Una vigezo vya kazi, kwanini unakosa kazi?

Una vigezo vya kazi, kwanini unakosa kazi?

Mema Tanzania

Member
Joined
Feb 23, 2020
Posts
66
Reaction score
65
Na Abby Msangi

05af3a9347b4f85b950956a3838e324d.jpeg



Tanzania ni moja ya mataifa yenye idadi kubwa ya vijana ikikadiriwa kufikia zaidi ya milioni 25. Kwa wastani zaidi ya vijana laki nane (800,000) huingia katika soko la ajira kila mwaka huku uwezo wa uzalishaji wa kazi zenye tija (ajira rasmi) ni kati ya 50,000 mpaka 60,000 kwa mwaka. Ufinyu wa soko la ajira hupelekea vijana wengi kuingia katika ajira zisizo rasmi kama machinga, mama ntilie, boda boda n.k.

Tatizo la ajira ni kubwa zaidi maeneo ya mijini hasa Dar Es Salaam ukilinganisha na vijijini ambapo vijana wengi wamejiajiri katika kilimo, uvuvi na ufugaji. Waathirika wakubwa zaidi wa uhaba wa ajira ni vijana wahitimu wa vyuo vikuu ambao mfumo wa elimu huwatengeneza kutegemea kuajiriwa.

Kwa muda mrefu nimekuwa nikitumia mtandao wa Twitter kuandika nyuzi (threads) zenye lengo la kusaidia vijana namna bora ya kujiandaa na soko la ajira. Kuna rafiki yangu alinitumia ujumbe binafsi (DM) akiniuliza “Kila niki-apply (omba kazi) siitwi au nikiitwa sifanikiwi kupata kazi despite (mbali) ya kuweka kila kitu sawa kwenye CV na kwenye barua”. Hivyo tuna shindwa wapi?


KUWA NA VIGEZO VYA JUU (OVER QUALIFIED) NA KUWA NA VIGEZO VYA CHINI (UNDER QUALIFIED)

Kuna vigezo viwili vikubwa kwa wewe unayeomba kazi dhidi ya kazi husika iliyotangazwa ambavyo ni Over Qualified na Under Qualified. Tuanze kunyambua kwa mifano halisi. Unaweza kuwa Over Qualified (vigezo vya juu) lakini haufuzi (qualify) kama mtu sahihi wa kazi husika.

Tangazo la kazi imetangazwa ya masoko (Marketing) ya kampuni X (Mfano tu), lakini wanataka mtu mwenye diploma na awe na uzoefu wa kazi miaka 5. Wewe una shahada (degree) ya masoko na uzoefu wa kazi miaka 5. Unaomba kazi lakini unakosa. Kwanini unakosa?

I. Kampuni ina bajeti ya kumlipa mtu wa diploma tu.

II. Tangazo la kazi linataka msaidizi (Assistant) cheo kinachomfaa mtu mwenye kiwango cha diploma na mtu mwenye shahada cheo chake cha kiofisi ni Afisa.

Au nafasi ya kazi imetangazwa ya masoko na anahitajika mtu mwenye shahada ya masoko. Lakini wewe una shahada ya utawala wa umma na shahada ya uzamili (masters degree) ya masoko na uzoefu wa kazi miaka 5. Kiuhalisia una uwezakano mkubwa sana wa kukosa. Waliozidi vigezo (qualifications) wanasumbua baada ya kupata kazi hasa upande wa maslahi/kujiona hawapewi thamani stahiki (under valued).

Over qualified iliyo sahihi ni ile tangazo la kazi linahitaji mtu mwenye digrii ya masoko na uzoefu wa mwaka mmoja, wewe unaomba ukiwa na digrii inayofanana na uzoefu wa miaka mitatu. Tena umeongeza na mafunzo (training) na unajua mfumo vizuri. Kuwa Under qualified hapo ndio tatizo lilipo sana. Utatambua vipi kama hapa nipo Under qualified kwa kazi iliyotangazwa?

attorneye28094gifts-at-work.jpg

Tambua nafasi kwenye maombi ya kazi yaliyotangazwa. Mfano Director, Manager, Principle, Senior, Officer au Assistant. Director, Manager, Principle hao ni watu walio kazini kwa miaka zaidi ya 7. Senior mfano ni miaka 6, Officer kuanzia miaka 1 mpaka 5. Maana kila hatua ina kiwango, kwa Officer ukitoka daraja la 1 na 2 unapanda Senior. Kuna Senior 1 na 2 ambao kupanda kiwango ni kila baada ya miaka 4 (huu ni muongozo kutoka serikalini).

Sasa unakuta kijana ana digrii kutoka chuo (fresh from school) na ameona kazi ya Meneja Ugavi (Procurement Manager) ana tuma maombi ya kazi. Bila shaka utapigwa nyundo mubashara ya utosini. Hata kwenye orodha fupi (shortlisting) hautafika. Japo kuna kampuni nyingine meneja ni cheo cha kawaida kama tunavyoitana boss/chief huku kitaa mfano supermarket. Mtu yeyote mwenye shahada anaanza na nafasi ya Officer, diploma na cheti mara nyingi huanza na msaidizi (Assistant).

TUNAPOSHINDWA NA NINI CHA KUFANYA

Tunakosea pale unaona tangazzo la kazi anahitajika Manager, Principle, au Director unaomba hiyo kazi ilihali ndio kwanza umemaliza shahada kutoka chuo kikuu flani. Msukumo ni kwa sababu uliambiwa “we tuma, kwani nini”.

Ujanja ni kufanya nini?

Una stashahada ya uzamili (masters degree) na wanataka wa shahada, kwenye CV yako usiweke masters kwanza. Masters yako ipeleke ukiwa ushaanza kazi au kwa kazi inayohitaji diploma halafu una shahada, kama hukusoma diploma usithubutu kutuma maombi. Ikiwa unayo weka diploma yako, mbeleni weka shahada yako.

Lazima watu wafahamu unaweza kufanya kila kilicho sahihi na bado usipate kazi. Unaweza ukaweka CV yako sawa na bado kila ukituma maombi hupati kazi. Ila kitendo cha kuitwa kwenye usaili basi wewe una nafasi kubwa. Hivyo tuendelee kujaribu, kutokata tamaa na tuendelee kumuomba Mungu.

Sio kila nilicho kiandika humu kinaweza kuwa sahihi ila unaweza kukosa kigezo kimoja tu (inaweza kuwa uzoefu au vigezo vya elimu), na CV yako wakaiweka pembeni na simu wasikupigie.

Abby Msangi ni mshauri wa vijana kwa masuala yanayohusu kazi na ajira. Unaweza kumfuatilia kwa kubofya kiunganishi hiki cha Twitter.
 
Bandiko zuri sana mkuu

Hii kauli ".....wee omba tu kwani shingapi...." imecost watu wengi sana

Umetuma maomba zaidi ya 20 ujapata ata moja unatafuta mchawi kumbe mchawi ni wewe mwenyew kwa kushindwa kwenda na beat la mchezo
 
Back
Top Bottom