Safi Sana Russia[emoji4][emoji106]
Ni kweli Urusi ina Nguvu kubwa Sana za Kijeshi Tena Sana. Lakini hawezi hata siku moja kuthubutu kutumia kombola la Nyuklia kwenye Vita. Kombola la Nyuklia ni kwa ajili ya Duterrence(Kutishia). Kinachosababisha mpaka Sasa NATO washindwe Kuingia vitani kuisaidia Ukraine ni kwasababu Russia ana Nyuklia Waepons ambazo zikitumika Basi NO WINNER,All are LOSSERS.
Urusi ina Makombora 7500 ya Nyuklia kwa takwimu za NIT. Makombora 2500 yako tayari kufyatuliwa kuelekea Endeo lolote Lile Duniani litakapotumwa. Marekani ina Miji mikubwa 358 na Majimbo 54. Kombora Moja linaugeuza mji kuwa Majivu kabisa. Kama Mrusi akituma Makombora yote 2500 kuelekea Marekani,Basi ndani ya dakika 30 hakutakuwa na USA Duniani.
Kwa Upande Mwingine,Marekani ina Makombora ya Nyuklia 6800. Kati ya hayo, 3500 yako tayari kufyatuliwa ndani ya Dakika 5 wakipokea Order na Direction ya kuyafurumusha. Urusi ina Miji mikubwa 43. Endapo USA akiona Russia kashatuma Makombora Yake kuelekea Marekani na hakuna jinsi Basi ndani ya Dakika 5, Makombora 3500 ya Marekani yatakuwa njiani kuelekea Urusi kuteketeza Miji 43,Ndani ya Nusu saa hakutakuwa na Urusi Tena. Hiyo inaitwa MUTUAL ASSURED DESTRUCTION(MAD).
Haya Sasa,Tuseme wewe ni Raisi wa Russia,utarusha hayo Makombora kuelekea Marekani au utafanya juhudi za majadiliano?
Mwishoni mwa Vita baridi kabisa (1988) Nchi za Marekani na Urusi Zilikuwa na Akiba ya Makombora 127,000 (Laki moja na elfu ishirini na Saba). Kati ya hayo, 58,000 ya Urusi na 69,000 ya USA. Embu fikilia. Kombora Moja linafuta mji mmoja wa Dar. Je,Dunia ina Miji 127,000? Jibu ni Hapana.
Kwahiyo ndugu yangu usiwe na tempa unapokuwa unachangia hizi maada,tumia Logic utaelewa tu.
Urusi na Marekani wanajuana,wakikutana Anga Furani Kila mmoja anaangalia Nani anamaslahi makubwa na anamwachia ili kuepusha Vita.
Georgia Mwaka 2008 Marekani hakuingiza mguu kusaidia Nchi hiyo dhidi ya Uvamizi wa Russia kwasababu Marekani anajua hapo Russia ana maslahi Makubwa.
Iraq mwaka 2001 Russia hakutia Mguu kwasababu Marekani alikuwa na Maslahi Makubwa.
Libya mwaka 2011 Russia hakutia Mguu kwasababu USA alikuwa na Maslahi Makubwa.
Venezuera Marekani aliogopa Msululu wa wakimbizi kumiminika nchini Marekani hata Kama angeliamua Vita Urusi angelipisha Coz pale ni Maslahi Makubwa ya kiusalama kwa USA.
Syria pale Wote Urusi na USA wanamaslahi na ndio maana mpaka Sasa wameigawana kijanja. Urusi inamhitaji Assad kwasababu Anamdai pesa ndefu. Marekani anahitaji Mafuta ndio maana mpaka leo Majeshi ya Marekani yapo Syria kulinda Visima vya Mafuta.
Kuhusu Ukraine,hata Marekani anajua kabisa Maslahi ya Urusi ni Makubwa kwahiyo lazima akae pembeni. Atashiriki tu kijanja lakini sio moja kwa moja.
MTz 255Dar.