Una mtaji ila hauna pesa ya kodi ya fremu? Zijue biashara zisizohitaji fremu

Una mtaji ila hauna pesa ya kodi ya fremu? Zijue biashara zisizohitaji fremu

Wewe hatari ya kuweka mitungu ndani yako huijui ila unajua pesa tu.
in Business we are dealing with risks

unapofanya biashara yoyote hayo mambo uliyoyasema ni ya muhimu kuyajua na kuyafikiria ila siku zote nawambiaga watu

usiyape nafasi hayo mawazo yanapokuja kikubwa jitahidi ufanye kazi kwa bidii na ujue kuweka akiba cause any time kinanuka

mimi kuna sehemu natumaga vijana wangu wakafanye biashara kabisa na ni sehemu HAZIRUHUSIWI (sehemu hatari) ila nawambia nyie nendeni wakikukamateni nipigieni simu (wanaenda) wanapiga pesa hata 50,000 chap chap then unaskia kadakwa...

unamuuliza umeingiza sh ngap? anakwambia hapa tayari nina 50,000 unamwambia "tulia" mpe simu huyo aliyekushika,unaongea nae unampooza kwa 10,000 anamwachia (dogo anasepa) faida mfukoni 40,000..Can you see that?

How if ningeogopa nikidakwa itakua noma halafu nisiende fanya biashara eneo hilo,hiyo 40,000 ningeitoa wapi?? ndio yale yale tunaambiwa "uoga wako ndio umaskini wako"

Unajua kwanini wafanya biashara wa madawa ya kulevya wanadunda uraiani na wanajulikana?? Wakikwambia bajeti wanayoitenga kwa ajili tu ya kuhonga mapolisi unaweza ukashangaaa, why wanahonga?? They know wanachofanya si sahihi but ndipo pesa ilipo so watafanyaje sasa and they need money???

ndipo wanaamua hapo Anaanza kuhongwa kuanzia IGP mpk mwenye V moja mzigo wao unaingia biashara wanafanya kiulainiiiii...sasa wewe jichanganye WAIGE uone kitakacho kukuta.

kwa ufupi ndugu yangu unapoamua kuingia kwenye biashara elewa umeingia VITANI,huku sio kwenye ajira,vitani unaweza kuwa na silaha zote ila na bado ukaenda ukarudi huna mguu,ndio mana wanajeshi siku hizi hawana ujinga wa kufa kufa,wanaenda vitani na wanarudi woteee (usitake kujua kinachofanyika huko vitani,acha kabisa)

Hii nchi ina wenyewe ndugu yangu,haya mabiashara tunayafanya tu ila usijiamini sanaaaaaaa hata kama una maleseni umejaza ukuta mzima,vibali vyoteeeee atakuja mtu mmoja tu atakutafutia sababu na hela itakutoka.

SO jiamini na elewa uko vitani na usiogope mtu pambana ya hela yote,MJINI inaongea PESA tu midomo siku hizi mapambo muraaaaa. King999
 
nafaka Pesa nnje nnje ila ndio Mtaji (kodi ya frem)

ila kama utaweza jikakamua ukachukua kontena lako la 1.5M

ukaligeuza frem sio siri lazima uwe mcharo.

Hii mimi ndio naifikiria niifanye [emoji125]‍♀️[emoji125]‍♀️
 
Ww unajua biashara! Its all about taking risk
 
nafaka Pesa nnje nnje ila ndio Mtaji (kodi ya frem)

ila kama utaweza jikakamua ukachukua kontena lako la 1.5M

ukaligeuza frem sio siri lazima uwe mcharo.
Wapi wanauza contena kwa bei hii mkuu.
Maana naonaga sehem nyingi bei mkasi
 
Wapi wanauza contena kwa bei hii mkuu.
Maana naonaga sehem nyingi bei mkasi
kontena za 1.5M ni used mkuu zile fupi fupi

zipo nyingi sana,kuna mahali nimeliona moja limetelekezwa barabarani

limechorwa linauzwa Nikachukua namba za muhusika kupiga akaniambia bei ni 1.8M ila mwsho 1.5M

Lile kontena nilimtonya mdau mmoja akalifata...

Ya bei hiyo mengi sana mkuu,tena Mengi ukihitaji usiende yafata Mapya hutoyaweza BEI.
 
Siku hizi watu wengi sana kinachowakwamisha sio kwamba hawana mitaji,wengi mitaji wanayo ila shida ni 1 tu inakuja kwenye suala la fremu wapi atapata pesa ya pango la chumba cha yeye kufanya biashara yake.

Fremu tunajua kila mtu bei zake zilivyo na kadri frem inavyokua sehemu yenye wateja ndio na Bei (kodi) inazidi kuwa kubwa, kwa waishio mijini wanaelewa kodi za fremu zilivyo za moto ambapo bei ya chini kabisa ni laki kwa mwezi.

Ubaya zaidi ni pale mwenye nyumba anapokwambia nyumba yake anapokea kodi kuanzia mwaka, wengine kodi miaka miwili, na kuendelea kutegemea na fremu ipo wapi na watu wanafika dau kiasi gani na ndio mwenye nyumba anavyokutandika za uso.

Turudi kwenye Mada leo nataka washirikisha biashara 7 ambazo hazihitaji fremu ila zinakuhitaji wewe tu na mtaji wako na kikubwa kingine inakuhitaji UTAYARI na MAAMUZI sio uwe tu na mtaji halafu uanze kusema "watanionaje, watanichukuliaje, si ntakuwa waajabu nk nk"

1. MITUNGI YA GESI

Hii biashara haitaki uwe na frem kule bara barani kwa sababu wateja wa hii bidhaaa karibia 90% hawapatikani huko ila wapo huku huku majumbani tulipo,watu wanaoweka biashara hii kule bara barani ni kwa sababu tu unakuta ana biashara zingine ambazo zinahitaji wapita njia,ila kama wewe una mtaji na unafikiria biashara hii ni chaguo lako

Kwa sababu utakaponunua mitungi yako lets say mitungi midogo ya kg 15 (minne) mikubwa size ya kati kg 38 (minne) then kwa siku ukabadilishia wateja gesi wateja wa nne yani mitungi midogo wawili mikubwa wawili.

Faida ya hii mitungi kwa mdogo ni 2000 mpk 3000 itategemea na wewe unauzaje (tufanye ni 2000) then mikubwa faida yake ni 6000 to 5000 itategemea na wewe vile vile unauzaje (tufanye ni 5000) so ukijumlisha wateja wako wa nne utapata 2000*2 + 5000*2 = 14,000 then chukua hiyo 14,000*30 = 420,000 hii itakua pesa yako isiyo na makato ya kodi wala nini yani unaikamata nzima nzima.

(Mtaji inategemea na unataka kuanza na mitungi mingapi)

2. MKAA

Hii biashara nayo haina mbwembwe ni suala la wewe kuangusha gunia mbele ya nyumba unayoishi then kupanga mkaa wako ndani ya mifuko na kishaa unarudi zako ndani kutulia ataetaka mkaa ataita "mkaaaaaaaa" ukiskia utatoka utaenda mpimia au mpatia mkaa wake kisha utarudi zako ndani.

Faida ya hii biashara siijui japo najua ina faida sana kwasababu nina jiko langu nilikuwa natuma wafanyakazi mkaa wa kupima nikawa sioni faida, ila tangu niwe nanunua mkaa kwa magunia faida naiona.

Hiyo maana yake ni kwamba mkaa una faida maana mkaa unauzwa wenyewe, chenga zinauzwa zenyewe, vumbi la mkaa linauzwa lenyewe.

Yaani hapo gunia utakalochukua sasa hivi lets say gunia la laki uhakika wa kukurudishia laki upo so itategemea na wewe unauza mkaa wako kwa speed kiasi gani.

(Mtaji wake itategemea na magunia mangapi unataka kuanza nayo)

3. MAJI

Unajua si kila sehemu kuna maji,na hata sehemu zenye maji si kila mtu ana vyombo vya ndani vya kujaza maji kama mandoo na majaba especialy mtu kama mimi nina allergy na mandoo mandoo sipendi kuona mandooo kwangu kabisa so kama unaishi sehemu maji yapo au hamna (japo hii nzuri kwa sehemu zenye shda ya maji au maji kukatika katika) na una ka hela kako kama ka laki 5 kamekaa tu,

Nenda kanunue tank lako la litre 2000 linauza kama 250,000 tu then lijengee hapo nnje kwenu kisha andika tank lako (maji yapo ndoo sh 200) then rudi zako ndani uchune, utasikia tu raia wataokuwa wanakuja, amini usiamini yale maji utauza tu (wala usiogope).

4. LUKU/GENERETA

Unapokuwa unaona watu wanalima wewe kama huwezi kulima, nenda kawauzie majembe walime then rudi zako tulia. Umeme ni changamoto sana hasa maeneo yenye masoko na wafanyabiashara wadogo wadogo wengi unakuta wengine wana utaratibu umeme wanawashiwa saa 12 jioni hadi 7 usiku.

Sehemu zingine ni majenereta nadhani hata wewe ni shahidi unaonaga majenereta huko usiku kwa wafanyabiashara.

Unaposikia jenereta ujue ni biashara ya mtu ile, anawawashia jenereta then anapitia 1000 kwa kila kichwa (hawa ni watumiaji taa tu) ila ana jenereta lingine kubwa kwa wenye mafriji na maduka kila kichwa kwa hawa watu anakula 5000, kwa hiyo unaweza ukaona jinsi hela watu wanaingiza.

Una hela yako ya jenereta kubwa nenda sehemu zenye biashara then waulize umeme wanatoa wapi kisha utawasikia jibu lao, wakikwambia ni shida wapelekee jenereta then kula pesa kwa kila mtu (mafuta weka mwenyewe)

Au unaweza ukaamua wavutia umeme LUKU mpya tanesco ni 321,000 unaweza kwenda kufanya mchakato wa umeme then ukawasambazia raia ukawa unakula pesa kila siku kwa kila ataetumia umeme wako.

5. M-PESA/TIGO PESA

Hii nayo inakuhitaji wewe na laini zako na pesa yako, unatafuta bango tu unalichora kisha unalieka hapo nje ya nyumba yenu unatafuta mwamvuli, kiti unaweka hapo kama vile unakaa kisha unaandika namba zako za simu in case mteja akija akupgie au akutext kisha unarudi zako ndani.

Mteja akija kwakuwa ni mtaani lazima akutext au akuite, utapiga hela si kidogo, ukishazoeleka utashangaa hela utazokuwa unaingiza (si kubwa sana ila si haba)

6. VIFAA VYA USAFI MAJUMBANI

Unachotakiwa kufanya hapa ni kutengeneza kamba kama ile ya kuanika nguo nyumbani kisha unaipgilia hapo nnje kwenu then huo mtaji ulionao hata kama ni laki mbili nenda town nunua mafagio, mopa, yale yakutolea bui bui, vidude vya chooni, vizolea taka,nk kisha tundika kwenye hiyo kamba yako kisha we nenda zako ndani tulia.

Wateja watakuja na kwakuwa unauza vitu vya matumizi ya kila siku amini usiamini utakua unafanya biashara ndani ya mwezi hela yako itakua imerudi then ukiangalia mzigo bado upo wa kutosha(ile ndio faida yako) unaweza ukauza ukatumia hela au ukfanya upendavyo.

Ila ni biashara inayolipa sana maana mfagio mmoja unauzwa 1000, ukiuza mfagio 3000 ina maana kwa kila mfagio faida yako 2000, haya Mungu saidia ukauza mifagio mitano utakuwa na 10,000 japo siku hazilingani unaweza usiuze hata hiyo mitano ukauza mmoja faida 2000 kwa mwezi ni 60,000

(ungeipata wapi hiyo 60 au angekupa nani bure?)

7. UDALALI

Hapa bwana mtaji ni simu yako au computer, zijue sites zote wanazouza vitu mbali mbali, iwe magari, simu nk. yaani ili mradi tu ni wauzaji wa hapa hapa Tanzania ingia hata huko Kupatana tafuta wauza vitu then wewe kazi yako ni kuzurula mitandaoni kutafuta wateja.

Ukiona mtu anatafuta "jamani mwenye simu ya iPhone 6 bajeti yangu
70,000" then wewe anza kutafuta hiyo iphone kwa mwenye nayo. Akipatikana mwambie una 50,000 then komaa nae akikubali rudi kwa mteja aliepost anatafuta iphone kwa 70,000 mwambie "unayo" kisha akikuomba picha na wewe unamuomba huyu huku unamtumia, akiridhika, akikwambia mpelekee, unatoka hapo unamfata yule jamaa uliemwambia una 50k unaenda unaikagua simu ukiona nzima unamwambia jamaa ukweli "bwana nina mteja wangu kaipenda simu yako nataka twende mimi nitakulipia nauli kwenda na kurudi (lazima akubali).

Mkienda kule wewe ndio unakuwa mwenye simu then mwenye simu anageuka rafiki yako au ndugu kakusindikiza, unafanya biashara.

Unachukua 70,000 yako then unampa jamaaa 50,000 yake nauli haizdi 3000 unampa DEAL DONE.

Kwa siku uza product 1 tu, kama ndio wengine wauza magari atahakikisha kwa mwezi kauza gari 1 tu maana gari 1 faida sio chini ya milioni au above laki 5.

Chukua inayokufaa. Usidharau maana wengine ndio wanaingiza hivyo pesa.

Ukiona chai au haiwezekani twenzetuni MMU.
Nikiri wazi, nimekuwa muumini wa hizi nondo zako kuhusu biashara. Hakika ni za msaada mkubwa sana hasa kwa mtu anayeilewa hii lugha unayoitumia. Maana japo unaandika kwa kiswahili, ila si kila mtu anakuelewa. Zidi kutulisha hiki chakula adimu kwa mafanikio yetu ya baadae.
 
🙏🙏🙏

Utakula sana mkuu
 
Ipo siku utakuja kupokea ushuda. Nazidi kuyakumbuka maneno yako ya kuwa huwa hauoni tatizo kumshirikisha fursa mtanzania sababu unajua ni mvivu wa kuzifanyia kazi.
hakika unanifatilia

ni kweli ulichosema

watanzania usiogope wapa taarifa maana wengi huzipokea kama story/umbea/ubuyu

watakao fanyia kazi idea/mawazo utayompa au mwambia katika 100 utampata mmoja

wengine wote akifikiria kuanza tu (kashasahau ulimwambia nini) Anasema ntaanza next time

sisi tutimize wajibu wetu

tuelimishane/tuburudishane/Tuonyane nk

Kuhusu kuingia ktk utendaji we waachie wenyewe

Acha tuendeleee.....
 
Back
Top Bottom