Una duka dogo la rejareja, mtaji ni mdogo na umezungukwa na maduka mengi na ushindani ni mkubwa?

Una duka dogo la rejareja, mtaji ni mdogo na umezungukwa na maduka mengi na ushindani ni mkubwa?

Hypolite

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2017
Posts
235
Reaction score
484
Maduka ya rejareja yanayouza vitu vinavyonunulika kwa haraka(Fast moving consumable goodsi.e sukar, ngano, sembe&N.k hua ni mengi sana mitaani tunamoishi na yamekaribiana yahitaji akili & mbinu zakufanya biashara kaitka mazingira ya namna hii.

Mtu mmoja aliwahi nambia ni heri afanyie biashara sehemu yenye ushindani na soko lina pesa (liquidity) kuliko kufanyia biashara eneo leny ushindani mdogo ila lisilo na pesa (illiquid market)

Yafuatayo ni mambo kadhaa uwezayo kufanya ukajiweka kweny nafasi nzuri yakuhakikisha unashindana vilivyo vyema na kuwa na kua na mzunguko mzuri wa pesa.

Epuka kufanya kijiwe sehemu ya biashara yako kwa gharama yeyote ile,
ushikaji na ushosti haupaswi kufumbiwa macho sehemu ya biashara na ukumbuke hili ukiwa muuzaji ni wa kike na mashosti hujaa kweny biashara yako kupiga stori basi tambua kabisa jinsia yakiume itakupita kama haioni kuna duka kwako nakwenda kununua fremu inayofuata vivyo hivyo kwa muuzaji wakiume unayeruhusu kijiwe kupiga stori na washikaji sehemu ya biashara, ondoa vivutio vinavyotengeneza mazingira yakijiwe kama benchi biashara yako haina muundo wa mteja kununua na kukaa kama mgahawa.

Usihodhi pesa ya biashara kama unahitaji kuikuza biashara yako, kumbuka kua upo kweny biashara ya kujumua na kuuza kwa rejareja (Trading business), hivo hakikisha mauzo yanabadilika kua bdhaa, jitahidi kununua bidhaa kila pesa inayoipatikana kulingana na mauzo(back to back reinvesting) na gharama kama vile za vyakula havikwepeki ukitumia kwa sku gharama ya 2000 kwa ajili ya chakula hakikisha hyo hyo sku utaingiza bidhaa yenye faida kubwa kuzidi 2000(+2000) kwa namna hyo utazimudu gharama zako binafsi huku unaikuza biashara yako kumbuka una mtaji mdogo na faida za duka la rejareja ni ndogo hivo ni rahisi mno kujikuta unakula mtaji badala ya faida.

Epuka kuuza hamna, najua mtaji ni mdogo ila yafaa kuhakikisha una vitu vinavyohitajika na soko, ikiwezekana usichukue katika mfumo wa carton chukua katika idadi ndogo kama supplier wako anakubali kufumua carton ili uweze pia kununua na bidhaa zingine usikusanye pesa mpaka ifike yakuhemea mzigo mkubwa hakikisha unanunua na kununua tena, ukomo ni pale duka la jumla limefungwa kwakua maduka ya jumla huwahi kufunga hivyo nunua bdhaa pesa ya mauzo ya kila sku mpaka sekunde ya mwishio kabla supplier hajafunga, usiende kulala na pesa ambayo ungeinunulia bidhaa hujijengi unajiharibu hakikisha unafuatilia mzunguko wako wa pesa kama unazidi kuongezeka(Money going out to buy goods&money comi ng in after selling)

Usikae mbali na biashara kiasi cha mteja kuita "dukaaaaaaaaaani" kumbuka hili ni duka la vitu vidogovidogo kama pipi, jojo, biscuits pia hivo sio rahisi mtu kukuinua ukiwa mbali huku anahitaji kununua jojo za 100 mteja ataona aibu kukusumbua kisa 100 ataenda
Mlango unaofuata muuzaji alipo anapotakiwa kuwa kama muuzaji, tayari mpaka hapo utakua umeshapoteza pato la 100

Epuka kukopesha mali kwa mteja, kumbuka muundo wa biashara yako ni kujumua nakuuza sio kujumua na kukopesha ufanyapo kukopesha ni kama kutengeneza tuta katka mfereji unaotiririsha maji, kumbuka ukopeshapo mteja ajapo kukulipa hakulipi na riba na kama ungezungusha hyo pesa kwenye mzunguko ingezaa hivo jitahidi kutokukopesha.

Kua shapu mikononi, wateja hupenda kuhudumiwa haraka na kuondoka hivo yafaa uwe haraka katika upimaji wa vitu kama sukari, ngano, sembe nakufungashia wateja kwa uharaka iwezekanavyo

Tumia simu kununua bidhaa & delivery (uwasilishwaji wa bidhaa mlangoni pako) kama supplier wako anafanya delivery kwa muda utumapo order yako basi hakuna haja yakuliacha duka au kulifunga kwa muda (temporary close) muda unaoutumia kwenda kununua huku nyuma unapoteza mapato wateja wajapo kama unauwezo wakupata kijana mwaminifu na mchapa kazi mzuri basi hakikisha yeye anakusogezea bdhaa nawe unakuepo dukani mara nyingi biashars ndogo za mitaani zinakosa kitu kiitwacho leverage other peoples resource, other peoples time badala yake hua ni my time, my resource.

Lets engage waweza ongezea point kadhaa mkuu tupate kujifunza sote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kukopesha aisee ndo Mchawi wa Biashara, Mimi mwanzoni nafungua duka .. nilikuwa nikikopesha wanapotea mazima. .... Umenikumbusha kitu hapo huyu dogo anaebakigi dukani ashajenga mazoea na vijana kiasi kwamba unaweza wakuta wamekaa dukani kama kijiwe hivi ..ntajitahidi hili nilisimamie mambo yazidi kusonga ... Asante Sana Mkuu
 
Epuka kufanya kijiwe sehemu ya biashara yako kwa gharama yeyote ile, ushikaji na ushosti haupaswi kufumbiwa macho sehemu ya biashara na ukumbuke hili ukiwa muuzaji ni wa kike na mashosti hujaa kweny biashara yako kupiga stori basi tambua kabisa jinsia yakiume itakupita kama haioni kuna duka kwako nakwenda kununua fremu inayofuata vivyo hivyo kwa muuzaji wakiume unayeruhusu kijiwe kupiga stori na washikaji sehemu ya biashara, ondoa vivutio vinavyotengeneza mazingira yakijiwe kama benchi biashara yako haina muundo wa mteja kununua na kukaa kama mgahawa.
Hii kitu uswahilini ipo sana aisee,na me nikishaona hiyo hali kwenye duka la mtu ni bora nitembee dakika kumi kufuata huduma kwenye duka lingine...
enewei,thanks kwa elimu....
 
Kuna duka nimeacha kwenda saivi napita tu nilikuwa nikienda lazima niite mzee m....dukaniii.kisa kuungisha duka la mtaani siku hizi narudi na pacel
 
Hiyo point ya kugeuza sehemu ya biashara kuwa kijiwe ni ukweli mtupu, kuna wengine wanahitaji kununua kondom au pedi dukani kwako,sasa akishaona kuna watu haji kununua anatafuta sehemu isiyo na watu"privacy "

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nje ya mada kidogo,

Hivi tatizo la kukosea kurudisha chenji kwa wateja hutokana na Nini?

Mwenye kujua tafadhari.

Sent using Jamii Forums mobile app
Watalaam wanasema kuna sehemu kuu 2 katk ufahamu
[emoji828]Conscious mind(Akili kubwa)
Chukulia sku ya kwanza ambapo ulkua unajifunza kuendesha baiskeli/gari akili yote na milango ya fahamu kama macho& masikio vilkua vyote vinashirikiana kufocus katk jambo moja lakujifunza tu hata kama kuna smu imepigwa huipokei.

[emoji828]Subconscious mind(Akili ndogo)
Baada yakujua kuendesha ukawa na uzoefu wa muda mrefu ukajikuta unauwezo wakupokea smu, kupepesa macho huku na kule huku unaendesha

Mara nyingi kukosea kurudisha chenji hutokea ambapo subconscious mind ipo katka control labda mteja alkukuta ukiwa unatumia simu na ulkua na very interesting topic ambayo imeshika akili yote, mteja akikupa 10, 000 ananunua kitu cha 750 ni rahisi kujikuta unarudisha chenji kwa kukosea maana itakuchukua muda kuhama kimawazo kusahau kilichoshika akili na umpe mteja attention yote

Hivo kweny scenario kama hyo sio vibaya kutumia calculator husaidia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watalaam wanasema kuna sehemu kuu 2 katk ufahamu
[emoji828]Conscious mind(Akili kubwa)
Chukulia sku ya kwanza ambapo ulkua unajifunza kuendesha baiskeli/gari akili yote na milango ya fahamu kama macho& masikio vilkua vyote vinashirikiana kufocus katk jambo moja lakujifunza tu hata kama kuna smu imepigwa huipokei.

[emoji828]Subconscious mind(Akili ndogo)
Baada yakujua kuendesha ukawa na uzoefu wa muda mrefu ukajikuta unauwezo wakupokea smu, kupepesa macho huku na kule huku unaendesha

Mara nyingi kukosea kurudisha chenji hutokea ambapo subconscious mind ipo katka control labda mteja alkukuta ukiwa unatumia simu na ulkua na very interesting topic ambayo imeshika akili yote, mteja akikupa 10, 000 ananunua kitu cha 750 ni rahisi kujikuta unarudisha chenji kwa kukosea maana itakuchukua muda kuhama kimawazo kusahau kilichoshika akili na umpe mteja attention yote

Hivo kweny scenario kama hyo sio vibaya kutumia calculator husaidia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ooh nashukuru kwa kunifafanulia hili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom