Una beti upate hela ama kufurahisha nafsi.. Kama unataka upate hela niige mimi mshindi wa Perfect 12

Guyz hayo mambo nifundisheni nalizwa daily
Kwa sasa sio wakati mzuri wa kutupia mzigo maana ligi nyingi zimefika tamati na hata zilizobaki hazina ushindani unaoeleweka maana baadhi ya timu zimeshabeba ubingwa na zinazoshuka daraja zimeshajijua. Mikeka mitamu wakati ligi zipo katikati huko ulaya
 
Mkuu wewe noma, kiukweli sijawahi fikiria kucheza mchezo wowote ule unao husu fedha
 
Aaaah, nilidhani nilipokuona huku upo active kwenye hii mikeka, sijawahi ila kuna mtu ananishawishi sana.
Mkuu mm naomba usijiingize kwenye hizo mambo
 
[emoji134]
 
Wacha ni subscribe. Kuna jambo la kuvutia naliona na nitajifunza kitu.
Miaka ya mwanzo wa2000 nikiwa chuo kikuu nilicheza sana kamari za soka (hazikuwapo online betting au mitandao ya betting mingi, kiuwazi na kiurahisi hivi). Ilikua ni zile bet za papo kwa papo, mtu na mtu. Tonge-nyama inaitwa.
Asikuambie mtu, kamari ni addictive vibaya sana. Mbaya zaidi mimi niliendeshwa na mapenzi ya timu yangu; Man u (international) na Simba (local). Nilibet mara nyingi kwamba timu yangu inashinda. It wasn't proffesional betting kwakweli.
Mwanzo mambo yalienda sawa ila baadae mambo yaliniharibikia vibaya sana. Shida ikawa nimeshakua addicted. Ilinilazimu jasho, machozi na damu kuondoka kwenye kamari. Ilinilazimu pia kuacha kushabikia na kufuatilia mpira ili nibadili mwendo wa maisha yangu. Nilishakua aibu mbele ya jamii yangu na hakuna cha maana nilipata zaidi ya kugeuka "teja" kabisa wa kamari.
Nashukuru kwa msaada wa ndugu na marafiki na Mungu mwenyewe niliondoka kwenye maisha yale.
Of recently nimekua tena interested hasa na hizi betting za kisasa. Nashawishika kwelikweli ninapoona vijana wanakamata millions hivi hivi (shida hizi za maisha zinasukuma vibaya jamani). Natamani nibet na mimi. Ila kisasa, ki-proffesional, oriented, kwa kiasi, hekima na maarifa. I am attempted sana sana.
Hapa napitia shuhuda za wachangiaji nijifunze. Niingie informed au niache tamaa nilinde hata kidogo nilicho nacho.
 
Jibu zuri sana
 
ila watu mitaji wanayo maisha si magimu km watu wanavyo fikiria km una bisha piga hesabu tangu uanze kubet umetumia kias gani


Jumla nimetumia kama laki mbili na ushee hivi...
Niulize sasa nimeingiza pesa kiasi gani....
Faida zaidi ya mara 5000 mzee...
 
Sikumbuki lakini nakumbuka sheria ya adhabu ( PENAL CODE ) ya Tanzania kuna kifungu kinakataza GAMBLING sasa hawa watu wanaosambaza vimashine vyekundu vinavyotafuna akili na fedha za watanzania kibali wanapewa na nani?
 
Hapa duniani kila MTU anapaswa aishi apendavyo.

Ukisoma kwenye rules zao wanakwambia DO NOT STAKE WHAT YOU CANNOT AFFORD TO LOSE.
Hayo maneno ni sawa sawa na yale yalioandikwa kwenye sigara " UVUTAJI WA SIGARA NI HATARI KWA AFYA YAKO" ukishakuwa adicted huyafuati hata kidogo. Hata kwenye betting kama zilivyo kamari nyingine, ukishakuwa adicted au umeliwa hela yako unaweza kumaliza akiba yako yote ukitaka kukomboa iliyoliwa kumbe ndio unaendelea kuteketea
 
Ligi ikianza nitakutafuta
 
Kwa kuwa hujiwezi ndio upuuzi?

Mimi MkekaBet ndio wanaonilipia petrol. Kwa shilingi 15,000 napata hadi 230,000 kutegemeana na wikiendi ina timu gani. Hivi sasa ligi nyingi zimefikia ukingoni, naona sasa safari zangu zitaanza kuwa limited.



hela yangu ya siku ni yako kubet mwez siwez fanya biashara ya kubatisha.

sijakulazimisha uwe kama mimi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…