Una beti upate hela ama kufurahisha nafsi.. Kama unataka upate hela niige mimi mshindi wa Perfect 12

Una beti upate hela ama kufurahisha nafsi.. Kama unataka upate hela niige mimi mshindi wa Perfect 12

Guyz hayo mambo nifundisheni nalizwa daily
Kwa sasa sio wakati mzuri wa kutupia mzigo maana ligi nyingi zimefika tamati na hata zilizobaki hazina ushindani unaoeleweka maana baadhi ya timu zimeshabeba ubingwa na zinazoshuka daraja zimeshajijua. Mikeka mitamu wakati ligi zipo katikati huko ulaya
 
Usiganganye watu.

1. Hakuna bingwa wa kubeti kwa ni kila timu inayoingia kwenye mchezo inataka kushinda ama kutoshindwa (bila kujali odd zilizotolewa)

2. Hana timu dhaifu kwani matokeo haumuliwa na dakika tisini hivyo usiidharau sana timu ukaishiwa kuliwa hela zako ( kama unataka majibu kama ulivyobeti nenda kwenye hizo timu ukacheze wewe ulazimishe matokeo utakavyo)

3. Suala la kubeti timu chaeche ama nyingi risk ya kuliwa ipo pale pale

4.Unapobeti timu chache maana yake odd nazo ni chache kwa maana nyingine lazima uweke hela kubwa , na haimaanishi kwa kuwa umeweka hata timu moja basi hutoliwa

5. Mfano wa timu 3 za over 2.5 ulizocheza kwa 30,000/= nikiangalia odd zake hazizidi hata 7 na ni moja wapo ya option ambayo ina risk kubwa sana kupotea, ukirudia tena hata mara 10 yamkini ukabahatisha mara 1 tuu, na ndio chance uliyokutana nayo na usijione bingwa sana

6. Tofauti ya mtu anayebeti timu nyingi na chache ni kwamba yule anaye beti timu chache anapoteza fedha nyingi sana katika ku bet na kama ni mfanya biashara jiandae kufilisika, lakini huyo anayebiti timu nyingi anakusanya odd nyingi kwa hela kidogo na akibahatisha mara moja hata kwa miaka 5 anakuwa ametoka kama wewe ulivyobahatisha hiyo perfect 12

7.Huu ni moja kati ya mchezo hatari sana na ningekuwa na mamalaka ningefukuza makampuni yote ya kubeti na kufungia mitandao yote ya online betting Tanzania kwa kuwa inazalisha Taifa maskini, watu hawataki kufanya kazi wanatarajia miujiza, wanafunzi wanaliwa ada, wazazi wanaliwa hela za kutunza familia, wafanyabiashara wanafilisika, watumishi wa Umma hawaridhiki na mishahara kwani wanazipeleka huko, watu hawafanyi kazi ngumu kutwa kucha wanatembea na vikaratasi mfukoni,

8. Bunge lipiteshe sheria ya dharura kuzuia mchzo huu haramu ambao unashusha thamani ya shilingi kwa kasi, sijui wachumi wako wapi, sijui wizara ya fedha inasema nini kuhusu hili, hali ni mbaya zaidi ya maelezo, kampuni zinazidi kuongezeka bongo kuja kuchota hela za bure, kwa siku watu wanaliwa zaidi ya bilioni moja na mshindi wa kupata kama ulizozipata waweza kupata baada ya miezi hata minne.

9. Say no to betting
Mkuu wewe noma, kiukweli sijawahi fikiria kucheza mchezo wowote ule unao husu fedha
 
Aaaah, nilidhani nilipokuona huku upo active kwenye hii mikeka, sijawahi ila kuna mtu ananishawishi sana.
Mkuu mm naomba usijiingize kwenye hizo mambo
 
Usitudanganye

Moja mshindi hapewi kiasi chote alichoshinda maana kuna kodi ndani yake hivyo kutuaminisha kuwa uneshinda milioni 109 na kuzipata zote hiyo ni moja wapo ya uongo....

Kule kwenye jukwaa letu ulisema kuwa malipo yanafanyika kwa benki 3 yaani Exim, Crdb na Dcb.
Ukasema tena kuwa umeshafungua acc exim jana

Leo unasema kuwa umepewa checque iliyoandikwa 109mil

Leo unatuambia kuwa unaenda chukua hela...

Kwa nijuavyo checque ikishazidi 1mil kama wewe sio mmliki wa account au signatory basi hiyo hela hutapewa zaidi utaambiwa udeposit checque


Hadi hapo nahitimisha kuwa wewe si mahindi wa zile hela

Wewe ni muongo



Bet What You can Afford to Lose
Bet Responsibly
[emoji134]
 
Wacha ni subscribe. Kuna jambo la kuvutia naliona na nitajifunza kitu.
Miaka ya mwanzo wa2000 nikiwa chuo kikuu nilicheza sana kamari za soka (hazikuwapo online betting au mitandao ya betting mingi, kiuwazi na kiurahisi hivi). Ilikua ni zile bet za papo kwa papo, mtu na mtu. Tonge-nyama inaitwa.
Asikuambie mtu, kamari ni addictive vibaya sana. Mbaya zaidi mimi niliendeshwa na mapenzi ya timu yangu; Man u (international) na Simba (local). Nilibet mara nyingi kwamba timu yangu inashinda. It wasn't proffesional betting kwakweli.
Mwanzo mambo yalienda sawa ila baadae mambo yaliniharibikia vibaya sana. Shida ikawa nimeshakua addicted. Ilinilazimu jasho, machozi na damu kuondoka kwenye kamari. Ilinilazimu pia kuacha kushabikia na kufuatilia mpira ili nibadili mwendo wa maisha yangu. Nilishakua aibu mbele ya jamii yangu na hakuna cha maana nilipata zaidi ya kugeuka "teja" kabisa wa kamari.
Nashukuru kwa msaada wa ndugu na marafiki na Mungu mwenyewe niliondoka kwenye maisha yale.
Of recently nimekua tena interested hasa na hizi betting za kisasa. Nashawishika kwelikweli ninapoona vijana wanakamata millions hivi hivi (shida hizi za maisha zinasukuma vibaya jamani). Natamani nibet na mimi. Ila kisasa, ki-proffesional, oriented, kwa kiasi, hekima na maarifa. I am attempted sana sana.
Hapa napitia shuhuda za wachangiaji nijifunze. Niingie informed au niache tamaa nilinde hata kidogo nilicho nacho.
 
Adanganye asidanganye poa tu, yeye kaelezea starehe yake, hata wewe unazo, betting ni starehe na kufaidika, kwako sio starehe, labda utataka uzikwe na mali zako kitu ambacho hakiwezekani hata kidogo, kaja duniani kapata mali na fedha zake, wacha azitumie atakavyo bila kuvunja sheria, wewe usiependa kaa pembeni fanya upendalo bila kuvunja sheria.
Usiingilie starehe za watu mkuu.
Jibu zuri sana
 
Hapa duniani kila MTU anapaswa aishi apendavyo.

Ukisoma kwenye rules zao wanakwambia DO NOT STAKE WHAT YOU CANNOT AFFORD TO LOSE.
411b53b1a6d9b8d438a3c391d8cd8cf0.jpg
 
ila watu mitaji wanayo maisha si magimu km watu wanavyo fikiria km una bisha piga hesabu tangu uanze kubet umetumia kias gani


Jumla nimetumia kama laki mbili na ushee hivi...
Niulize sasa nimeingiza pesa kiasi gani....
Faida zaidi ya mara 5000 mzee...
 
Adanganye asidanganye poa tu, yeye kaelezea starehe yake, hata wewe unazo, betting ni starehe na kufaidika, kwako sio starehe, labda utataka uzikwe na mali zako kitu ambacho hakiwezekani hata kidogo, kaja duniani kapata mali na fedha zake, wacha azitumie atakavyo bila kuvunja sheria, wewe usiependa kaa pembeni fanya upendalo bila kuvunja sheria.
Usiingilie starehe za watu mkuu.
Sikumbuki lakini nakumbuka sheria ya adhabu ( PENAL CODE ) ya Tanzania kuna kifungu kinakataza GAMBLING sasa hawa watu wanaosambaza vimashine vyekundu vinavyotafuna akili na fedha za watanzania kibali wanapewa na nani?
 
Hapa duniani kila MTU anapaswa aishi apendavyo.

Ukisoma kwenye rules zao wanakwambia DO NOT STAKE WHAT YOU CANNOT AFFORD TO LOSE.
411b53b1a6d9b8d438a3c391d8cd8cf0.jpg
Hayo maneno ni sawa sawa na yale yalioandikwa kwenye sigara " UVUTAJI WA SIGARA NI HATARI KWA AFYA YAKO" ukishakuwa adicted huyafuati hata kidogo. Hata kwenye betting kama zilivyo kamari nyingine, ukishakuwa adicted au umeliwa hela yako unaweza kumaliza akiba yako yote ukitaka kukomboa iliyoliwa kumbe ndio unaendelea kuteketea
 
Kwa sasa sio wakati mzuri wa kutupia mzigo maana ligi nyingi zimefika tamati na hata zilizobaki hazina ushindani unaoeleweka maana baadhi ya timu zimeshabeba ubingwa na zinazoshuka daraja zimeshajijua. Mikeka mitamu wakati ligi zipo katikati huko ulaya
Ligi ikianza nitakutafuta
 
Kwa kuwa hujiwezi ndio upuuzi?

Mimi MkekaBet ndio wanaonilipia petrol. Kwa shilingi 15,000 napata hadi 230,000 kutegemeana na wikiendi ina timu gani. Hivi sasa ligi nyingi zimefikia ukingoni, naona sasa safari zangu zitaanza kuwa limited.



hela yangu ya siku ni yako kubet mwez siwez fanya biashara ya kubatisha.

sijakulazimisha uwe kama mimi
 
Back
Top Bottom