Mbishi 4 real
JF-Expert Member
- Jan 16, 2014
- 640
- 651
Kumekua na wimbi kubwa la watu wanaojiita manabii likiongezeka kila kukicha na manabii wote hao wameanzisha makanisa yao.
Manabii hawa wamekua ni wengi kuliko hata wale ambao wametajwa kwenye biblia takatifu.
Kwa ulewa wangu mdogo ni kwamba wale manabii wa kale ambao walitajwa kwenye biblia takatifu unabii hawakujipa wenyewe bali walipewa kutokana na matendo yao mazuri kwa mwenyezi Mungu na kwa jamii iliyowazunguka.
Siku hizi kumezuka idadi kubwa ya watu wanaojiita manabii na hatujui hiko cheo cha unabii wamepewa na nani na wengi wao wameweka viingilio kwa wale watu wanaotaka kuwaona na viingilio vyao kiukweli vimechangamka.
Hawa manabii wa kuzuka most of them dance according to the sound of the music na wengi wao sio wakweli bali wanawaongezea tu umaskini wananchi, wameshajua asilimia kubwa ya wananchi wanasumbuliwa na nini au wanahitaji nini kwenye maisha yao na wao wanapita mulemule ili waweze kuaminika.
Yesu alipokuja duniani alisaidia kila mwenye shida pasipo kujari hali zao za kiuchumi lakini hawa manabii wetu wa kisasa ili kuwaona inabidi ujipange kwelikweli na unaweza pigwa pesa bila hata kupata kile ambacho ulikitarajia.
Wewe mdau wa JF nini mtazamo wako juu ya hili?