Una mipango gani kwa miaka 10-20 ijayo?

Mkuu pambania kombe hapa hapa nyumbani bongo Tanzania....

Bongo Kuna fursa nyingi sana Kwa Sasa tafuta giant kwenye field yako au field yeyote jifanye royal Kwa miaka mi nne wewe fanya business intelligence then anzisha chako hope utafanikiwa.....

Cc. Mshana Jr
 
Asante sana kwa maoni yako. Unajua kilichofanya nikimbie Software Development / Programming ni kwasababu haina uhusiano mzuri na mazingira niliyopo.

Mimi kujifunza Programming kwa umri huu nilijua kabisa nitapoteza vitu vingi vya msingi. Ndiyo maana nikachagua career kwenye Web Development na hapo bado nikapunguza mzigo mimi nafanya Front-end Development tu, maybe huko baadaye nitakuwa Full stack Developer. πŸ˜‚πŸ€
 
Asante sana kwa ku-share hii. Nimechukua points. Ni kweli career ya IT kwa hapa nyumbani hailipi sana ndiyo maana mimi nime-base zaidi kwenye International clients. Graphic Design naweza kusema ndiyo kitu nilikipenda kabla hata sijaingia darasa lolote la masomo ya IT. Ilitokea tu napenda sana Sanaa na baadaye nilikuja kujua ni career kabisa watu wanaishi kupitia hiyo.

Ni kweli naangalia pia fursa zilizopo mtaani, back-up plan ipo.
 
Uwe blessed sana mdogo wangu
 
Kweli mkuu. Nyumbani ndiyo kila kitu. Hapa ndiyo kuna watu tutakaoelewana ndiyo maana naangalia fursa na njia za kujijenga hapahapa Bongo.
 
πŸ€“
 
Miaka 10 mpaka mwisho wa 2023
FAMILIA
1. Watoto
kuwekeza kwa wanangu kielimu (darasani kidunia na ujuzi), kiuchumi (investments) Kuwepo pale kwaajili yao na kuwaongoza katika kila hatua (kiuchumi, kiakili kiafya....etc)mpaka watakapofika umri wa chuo au kujitegemea (boarding school haipo kwa plan) and creating beautiful and lasting memories
2. Baba watoto
Kujibamba tu na kuhakikisha tuna furaha, watoto wametukuta na wataondoka watatuacha so maisha lazima yawe bomba nyakati zote
UCHUMI
passive income ya $1M kwa mwaka (real estate, stocks,bonds na mengineyo kadi nnavyojifunza
AFYA
Kula vizuri, mazoezi na kujiweka kukabiliana na changamoto za umri zisizozuilika
Kuendelea kufeed ubongo wangu non toxic contents as much as possible maana dunia imekua na too much negativity
SPIRITUAL
kuwa mtu wa kujitoa sana kwa wahitaji

20 yrs... ya miaka 10 yakitimia ntakua naenjoy tu na baba chanja maana watoto wote watakua watu wazima
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…