Una mtoto wa nje? Wahi hapa!

Una mtoto wa nje? Wahi hapa!

Hovering

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2018
Posts
275
Reaction score
912
Habari wana JF, tumaini langu mnaendelea vyema. Chapu tushuke kwenye mada.

Ni jambo la furaha kuanzisha mahusiano ya kimapenzi na mtu ulievutiwa nae katika mazingira yoyote na kwa lengo lolote liwe la ndoa au lah! danga and run /eat and run)).

Ni jambo la huzuni sana pale kwa pamoja mnaposhindwa kukubaliana na matokeo (impacts) za mahusiano yenu ikiwemo Mimba, magonjwa ya zinaa au Fumanizi kwa wale wadau wapenda wake za watu.

Katika mahusiano mimba inaweza kutarajiwa au kustusha wahusika. Siku zote ni baraka kwa wale waliojiandaa na kukusudia kupata mtoto katika maisha yao. Isivyo kawaida kwa upande wapili huku mimba hupokelewa kama mhamiaji haramu aliyeingia nchi ya ugeni bila hati ya kusafiria. Hukumu yake huwa nikurudishwa alipotoka(abortion ) jambo ambalo ni kinyume na sheria na si uungwana kabisa.

Sasa tuje kwa sisi wenye watoto tayari, imekuwa desturi kwa watalaka au watu waliochana baada ya kupata mtoto au watoto kukomoana kupitia mtoto bila ya kujali hisia za mtoto. Kukosa fursa ya kumuona mtoto mara wa mara ni moja ya adhabu kwa wanaume kadharika kwa wanawake kutelekezewa mimba au mtoto pasipo kupewa msaada wa malezi kama chakula, mavazi, elimu, afya n.k. Ni ukweli usiopingika kwamba mtoto hua ni mhathiriwa wa kwanza endapo wazazi mmeamua kuishi hivi.

Wanaume wanahangaika sana kupata nafasi ya kumuona mtoto na mara kadhaa hufanikiwa japo inaweza kuwa mara moja moja.

Yapo maswali unayoweza kujiuliza kufuatia ukinzani anaoonesha mzazi mwenzio juu ya kuumuona mwanao, lakini pamoja na hayo chunga na epuka unapokutana na mtoto wako haijalishi umemtafuta wewe au kakutafuta yeye mtoto kuuliza au kutoa kauli zifuatazo.

Muulize mama yako baba yako.
Kwasababu ya usumbufu na ukinzani anaokuonesha mzazi mwenzio unaingiwa na hisia za kujihoji “kama ni mwanangu kwanini anisumbue/kuzuia mimi kumuona mwanangu? Em ngoja nimuulize mtoto mwenyewe!” na kwa gadhabu au hisia ya huzuni unajikuta unauliza hili swali kwa mtoto.

Mtu pekee wa kukupa majibu sahihi sio mtoto wako bali ni mzazi mwenzio. Bila kujali umri wake swali hii huleta hisia hasi kwa mtoto dhidi yako baba. Mosi, huna upendo kamili kwake kwasababu umeonesha wazi unahofia kama ni mtoto wako wa damu.

Pili, linafungua ukurasa mpya wa kujiuliza au kuwaza kumbe inawezekana huyu sio baba yangu na matokeo yake kuanza punguzua hisia na hamu ya kukutana na baba kwa kuhofia sio baba mzazi. Hii haijalishi umri wa mtoto au jinsia, awe anaanza shule ya awali au kijana anaejitegemea.

Wewe bado mtoto ukikua utajua/ utanielewa. Watoto wengi hupenda kujua sababu au chanzo cha utengano baina ya wazazi wao. Wazazi baadhi wanapoulizwa swali hili hujibu kuwa “wewe bado mtoto ukikua Utajua” wakati wengine wakishusha gazeti kwa kuelezea ubaya wa mama au baba wakimalizia na ukikua utanielewa.

Haya majibu yote hayapaswi kuambiwa mtoto haijalishi umri wake ama jinsia. Kwakua mtoto anawatambua kama wazazi wake basi isiwepo kitu chochote cha kutengua mindset yake, majibu haya ukikua utajua au kumshushia gazeti haitamjenga kwa namna yoyote chanya Zaidi ya kuibua mtazamo mpya na mbaya dhidi ya mzazi wake (mama au baba).

Mfano kumbe mama ni malaya, ukoo wa baba ni wachawi, mama hakuwai mpenda baba, baba alinikataa tangu nikiwa tumboni n.k. Usisahau lengo kuu na dhumuni la kuonana na mwanao ni akue akitambua wewe ni mzazi wake halisi na akupende na ikiwezekana asijepitia ulichopitia wewe na mzazi mwenza mpaka mkahafiki kuachana.

Hatuna jibu moja tunaloweza sema ni sahihi Zaidi ya matumizi ya majibu yasio na ukweli wa moja kwa moja ila yenye busara na kujenga, kwa mfano “ mimi na mama yako tunakupenda sana na tutaendelea kukupenda, majukumu ya kazi ndio yalipelekea mimi kuwa mbali na mama yako”,(haijalishi mama kamlisha sumu kuhusu wewe au lah!) vivohivyo kwa mama “baba yako yupo mbali kwasababu za kazi lakini atakuja na utamuona”

Jawabu hili ni la busara sana kwa faida ya saikolojia na makuzi ya mwanao. Huna sababu ya kuongelea maisha yaliopita kwa mwanano Zaidi ya kuziangalia changamoto zake na kuzitatua kadri Mungu anavyokujalia.

Kwa upande wa wazazi wa kike ni vizuri kujenga/kutengeneza mahusiano ya heshima kwa wazazi wenza kwa maslahi ya mtoto. Kukatalia historia ya maumivu uliopitia mpaka kuachana na mzazi mwenzio inatafsirika kama ubinafsi wa kujali hisia zako na huzijali hisia za mtoto jambo ambalo si sawa.

Huna sababu ya kuzuia au kumdanganya mwanao kwamba baba yake alishafariki. Toa nafasi mwanao aonane na baba yake bila kusahau kuheshimu mahusiano yako mapya kama tayari una mpenzi mwingine.

Kuwa na utaratibu ulio wazi wa mzazi mwenzio kuonana na mwanae ni moja ya jambo lilonaweza kuepusha migongano baina yako, mpenzi mpya na mzazi mwenza.

Naomba kuwasilisha!
 
Nimeongea na mdau hapa kumuuliza majibu ya hoja hii.

Conclusion ni....
Mchawi Pesa

Yani pesa ipo ushindwi kuwa na miji miwili wewe kama mwanaume.

ama hata kama utaachana na bebi mama, basi umempa mali ya kumsaidi aisewe na shida ya kipato, inshort itasaidia hawezi kukusnich kwa mtoto wako.

Na hata mtoto akikua kama unamtumiaga hela tu, atajua baba Ananipenda na kunijali, lipa hata ada tu, awe anakutafuta kukukumbusha kuwa Ada mwakani itakua sh. ngap.

Ukiwa na uchumi mzuri hakuna kitakacho bomoka, na kijana (mtoto) wako hana kazi unaweza muajiri.

Kila kitu kitakua sawa ikitokea shida ni lahis kutatua na kikubwa zaidi ni Akili mtu wangu, the devil is working
 
Upo sahihi mkuu lakini Fikiria pia upo katika hali ya kutokua na pesa za kumudu miji miwili unafanyaje.

Usisahau pia wapo wanawake wanaojimudu na hawahitaji kabisa msaada wako. Sasa nafasi yako kwa mtoto itakua ni ipi wakati kila kitu mama anaprovide.

Just be good and positive to kid. Inasaidia kuweka sawa saikolojia.
 
Upo sahihi mkuu lakini Fikiria pia upo katika hali ya kutokua na pesa za kumudu miji miwili unafanyaje.

Usisahau pia wapo wanawake wanaojimudu na hawahitaji kabisa msaada wako. Sasa nafasi yako kwa mtoto itakua ni ipi wakati kila kitu mama anaprovide.

Just be good and positive to kid. Inasaidia kuweka sawa saikolojia.
Ni kweli.
Hasa wewe baba ukijua kuwa kuna kitu fulani utataka kiwepo kwa mtoto wako kwa sababu huyo ni mwanao na kuna vitu vingi karithi kwako, hasa tabia na uwezo au akili fulani ya maisha.

Kwahiyo wewe kama baba still utatakiwa kuwa supporter kwa mtoto wake hata kama yupo mbali lazima umsikilize mtoto kuwa anapitia changamoto gani au maswali gani ya kimaisha kwa wakati huo.

Kama ni kusoma kuhusu masomo au kitu gani kizuri cha kusomea lazima mawazo ya best father yatahitajika tu.
"big brain matter more"
 
Muhimu pesa tu; wakipata mahitaji muhimu hawatakusumbua
 
Back
Top Bottom