Mwanamwana
Platinum Member
- Aug 1, 2011
- 9,604
- 22,722
Ripoti mpya ya UN Women yenye kichwa "Chukua Hatua Sasa Kukomesha Ukatili Dhidi ya Wanawake" imebaini kuwa asilimia 70 ya wanawake walioshiriki utafiti wamewahi kukumbana na ukatili wa mtandaoni wakati wa kutekeleza majukumu yao. Aidha, asilimia 41 walisema unyanyasaji huo uliendelea hadi nje ya mtandao, ambapo walishambuliwa au kudhuriwa kutokana na matusi na manyanyaso ya kidijitali
Soma Pia: Unyanyasaji wa kijinsia mtandaoni unawanyima Watu wengi kupata fursa zilizoko huko mtandaoni
Ripoti hiyo ilizinduliwa jijini Geneva, Uswisi, na imeandaliwa na Tume ya Ulaya na UN Women kwa ushirikiano na TheNerve, City St George's, University of London, Kituo cha Kimataifa cha Waandishi wa Habari (ICFJ) na UNESCO.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, ukatili wa mtandaoni unawafanya wanawake wengi kujiondoa kwenye majukwaa ya kidijitali, jambo linalopunguza ushiriki wao katika mijadala ya umma na kuhatarisha uhuru wa kujieleza pamoja na misingi ya demokrasia. Kutokana na hali hiyo, UN Women inasisitiza umuhimu wa kuwa na sheria madhubuti, uwajibikaji wa kampuni za teknolojia na ulinzi zaidi kwa wanawake wanaoshiriki mijadala ya umma.
Ripoti pia inaonyesha kuwa madhara ya ukatili wa mtandaoni yanaendelea kuongezeka nje ya mazingira ya kidijitali. Kwa waandishi wanawake, matukio ya madhara ya nje ya mtandao yanayotokana na mashambulizi ya mtandaoni yameongezeka kutoka asilimia 20 mwaka 2020 hadi asilimia 42 mwaka 2025.
Sarah Hendricks wa UN Women amesema takwimu hizo zinaonyesha kuwa ukatili wa kidijitali ni tishio halisi linalowaathiri wanawake katika maisha yao ya kila siku. Amesema wanawake wanaoripoti habari, kutetea haki za binadamu au kuongoza mijadala ya kijamii hulengwa na mashambulizi yanayolenga kuwanyamazisha, kuwaaibisha na kuwaondoa kwenye mijadala ya umma, huku baadhi ya vitisho hivyo vikihama kutoka mtandaoni hadi kwenye maisha halisi.
Ripoti hiyo pia inaonya kuwa matumizi mabaya ya akili mnemba (AI) yanazidisha tatizo hilo. Inaeleza kuwa karibu mwanamke mmoja kati ya wanne miongoni mwa waandishi wa habari, wanaharakati na watetezi wa haki za binadamu amewahi kukumbana na ukatili unaowezeshwa na AI, ikiwemo matumizi ya deepfakes na maudhui yaliyobadilishwa. Aidha, watayarishaji wa maudhui na washawishi wanaojihusisha na masuala ya haki za binadamu ni miongoni mwa makundi yanayolengwa zaidi.
UN Women imetoa wito wa kuimarishwa kwa sheria na sera za kukabiliana na ukatili unaotumia teknolojia, kuongeza uwajibikaji wa kampuni za teknolojia, kuimarisha ulinzi kwa waathirika na kuwekeza zaidi katika utafiti na takwimu ili kuandaa sera zinazotegemea ushahidi. Pia imetangaza kuwa itazindua mkakati mpya wa kuzuia na kukabili ukatili wa kijinsia unaowezeshwa na teknolojia.
Chanzo: Wanawake 7 kati ya 10 wanakumbana na ukatili mtandaoni: UN