Una kadi yoyote ya chama cha Siasa? Uliichukua kwa madhumuni gani?

Una kadi yoyote ya chama cha Siasa? Uliichukua kwa madhumuni gani?

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Leo nimeshuhudia watu wakitembea kuwashawishi watu wajiunge na chama chao cha siasa, Watu hao walikuwa wawili walinifuata na mimi wakanambia nijiunge kwenye chama chao ili niwe mwanachama nipate na kadi ya chama chao huku wakinishawishi kuwa siyo gharama kubwa kulipia kadi hiyo kwa mwaka.

Jambo hilo likanipa kuwaza je, kila aliye na kadi ya chama aliichukua kwa kuwa alikipenda chama hicho na ameona kina Sera, mitazamo na malengo ya chama hicho ameyaridhia au aliichukua kwa minajiri gani huenda kuna jambo linafanyika na kadi hizo za vyama siasa tofauti na utambulisho wa kuwa mwanachama wa chama cha siasa.

Hebu nambieni kadi ya chama uliyonayo uliichukua kwa lengo la utambulisho wa uanachama au kuna jambo gani inakusaidia tofauti na hilo?
 
Kadi ya chama DUME Ni muhimu Sanaa
 
Siku hizi ukiomba ajira wana kuuliza unayo kadi ya CCM, kama huna na ajira hupewi.
Toka hapa. Uwongo huu. CCM Kwenyewe unaomba kazi na unapewa. Camera man It's vijana kibao. Na wapo kikazi na si wanasiasa.
 
Back to the topic, mimi ninayo ya CCm wayback, na ilikua kwaajili ya kushiriki chaguzi za viongozi ndani ya CCM. Wenye uadirifu. Ila sijapata nafasi kushiriki chaguzi hata moja.

Sijawahi jua mfumo wa vyama vingine, ila pia kwasbabu sioni malengo yao.
 
Mimi sina kadi ya chama chochote ila nawaza kutafuta kadi ya chama kile kikongwe, sio kwamba nakipenda ila nalazimika maana marafiki zangu hawasumbuliwi kwenye biashara zao kisa wana kadi hiyo hata wao walitafuta kwa ajili ya ulinzi tu wa biashara

Tulikuwa kwenye viti virefu wakanikutanisha na mwenyekiti wa chama kikongwe wa eneo tunalofanyia kazi akanambia ili niwe salama lazima niitafute kadi la sivyo biashara zangu zitakuwa za misukosuko.
 
Jirani yangu nyumba ya tatu kutoka kwangu ni mjumbe wa shina,ilitokea offer ya dawasa kutembelea shina lake kwa ajili ya kuangalia na kuwafikia wahitaji wa maji.

Siku hiyo nipo kazini wife akanipigia akisema mjumbe anauliza wewe chama gani,Inner voice ikaniambia sema CCM kesho yake pick up ya dawasa ikaja kushusha vifaa vya bomba pale home siku tatu mbele maji yakatoka waliojibu tofauti na mimi na wengine tuliostuka wakawa wanakuja kuchota maji kwangu.
 
Toka hapa. Uwongo huu. CCM Kwenyewe unaomba kazi na unapewa. Camera man It's vijana kibao. Na wapo kikazi na si wanasiasa.
Sijaandika hio comment kudanganya au kupata like mkuu nimeandika kwasababu ndio uhalisia. Ninao wana mpaka ikulu wanafanya kazi wakishapasi interview wanaulizwa mlego wao wa siasa na wakisema hawana chama hapo huambiwa kachukuwe kadi ya ccm upate ajira. Juzi kuna mwana kakosa ajira sababu kuna wanawake wametoa rushwa ya ngono ni kazi ya jeshini hawa wote wana kadi za ccm.
 
Jirani yangu nyumba ya tatu kutoka kwangu ni mjumbe wa shina,ilitokea offer ya dawasa kutembelea shina lake kwa ajili ya kuangalia na kuwafikia wahitaji wa maji.

Siku hiyo nipo kazini wife akanipigia akisema mjumbe anauliza wewe chama gani,Inner voice ikaniambia sema CCM kesho yake pick up ya dawasa ikaja kushusha vifaa vya bomba pale home siku tatu mbele maji yakatoka waliojibu tofauti na mimi wakawa wanakuja kuchota maji kwangu.
Kwa hiyo ili kupata huduma za kijamii kwa urahisi inabidi uwe mwanachama wa CCM la sivyo inakula kwako!
 
Back
Top Bottom