Una swali lolote kwa Waziri wa Habari, Dk. Harrison Mwakyembe? Atakuwa live Star TV kuzungumzia Sekta ya Habari na janga la Corona, uliza hochote

Una swali lolote kwa Waziri wa Habari, Dk. Harrison Mwakyembe? Atakuwa live Star TV kuzungumzia Sekta ya Habari na janga la Corona, uliza hochote

Pascal Mayalla,

Ebu nyie msivunje sheria jaman, masuala ya korona yana wasemaji wake, msitutie katika uvunjifu wa sheria.
Tuliisha ambiwa na bwana mkubwa wasemaji juu ya Corona ni President, VP, Majaliwa au Ummi mwalimu, otherwise mjijue mnavunja sheria ambazo wenzetu kadhaa wameshakamatwa na polisi
 
Kuna ushahidi wa video Rais wa SA akiituhumu Tanzania, kama mwenyekiti, kushindwa kuitisha kikao cha nchi wanachama wa SADC kujadili janga la Corona. Nini msimamo wa serikali?
 
Ni nani anayepaswa kujibu hoja ambazo Serikali yetu huwa inatuhumiwa na vyombo vya habari za nje kuwa huwa inabinya Uhuru wa watu kuongea?

Ni nani ambaye huwa yupo kujibu mashambulizi ya Baadhi ya mashirika kuituhumu Tanzania huwa haichukui hatua mapema hasa kwenye mambo yanayohusu uhai wa watu? Mfano, kunatuhuma nyingi SASA kuhusuana na janga hili la Covd 19 kuwa serikali haijachukua hatua yoyote Ile, tuhuma hizi zinatoka kwenye Baadhi ya mashirika ya kimataifa na Sisi kama Watanzania hatuoni ni Nani ambaye ni mahususi Kwa kuondoa hayo makandokando?

Msije mkatuchukulia powa, kama Watanzania wapenda nchi, tunajikuta tunaumizwa Sana na kusakamwa Kwa nchi yetu Kwa mambo ambayo yanapaswa kuwekwa Sawa,

Kama huwa yupo, Kwa nini huwa anachelewa kiasi kwamba mpaka tunachafuka na kuchafuka
 
Maswali kutoka kwa Sifileo kwenda kwa Mh Waziri wa habari Mh Mwakyembe.

1.Yeye kama waziri amechukua hatua gani kuhakikisha wanahabari hasa wale walio bobea katika masuala ya Afya wanapewa elimu ya kutosha katika kuripoti habar za maradhi ya mlipuko mfano Corona,kipindu pindu?

2.Amejipangaje kama waziri katika kuakiki ministrem media haziripoti taarifa za ovyo ili hali zinazidi kuongezeka nchini Tanzania.?

3.kama waziri wa habari anajisiiakiaje anapoona chombo cha habari kinakarbia kufunga milango kisa kukosa mapato ambapo vyombo hivho vidai wizara ambazo yeye ni sehemu ya baraza la mawaziri?

4.Amejilangaje yeye kama waziri kuakikisha anawaweza wanahabari wa Tanzania kujiendeleza kielimu ili kuepuka mapungufu ya uhana habari yatakayo jili baada ya kuanza kusmamia sheria mpya ambapo wanahabari wengi watakosa sifa za kuendelea na kazi kwa mujibu wa sheria hasa sheria mpya?

Mh Waziri ebu tuimbie wimbo mmoja unao upenda?(nataka acheke asiendelee kuchoka na interview).

5.Mh Waziri serikali ina mpango gani kuwaenzi wanahabari nguli ambao wametangulia mbele ya haki huku walikuwa wanahabari wazuri mfano Marine Hassan Marine.?

6.Waziri wa habari hivi unajua kuwa una maafisa habari mizigo hawajui hata wafanye nini? je anatoa tamko gan dhidi yao hao mizigo?

7.Mh Waziri tungependa kujua hatua za mwandishi wa habari wa kujitegemea kama kaka yetu Pascal Mayyala anatakiwa kuwa na sifa gani kwa mujibu wa sheria za nchi yetu?

8.Mh waziri taratibu zipoje za kuwa mwanahabari huru au wa kujitegemea?(ili swali mkuu Pascally kama waweza lijibu sio mbaya).

Zingatio sijajikita kwenye mambo ya corona sana maana mimi najua corona inapita kama mengine yalivyopita.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pascal Mayalla,

Serikali imeishia wapi ktk Sera yake ya kuwataka waandishi wawe na degree, kinachoendelea sekta ya habari ni aibu kusemwa. Mtu kamaliza form 4 na 4 ya D 4 anakuwa mwandishi. Hatari Sana
 
Pascal Mayalla,

Ingekuwa ni mtu huru ningepoteza muda wangu kuweka maswali, ila kwakuwa amemkabidhi Magufuli amshikie akili, natarajia atatoa maelezo mengi kujigamba na blabla kibao za kumsifia mungu wa Tanzania. Huyo ni msomi aliyekabidhi tumbo limfanyie maamuzi. Sioni jipya toka kwake.
 
Dunia nzima, information ni bure. Ni kwa nini serikali inatoza ada kwa TV za online ambazo kimsingi haijawekeza chochote? Haioni kuwa ni kutoza mara 2 kwa mtoa habari, analipa kodi kwenye bando na bado analipishwa ada, na hii inapelekea habari kuwa zinauzwa wakati information ni bure. Pascal Mayalla
 
Muulize kwa nn Tanzanite hayachukuliwi hatua wanapoandika habari za uchochezi?
 
Back
Top Bottom