UNA MUDA GANI HUJAOKOTA POCHI YA HELA

UNA MUDA GANI HUJAOKOTA POCHI YA HELA

Nimekaa hapa kibarazani na mbalamwezi hii nikasikia upande wa pili huko kuna watoto wanapigizana kelele

Yanguu,yanguu ....

Nikataka nijue nini hiyo basi nikasogea hadi walipo nikamkamata mmoja nikamuuliza yako nini

Akanionesha sh 50 imekwanguka balaa basi nikajikuta nacheka mwenyewe na kuwaamulia ugomvi ule kisha nikawapa mia mbili wagawane maana walikuwa wanne na watoto wa jirani yangu basi wakafurahi wakasahau ugomvi wao

Basi nikakaa nikawaza hivi mimi mara ya mwisho japo kuiona hela imedondoka ni mwaka gani nikajaribu kupiga hesabu zangu ila sikukumbuka kabisa

Je wew ni lini umeona au kuokota pesa kwa mara ya mwisho
Mwaka juzi
 
Back
Top Bottom