Una mtazamo gani juu ya ongezeko la manabii hapa nchini?

Yule wa kujiita nabii kiboko ya wachawi ni balaa kwanza nabii kajichubua hadi roho alafu pembeni kuna mwarabu fighter aliyekua baunsa wa diamond katunisha kifua kanisani kama dume la njiwa pori ,
Ila yule jamaa aangaliwa kwa jicho la tatu ipo siku atasababisha majanga
 
Kila kitu kinawezekana
Kwa sababu ya imani dhaifu za watu basi kila mmoja wanamuona ni mkweli

Angalieni Kagame alivyokomesha hii tabia
Ukiwa Raisi lazima uwe na maamuzi magumu
Yaani mtu anaingia kanisani miaka 3 anajifunza nae kufoka foka anafungua kanisa
 
Kuna shehe mmoja alisema kama una matatizo ya kiroho,tafuta kiongozi wa kiroho ambaye kasimama kwenye imani kweli,wengine ni wapigaji. Dini zimeingiliwa kuna watu wamegeuza biashara. Wale jamaa wa makobazi nao siku hizi wapo waliogeuka wapigaji,kuna mzee mmoja aliomba wakasome hitma nyumbani kwake wakamwambia toa sh.elfu 40 kwanza ndio tutakuja,akaamua kuondoka huku anasikitika.. Kwa mimi niliyezaliwa mkoa wa makanisa mengi huwa sishangai utitiri wa makanisa
 
Ongezeko linatokana na kuwapo kwa soko kubwa la wapumbavu wa imani.
Na kwa Sasa wateja wakubwa wa Hawa manabii ni waislamu. Ukweli ulio mchungu.
 
kila mmoja atakula kwa urefu wa kamba yake, maitaji ya manabii yameongezeka wananchi wanataka utajiri bila kufanya kaz
 
Duh, kumbe una mimba mkuu
 
Nabii ana kazi kuu tatu:

1. kutabiri mambo yajayo, yawe mema au mabaya sawa sawa na neno la Mungu

2. Kuonya na kemea maovu, na kuwataka watu wamrudie Mungu

3. Kwa kutumia uwezo wa Mungu ndani yao, wataponya wagonjwa, watatenda yale yote Mungu atakayowaamuru.

Lakini katika agano jipya kazi za manabii zimepungua kwa sababu ya uwepo wa roho mtakatifu kwa waamini wote, hivyo yale uliyotakiwa kuambiwa na nabii utaambiwa na roho mtakatifu moja kwa moja.

Manabii wengi wa sasa hata bila kutumia ufahamu wa maandiko utaona tu ni waongo sana, wanatumia media kujibrand, kujitengenezea umaarufu, wanafanya maigizo mengi ili kuwarubuni watu wenye imani ndogo, ni juu yako kuwatambua na kuwaepuka
 
Mi namkubali Nabii Mswahili. Jamaa anatisha sana
 
Hawa inabidi washughulikiwe kama wanavyoshughulikiwa mafisad
Wanajilimbikizia pesa kwa utapeli bila kulipa hata kodi (wanakula pesa nzima nzima)
Wanawafanya watu wawe maskini,
Wanadanganya watu kuamini kwamba umaskini wao dawa yake maombi mwisho wa siku hali ya kufanya kazi kwa bidii inapungua coz mtu anaamini amelogwa
Watu hawafanyi maendeleo pesa inaishia kwa nabii na kushinda kanisani
Hawa ni wahujumu uchumi kama wahujumu uchumi wengine
 
Kila mmoja anatafuta shekeli.

Siyo ile miaka ya wamisionari kutembea kwa miguu kueneza injili, hao sasa ndiyo walikuwa manabii.
Walikuja kujaza watu ujinga, wamewawachia biblia wakachota almasi na dhahabu.
 
Me niseme tu ni Wanaume wa shoka wanaojua kukamata fulsa na kutengeneza vibunda nataman kua kama wao ni wivu tu unanifanya niseme ni matapeli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…