Una mipango gani kwa miaka 10-20 ijayo?

You can't choose your fate... Okay??
Hapa sasa ni mtazamo mwingine kabisa kwenye maisha. Mimi siamini kwenye vitu 3: miujiza, bahati na hatma.

Kila maamuzi ninayofanya yana-reflect maisha ninayoishi sasa. So, your point isn't valid in my opinion.
 
Ufanye nini? Zaidi ya kula na kulala sioni cha ajabu
 
Siri Huwa haiwekwi wazi plus mipango wewe subiria matokeo
 
Hongera mkuu,
Hata sisi tulikuwa na mipango na kuiandika sana kwenye MS Word, leo tunaishi tu liende 🀣
 
Hongera mkuu,
Hata sisi tulikuwa na mipango na kuiandika sana kwenye MS Word, leo tunaishi tu liende 🀣
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Si wamasemaga "maisha hayana formula". Kila kitu ni kujaribu, uzuri maisha yanakupa fursa kulingana na uwezo wako. Majani ya juu yakikushinda, kuliko kujifanya Twiga unarudi kula chini tu "kila Mbuzi atakula kwa urefu wa kamba yake".

Ila mpaka una-survive sasa hivi maana yake kuna mpango mwingine umetiki. Muhimu ni kukimbizana na fursa tu "kama kinyonga" unabadilika rangi kuendana na mazingira.
 
OMBA MUNGU USIFE UJIONEE MWENYEWE SCRIPT YAKO πŸ˜€
 
Kumiliki kampuni ya plumbing iwe kubwa kwa sababu ndio kitu ninacho kipenda sana
 
OMBA MUNGU USIFE UJIONEE MWENYEWE SCRIPT YAKO πŸ˜€
Hahah! Kama nilivyosema ni afya na kifo tu ndiyo vinaweza kukwamisha mpango kutimia. Hivyo ndiyo vitu ambavyo siyo guaranteed na sina uwezo wa kuamua viendaje kwenye maisha yangu.

Hapo juu kuna mdau nilimjibu mimi siamini kwenye vitu 3: miujiza, bahati na hatma. "Script" maana yake ni hatma nikiishi kutimiza yale niliyopangiwa. Mimi siamini hicho, ikitokea nimefeli itakuwa ni kwasababu yangu mwenyewe: labda sikujipanga vizuri au mpango kazi sikuufanyia kazi ipasavyo.

Maisha yangu yapo kwenye mikono yangu mwenyewe, mpaka nilipofika kuna vitu nimefeli kutokana na maamuzi niliyofanya miaka iliyopita.
 
Kwa mipango yako hii ulio ipanga,Hatua ya kwanza ni uondoke Tanzania.

Tanzania ni sehemu ngumu sana kufanikisha hayo uliyo yasema.
 
hongera kwa KUadmit hili,, ilikuaje ukasoma diploma baada ya degree?
umenikumbusha nilivyoacha kozi ya degree kwenda kusoma kozi ya mambo ya madini diploma kipindi hicho inaanzishwa chini ya MH MUHONGO SOSPETER.Yaani sijutii maamuzi yale baada ya kumaliza degree yangu ila ile kozi ningesota ila MUNGU MWEMA NA MIPANGO YAKE.
 
Miaka 10 au 20 ijayo Sina uhakika km ntakua bado naishi kwenye hii Duniani nadhani ntakua kwenye sayari nyingine huko naendelea na Maisha mengine, MUNGU akipanga na wewe unapanga unaweza hata kesho usifike hii ndio ikawa comment yako ya mwisho
 
Kwa mipango yako hii ulio ipanga,Hatua ya kwanza ni uondoke Tanzania.

Tanzania ni sehemu ngumu sana kufanikisha hayo uliyo yasema.
Kulingana na kazi zangu za freelance upo mpango kazi mwingine wa kuondoka Tanzania ila unahitaji pesa kuukamilisha.

Kwa sasa kuna nchi nyingi zinatoa Digital Nomad Visa ila kuna minimum requirements bado sijakidhi vigezo: kwenye kiasi cha pesa ninachopata kwa mwezi ndiyo tatizo.

Nahitaji kufikia €750 - €2,500 kwa mwezi kuwaza kuondoka Tanzania.

Tayari kuna nchi ndani ya Europe ipo kwenye mipango ila bado siuoni kama ni mpango halisia kwa sehemu niliyopo kwasasa katika maisha.
 
Kila lakheli mkuu....

1. Career Building. Hapa nataka kujenga career yangu kwenye Web Development & Graphic Design (Freelancer) ndiyo kitu ninachifanya kwa sasa ila ninapotaka kufika ni safari ndefu ambayo siwezi kufika kwa usiku mmoja ndiyo maana ujenzi wa career yangu upo kwenye first phase. Malengo ni kuwa bora kwenye hizo field: bora kweli.


Mdogo angu Dunia imebadilica sana nakupa huu ushuuda wa mdogo wetu cousin last born...

Mwaka 2021 alimaliza bachelor degree upande wa computer science na jua computer science ni wide sanaaaa...

Dogo akahudhuria Kila interview kuanzia Takukuru, utumishi, Tra hakupata akajiunga na bro angu ana kampuni ya mambo ya finance na accounting software......

Bro alikua anampa kazi za coding sanaaa mda mwingi yupo pekeake jifungia sana ndani mpaka nikagundua izo kazi za software developer Zina damage Brain 🧠🧠 πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

All in all naona kama umechagua njia yako hongera timiza hitaji la moyo wako stay safe and blessed
 
Hongera sana mdogo wangu kwa good plan hii plan yako watanzania wengi wakishastaafu ndo wanataka kuwa na financial freedom wakati umri ushaenda.

Mie pia mipango yangu inafanana na yako kasoro we are in diffent professional my main target to retire young but rich then to travel the world.

Hamna kinachoshindika kama Mwenyezi Mungu atakupatia uhai mrefu na Afya nzuri, watanzania wengi huwa wanaamini baada ya kuona matokeo hivyo usikatishwe tamaa na maneno yao...
 
Baada ya kumaliza Secondary Education sikuendelea na Advance kwasababu sikupata ufaulu mzuri kwenye masomo ya Sayansi na option iliyobaki ilikuwa kwenda kusoma Arts. Huko sikuwa na passion na kitu chochote.

Nikafanya uamuzi wa kujiunga na chuo kusoma kile ninachofanya sasa kwa furaha zaidi. Ni uamuzi bora niliofanya kwenye maisha yangu.
 
Miaka 10 au 20 ijayo Sina uhakika km ntakua bado naishi kwenye hii Duniani nadhani ntakua kwenye sayari nyingine huko naendelea na Maisha mengine, MUNGU akipanga na wewe unapanga unaweza hata kesho usifike hii ndio ikawa comment yako ya mwisho
Ni kweli kabisa wote tunaishi kwa matumaini kuwa sekunde 1 ijayo tutakuwa hai na wapo wengi tunavyoandika hapa hawatafika sekunde 1 ijayo.

Kifo ni sehemu ya maisha, haimaanishi tusiwe na mipango kwasababu miaka kadhaa mbele hatutakuwepo.
 
Una plan nzuri, una malengo ya mbali ila kikubwa maisha yana namna yake sio pdf

Nikiwaa na 23 tayar nlikuwa na hyo degree ya IT, graphics nlifanya sana, web nlitengeneza na nlifanyia watu project zile za final year ila maslahi yake ni madogo kikubwa nachoweza kukushauri jaribu kufocus na mtaaa unahitaji nn switch malengo yako vzr lkn jitahidi uwe na multiple streams of income
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…