Usiganganye watu.
1. Hakuna bingwa wa kubeti kwa ni kila timu inayoingia kwenye mchezo inataka kushinda ama kutoshindwa (bila kujali odd zilizotolewa)
2. Hana timu dhaifu kwani matokeo haumuliwa na dakika tisini hivyo usiidharau sana timu ukaishiwa kuliwa hela zako ( kama unataka majibu kama ulivyobeti nenda kwenye hizo timu ukacheze wewe ulazimishe matokeo utakavyo)
3. Suala la kubeti timu chaeche ama nyingi risk ya kuliwa ipo pale pale
4.Unapobeti timu chache maana yake odd nazo ni chache kwa maana nyingine lazima uweke hela kubwa , na haimaanishi kwa kuwa umeweka hata timu moja basi hutoliwa
5. Mfano wa timu 3 za over 2.5 ulizocheza kwa 30,000/= nikiangalia odd zake hazizidi hata 7 na ni moja wapo ya option ambayo ina risk kubwa sana kupotea, ukirudia tena hata mara 10 yamkini ukabahatisha mara 1 tuu, na ndio chance uliyokutana nayo na usijione bingwa sana
6. Tofauti ya mtu anayebeti timu nyingi na chache ni kwamba yule anaye beti timu chache anapoteza fedha nyingi sana katika ku bet na kama ni mfanya biashara jiandae kufilisika, lakini huyo anayebiti timu nyingi anakusanya odd nyingi kwa hela kidogo na akibahatisha mara moja hata kwa miaka 5 anakuwa ametoka kama wewe ulivyobahatisha hiyo perfect 12
7.Huu ni moja kati ya mchezo hatari sana na ningekuwa na mamalaka ningefukuza makampuni yote ya kubeti na kufungia mitandao yote ya online betting Tanzania kwa kuwa inazalisha Taifa maskini, watu hawataki kufanya kazi wanatarajia miujiza, wanafunzi wanaliwa ada, wazazi wanaliwa hela za kutunza familia, wafanyabiashara wanafilisika, watumishi wa Umma hawaridhiki na mishahara kwani wanazipeleka huko, watu hawafanyi kazi ngumu kutwa kucha wanatembea na vikaratasi mfukoni,
8. Bunge lipiteshe sheria ya dharura kuzuia mchzo huu haramu ambao unashusha thamani ya shilingi kwa kasi, sijui wachumi wako wapi, sijui wizara ya fedha inasema nini kuhusu hili, hali ni mbaya zaidi ya maelezo, kampuni zinazidi kuongezeka bongo kuja kuchota hela za bure, kwa siku watu wanaliwa zaidi ya bilioni moja na mshindi wa kupata kama ulizozipata waweza kupata baada ya miezi hata minne.
9. Hapo unataka kumaanisha watu kuwa kwa kuwa wewe umebahatisha , basi kila mtu acheze na atapata kiasi kama wewe, my friend you are wrong. Hata wewe mwenyewe ukirudia hizo option ulizopata unaweza kuanza mwanzo wa msimu mpaka mwisho kila siku unaliwa tuu na haijawahi kujirudia. Kumbuka wakati wewe umebahatisha hizo ni sehemu ya kiasi kidogo cha hela za watanzania wenzako zinazoliwa na huyo kanjubai kiulaini, na sasa mmeongezewa sport pesa, wachina nao wamesambaza madude mengine yanafanana na mashine za kutolea mafuta sheli zipo karibia kila baa, vibanda vya biashara vimefungwa na kufunguliwa ma TV yanayokimbiza mbwa kila kona , sasa hapo kuna uchumi???
10. Say no to betting