Una mtazamo gani juu ya ongezeko la manabii hapa nchini?


Kuna "nabii" mmoja baada ya utafiti wake, kaja na kitu kimoja kinaitwa "dhambi mpya". Nami baada ya kutafiti nimegundua kuwa kuna "ajira mpya" inayoitwa "nabiii". Nafasi hii ya ajira ina wahitimu wengi sana. Hauna majukumu ya kazi (job description). Kila mtu anajiongeza kadiri alivyoongozwa na roho isiyojulikana. Kwa hiyo, mjitahidi kuwa macho kwa kuwa wengi wanavutwa kwao kwa kuwa wana majibu mepesi kuhusu mambo mazito na ya msingi kuhusu maisha.
 
kimsingi katika nyakati hizi hakuna cha nabii wala nini wooote wajasiriadini tu maamae zao na hivi wanatumia ndumba yaani mtakamuliwa mpaka mshangae , mpaka watu waje kushtuka too late.
 
U
nabii ni kitu kizuri. Tatizo ni pale wanapo danganya kuwa wanakipaji cha uponyaji uponyaji ni kipaji tofauti sana na unabii. Unaweza ukawa na uwezo wa kuombea mtu akapona na usiwe nabii. Hapo ndiyo wanakosea
 
1.wajinga ni wengi
2.shida ni nyingi za kiimani
3.kuamini kila kitu/tatizo ni la kiimani
4.watu hawatoi kipaumbele ujifunzaji wa biblia
5.wakristo wengi hawajui hata mstari mmoja wa biblia
6.Wajanja wanaona fursa za kupiga hela
 
Jamii ambayo haijaelimika inategemea miujiza
 
Kumbe ushajazwa mkuu...
 
Acha wajinga wapigwe....
 
Tazama makala ya Al Jazeera inaitwa Gold mafia YouTube.

Ni mfumo rahisi wa utakatishaji pesa kupitia haya makanisa. Sadaka ni kitu kidogo sana kwenye utajiri wa hawa manabii.
 
Mimba ipi? Unalilia mimba? Utaipata tu
 
Jana nimesikia kuna Profesa wa manabii. Mmoja wa waumini wake katika ushuhuda alisema "Nimetoka nyumbani kwa mguu nikiwa sina nauli, lakini baada ya kufika hapa nimekuta mfukoni kwangu nina Tshs 10,000"

πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†
 
Angechukua hiyo laki 4, angekupa dawa kupitia dushe lake angekukula.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…