UN yaitaka Urusi iondoe wanajeshi wake Ukraine

UN yaitaka Urusi iondoe wanajeshi wake Ukraine

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa(UN), Antonio Guterres amemtaka Rais wa Urusi, Vladmir Putin kurudisha wanajeshi wake aliwapeleka Ukraine

Guterres ameandika ujumbe huo katika ukurasa wake wa Twitter ambapo katika ujumbe mwingine aliandika watu wengi wameshafariki kutokana na mzozo unaoendelea kati ya Urusi na Ukraine.

Aidha Rais wa Marekani, Joe Biden amesema Urusi itabeba lawama kwa madhara yatakayotokea katika mzozo uliopo. Marekani na washirika wake watajua cha kufanya.

Screenshot 2022-02-24 at 09-12-53 António Guterres ( antonioguterres) Twitter.png

Screenshot 2022-02-24 at 09-11-13 President Biden on Twitter.png
 
Mbona kelele Kama hizi huwezi sikia pale USA na washirika wake wakivamia nchi za watu mfano Libya, Iraq nk kafanya Urusi basi Mambo ya humanity yameanza ,UN ni Kama mbwa Koko tu
All people are equal, but some are more equal than others
 
Vipi kuhusu matendo ya hao mnao waita wapenda demokrasia wa Magharibi na USA kwa Syria,Libya, Iraq nk
Putin amerukwa na akili, kwa dunia ya sasa ni aibu kwa taifa kubwa kama Urusi kufanya hiki kinachoendelea huko Ukraine.

Raia wa Urusi ni lazima wachukue hatua ya kukataa kutawaliwa na mgonjwa wa akili.
 
Putin amerukwa na akili, kwa dynia ya sasa ni aibu kwa taifa kubwa kama Urusi kufanya hiki kinachoendelea huko Ukraine.

Raia wa Urusi ni lazima wachukue hatua ya kukataa kutawaliwa na mgonjwa wa akili.
Putin hawezi kubali silaha ziwekwe mlangoni kwake. Yupo tayari kwa lolote lakini sio kuwekewa silaha dirishani.
Ukraine kashaingizwa cha kike na hana msaada wowote zaidi ya vikwazo ambayo havina madhara kwa Russia.
 
Putin amerukwa na akili, kwa dunia ya sasa ni aibu kwa taifa kubwa kama Urusi kufanya hiki kinachoendelea huko Ukraine.

Raia wa Urusi ni lazima wachukue hatua ya kukataa kutawaliwa na mgonjwa wa akili.
Ila si aibu kwa marekani na ulaya sio, mlifurahi ilipopigwa Libya eeee
 
Back
Top Bottom