Nina namba ya mwanamke mmoja toka 2008 wa Mamba Marangu.Ndiye mwanamke wangu wa kwanza kumpenda.Kipindi hicho nasomea ualimu Marangu pale.Nilikua mlokole usipime.Demu anakuja Mpaka geto na hatufanyi lolote namwambia nimeokoka Mpaka tuoane.Yule demu aliibiwa na iliniuma sana japo sikufanya naye mapenzi.Niliwaza sana na ilikua karibu na mitihani.Hiyo demu alikua anafanya kazi stationary hapo Marangu mtoni.Ndio ikawa Mara ya kwanza kuachwa na mwanamke.Maumivu yake usipime mana hayalinganishwi na chochote.Wadau waliniweka kikao wakanishauri dogo tulia piga pepa mademu wapo.Toka 2008 Mpaka Leo namba ya Yule mwanamke ipo kichwani.Popote ulipo upendo agiza juisi ya upupu nitalipa