Una mtazamo gani juu ya ongezeko la manabii hapa nchini?

Mbishi 4 real

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2014
Posts
640
Reaction score
651
Kumekua na wimbi kubwa la watu wanaojiita manabii likiongezeka kila kukicha na manabii wote hao wameanzisha makanisa yao.

Manabii hawa wamekua ni wengi kuliko hata wale ambao wametajwa kwenye biblia takatifu.

Kwa ulewa wangu mdogo ni kwamba wale manabii wa kale ambao walitajwa kwenye biblia takatifu unabii hawakujipa wenyewe bali walipewa kutokana na matendo yao mazuri kwa mwenyezi Mungu na kwa jamii iliyowazunguka.

Siku hizi kumezuka idadi kubwa ya watu wanaojiita manabii na hatujui hiko cheo cha unabii wamepewa na nani na wengi wao wameweka viingilio kwa wale watu wanaotaka kuwaona na viingilio vyao kiukweli vimechangamka.

Hawa manabii wa kuzuka most of them dance according to the sound of the music na wengi wao sio wakweli bali wanawaongezea tu umaskini wananchi, wameshajua asilimia kubwa ya wananchi wanasumbuliwa na nini au wanahitaji nini kwenye maisha yao na wao wanapita mulemule ili waweze kuaminika.

Yesu alipokuja duniani alisaidia kila mwenye shida pasipo kujari hali zao za kiuchumi lakini hawa manabii wetu wa kisasa ili kuwaona inabidi ujipange kwelikweli na unaweza pigwa pesa bila hata kupata kile ambacho ulikitarajia.

Wewe mdau wa JF nini mtazamo wako juu ya hili?
 
Yupo nabii kiboko ya wachawi, yaani kila siku anafufua wafu kwenye radio. Cha kufanya ndugu yako akiaga dunia wewe mpigie simu laivu redioni atakuambia ndugu yako hajafa yuko nyuma ya mlango, na fasta anamfufua. Inafurahisha sana na watu wanamuani.
 
Wajinga ndio waliwao,
Mungu anampa kila mtu kwa wakati wake.

Mwaka 2017 nilienda kanisa lipo kigogo kwa Nabii ametoka Nigeria sitomtaja jina
Nilienda ili niweze kupata ujauzito nizae baada ya kukaa kwenye ndoa miaka mingi bila mtoto.

Nabii akaniambia nipeleke laki 4 ili aniombee, nilivyotoka pale sikurudi
Imepita miaka 8, sasa hivi nina mimba
Ningepeleka hiyo laki 4 ningepigwa kiboya.
 

PAKA aliwaondoa manabii feki kibao Rwanda ,na huku inabidi Serikali ifanye hivyo ,wengi ni MATAPELI.
 
Kumbe una mimba Aisee.
 
Dini ni fursa kama fursa nyingine tu don't take it seriously..!
 
heri ungekuja kwangu ningekupa dawa haizidi hata elfu tano....🤣🤣🤣
 
Ungepigwa au ungezaa mashetani yake
 
Mungu akujalie ujifungue salama mumy,,,kwahiyo ushaanza kula udongo 🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…