JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Tarehe 4 na 15 Februari ni siku za maadhimsho ya siku ya Saratani na Siku ya Saratani kwa Watoto ulimwenguni. Lengo la maadhimisho hayo ni kuokoa maisha ya mamilioni na kuepusha vifo vinavyoweza kuzuilika kila mwaka kwa kuongeza ufahamu na elimu kuhusu saratani ya utotoni, pamoja na kushinikiza serikali na watu binafsi kote ulimwenguni kuchukua hatua dhidi ya ugonjwa huo.
Jamii Forums kwa kushirikiana na MUHAS, MNH, TLM wameandaa Mjadala utakaofanyika kupitia Clubhouse ya JamiiForums ili kuongeza uelewa juu ya Saratani kwa Watoto Nchini Tanzania
Mjadala huu unatarajiwa kufanyika Jumanne, Februari 15, 2022 ambapo Wataalamu mbalimbali wa Afya wataeleza kwa kina kuhusu Saratani ya Watoto na namna ya kukabiliana nayo.
Kichwa cha mjadala kitakuwa: “Safari ya matibabu kwa Mtoto mwenye Saratani”
Wawasilishaji wa siku hiyo watakuwa:
1. Dk Hadija Mwamtemi - Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Watoto- MNH
2. Ruchius Philbert- Muuguzi-TLM
3. Mwakilishi wa Wagonjwa
4. Mwakilishi Wizara ya Afya
Orodha ya Wanapaneli itakuwa na:
1. Dk Lulu Chirande- Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Damu kwa Watoto na Oncologist (MUHAS)
2. Dk Moses Karashani-Daktari wa magonjwa ya damu kwa watoto na Oncologist (MLOGANZILA)
3. Dk Jane Kaijage- Mtaalamu wa Huduma ya Palliative (TLM)
4. Dk Jerry Ndumbalo- Rais Tanzania Oncology Society
Mjadala huu utajikita kwenye mambo yafuatayo:
1. Jukumu la jamii katika safari ya mgonjwa kupata huduma
2. Wajibu wa watoa huduma za afya
3. Wajibu wa serikali
4. Changamoto na fursa
Je, una swali gani au ungependa kufahamu nini kuhusu hali ya Saratani kwa Watoto?
Karibu ujiunge nasi katika Mjadala huu.
Pia soma:
- News Alert: - Yaliyojiri katika Clubhouse session ya Jamiiforums 15/02/2022: Safari ya matibabu kwa Mtoto mwenye Saratani