Una tatizo la kuchelewa kuamka? Tumia njia hizi 10 kuwahi kuamka asubuhi

Joseverest

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2013
Posts
52,812
Reaction score
71,392
1.Kuna chakula/tunda unalolipenda zaidi? Jiwekee zawadi, kwamba ukiamka asubuhi tu cha kwanza ni kula chakula hicho/ tunda/ chokleti nk. Hii itakufanya Utoke kitandani pale tu utakaposhtuka!

2.Iwekee Kipaumbele kazi unayopenda kufanya zaidi iwe ya kwanza kutendeka asubuhi. Utajkuta unatamani kuamka mapema zaidi kuwahi kazi hiyo na siku yako itaenda vizuri

3.Andaa mapema nguo ya kuvaa siku inayofuatia, ili kuwahi jumatatu, andaa nguo ya kuvaa jumapili usiku. Utafiti unaonyesha kuwa asilimia 40 (40%) ya watu huchelewa kutoka kitandani kwa kuwa walitumia muda mwingi kupanga watavaa nguo gani.

4. Anza kupunguza dakika 20 kila siku Taratibu; Kama ulikua unaamka saa mbili kamili, amka saa moja na dakika arobaini, baada ya siku mbili punguza tena dakika ishirini mpaka utakaporidhika

5. Jiwekee Lengo na uwaambie watu. Hii itakufanya ufanye kazi kwa bidii kwa kutaka kuwaonyesha watu kwamba umetimiza lengo lako na utajikuta unawahi kuamka asubuhi

6. Tengeneza “appointment” (Miadi) ya kuonana na mtu asubuhi, utajikuta unawahi kuamka kwa kuogopa kumuangusha mtu huyo.

7. Kama una mtu unaishi nae, tengeneza ratiba ya pamoja kama kufanya mazoezi, maombi, kusoma nk! Itakusaidia kukuongeza morali ya Kuwahi kuamka.

8 Weka saa ya kukuamsha (alarm clock) mbali na kitanda ikiwa na sauti kubwa, ni vizuri ukitumia wimbo uupendao.

9. Muombe mpenzi wako akuamshe kila asubuhi, au jenga tabia ya kumpigia mpenzi wako simu asubuhi

10.Ondoa vitu Vinavyokufanya uchelewe Kuamka mfano; pombe, kahawa na kuwahi kulala usiku.
 
Asante sana mkuu, mie nalala saa 9 na madk usiku asubuhi nachelewaga sana kuamka.
 
Ahaa mim kwa hapo nashukuru nikiwa na shughuli za asubuhi ninajua kujisupervise v.baya lkn siku Niko free k.ukwl napenda tu nijipumzikie mpaka SAA 2 au moja unusu hivi..kwan nakimbilia wapi kama ni siku ya kupumzika...
 
Mimi nimeamua kuwa nalala saa nne kamili usiku....maana Kuna kipindi nilikua nalala saa sita au saba, nikawa nachelewa kuamka, nikawa naamka saa moja asubuhi, nikawa nachelewa kazini... Ila sasa nashukuru.. Sasa hivi saa nne nalala, saa kumi na mbili kasoro naamka
 
Mm ninavyo juwa kwa kawaida mtu Ana takiwa kulala masaa nane kwa siku.
 
Ahaa mim kwa hapo nashukuru nikiwa na shughuli za asubuhi ninajua kujisupervise v.baya lkn siku Niko free k.ukwl napenda tu nijipumzikie mpaka SAA 2 au moja unusu hivi..kwan nakimbilia wapi kama ni siku ya kupumzika...
Yaani ulale kwa saa mbili tu au moja na nusu kati ya saa 24???
 
Mimi nimeamua kuwa nalala saa nne kamili usiku....maana Kuna kipindi nilikua nalala saa sita au saba, nikawa nachelewa kuamka, nikawa naamka saa moja asubuhi, nikawa nachelewa kazini... Ila sasa nashukuru.. Sasa hivi saa nne nalala, saa kumi na mbili kasoro naamka
Umefanya uchaguzi muhimu sana mkuu kwa Afya yako...BRAVO
 
Hata ukiwa na mkopo bank ni lazima uwahi kuamka

Kopa bank kwa nidhamu ya kuamka mapema
Ahahahaha ....Madeni ni balaa yanakupa hamasa ya kufanya kazi kwa bidii ili uje uwalipe chao
 
Back
Top Bottom