juma lijalo Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan anakutana na Rais wa Urusi Komredi Putin kuhusiana na kiitwacho UHUSIANO NA UKURASA MPYA kinyume na wa zamani(kambi ya NATO).....

Hapa pia tusisahau kuwa pamoja na Uturuki kuwa ndani ya NATO bado Marekani inawasapoti waasi wa KIKURDI....na ule Upande mwingine Pakistan iliyo rafiki na Marekani iko pamoja na China iliyo kinyume na mahasimu wao India......

Kwa ufupi kabisa DUNIA INABADILIKA KILA UCHAO na TANZANIA HAIFUNGAMANI NA UPANDE WOWOTE.....

#SiempreJMT
#NchiKwanzaKablaYaUhaiWetu
 
Tanzania ilishapoteza ushawishi iliyokuwa nayo enzi hizo, siku hizi imebaki tu "One of those shithole countries with no any international influence famous only for human rights abuses".
Enzi za kuwa na misimamo ya KIKOMUNISTI eee?!!
Si ndio eee?!!!

#SiempreJMT
#NchiKwanza
 
Kuna haja ya kuambiana ukweli. Kama taifa UN hatukufurukuta.

Siyo siri, madhumuni ya mkutano ule ilikuwa ni kwa mataifa kuweka wazi sera zao za nje zenye kuelezea maingiliano baina ya nchi na nchi.

Mkutano ule haukuwa wakutafutia wawekezaji, kutangazia utalii wala kuhusiana na mambo ya ndani ya nchi.

Badala yake tukatumia muda kujielekeza kwenye mambo ya kijinsia. Kwani tulivisahau vyuma vilivyo tikisa dunia hii wakiwamo akina Angel Merkel, Thatcher, Indira Gandhi, Golda Meir, nk?

Usawa wa kijinsia katika mataifa nje ya Africa si agenda za kupeleka UN labda AU. Huko waungwana walikwisha toka zamani. Mama Clinton alikuwa achukue urais wa dunia na wala si kwa kudra za Mola.

Taarifa za Corona tulizosoma ni za WHO ambayo ni agency tanzu ya UN yenyewe.

Kwamba tuna ushauri kuhusu chanjo ya Corona ambayo aghalabu tungetaka hata copyright kwenye chanjo isiwepo wakati tunapewa bure?

Hatuna neno lolote kuhusu nyungu, maombi, mikaratusi, michai chai, malimao au hata na matango pori mengine?

Hatuna neno lolote kuhusiana na vita vya kiuchumi hasa hasa mabeberu dhidi ya Tanzania?

Hatuna neno kumhusu beberu yeyote na upigaji wake kwenye chanjo, barakoa, PPE au kuhusu Corona kwa ujumla?!

Kwani dunia haikupata kutusikia na misimamo yetu na shujaa wetu wanayeshuku Corona haikumnusuru?

Kwani zile takwimu za ugonjwa wa Corona ambazo dunia imekuwa ikituasa kuzitoa tumewahi kuzitoa?

Tupitieni hotuba za wengine kulinganisha na ya kwetu.

Ama kwa hakika hatukufua dafu!
Jiandae kumwagiwa mvua ya matusi na waunga juhudi wapya

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Kazi ipo
Nakubaliana na mleta uzi. Naomba muitafute hotuba ya mama Waziri Mkuu wa Barbados muone mfano halisi wa tulichotakiwa kufanya na sisi.

Huyu ni wa kupigiwa mfano:

"Who will stand up and rise up and fight for the rights of the people?" Bob Marley
 
Sera yetu ya mambo ya nje HAIJABADILIKA SANA......

Yako maeneo tumeamua KUGEUKA....mfano kufungua BALOZI nchi ambazo tulikuwa kinyume nazo mfano Israel.....

Dunia imebadilika sana....hatuwezi kung'ang'ania misimamo ya kizamani.....

Mathalani tumeona Marekani ikiwaachia nchi Taliban pamoja na kupigana nao miaka 20...pamoja na Taliban kutoendana na DEMOKRASIA YA MAGHARIBI.....

Juma lijalo Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan anakutana na Rais wa Urusi Komredi Putin kuhusiana na kiitwacho UHUSIANO NA UKURASA MPYA kinyume na wa zamani(kambi ya NATO).....

Hapa pia tusisahau kuwa pamoja na Uturuki kuwa ndani ya NATO bado Marekani inawasapoti waasi wa KIKURDI....na ule Upande mwingine Pakistan iliyo rafiki na Marekani iko pamoja na China iliyo kinyume na mahasimu wao India......

Kwa ufupi kabisa DUNIA INABADILIKA KILA UCHAO na TANZANIA HAIFUNGAMANI NA UPANDE WOWOTE.....

#SiempreJMT
#NchiKwanzaKablaYaUhaiWetu

Mkuu nondo za Tanzania ya kina mzee Nyerere (rip) ni kama hizi hapa:

"Who will stand up and rise and fight for the rights of the people?" Bob Marley.

Who ..? Who ..? ......... Who?

Kwamba hatuja nyembuka nyembuka? Mbona itakuwa ni kujifariji tu?
 
Halafu kiongozi wa hii nchi anajisifu kutoa hotuba UN akidhani anao wahutubia hawajui kumbe wanamchora tu, ndio maana VP wa US naskia amegoma kuonana nae

We were totally out of place
 
Change your mindset,Tanzania is not a shithole country,may be your mind has full of darkness,I welcome you to the light.
Everyone is entitled to his own opinion. You can't dictate anyone's mindset.
 
This world is beautiful. Full of all varieties. Above all, including the idiots 😂😂.

Hiiiiii bagosha!
 
Back
Top Bottom