Unaanzaje kuahirisha sherehe za Uhuru? Ahirisheni na sherehe za Muungano

Unaanzaje kuahirisha sherehe za Uhuru? Ahirisheni na sherehe za Muungano

Carlos The Jackal

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2017
Posts
25,725
Reaction score
78,589
Yaani inakuajekuaje mtu unaahirisha Sherehe za Uhuru? Uhuru? UHURU?

Sababu kubwa? Pesa ziende kwenye MAENDELEO?

Yaan Mnaacha mafisadi yanajipigia, Mnajipa masafari Kila kukicha, Mnajipa matumizi makubwa kupindukia, wafanyabiashara mmewaita wafanyabiashara wazuri, alafu from nowhere, Unazuia Sherehe za Uhuru ,Et Pesa iende Mahali Fulani?

Hivi nyie Vyombo vya Dola, Hata Nyinyi hamjui umuhimu wa Sherehe hizi? Kweli kabisa?

Kwamba, mnaomshauri mama, na nyinyi kabisa na ndevu zenu, kende na matiti Kifuani, Kabisa kabisaaa, mnaamua kumpa go ahead?

SHEREHE ZA UHURU? Hivi nyie Uhuru wa Tanganyika mnauchukuliaje?

Wakati Mataifa kama Russia, kwa sasa likipitia vita ya kulinda Tunu zake za kihistoria kwa vizazi, wakitumia mabilioni Kwa mabilioni kuazimisha Kumbukumbu za matukio yao, sisi tunakua mstari wa mbele kabisaaa kusema tunaahirisha Sherehe hizi, na hizo Pesa ziende. SHAME ON YOU!

Mnalipa majizi ya hela za walal hoi, mabilioni na mabilioni, alafu leo hii unaahirisha sherehe za UHURU kisa Pesa ziende Mahali Fulani?

Kwamba hamjui Faida ya kufanya Kumbukumbu Kila mwaka za Sherehe hizi ambazo zinasimama Kihistoria?

TENA SHEREHE ZA UHURU?

Ya kwamba mnaihirisha kutambulika na kukumbukwa Kwa juhudi za Mababu zetu walojitoa kupambana Kwa hali, mali, jasho, matone na Damu?

Ama kweli TAIFA likiongozwa na asokua Hekima, njia zake zote huelekea shimoni.

Aliyemwelewa anisaidie.
 
Na TAIFA linalo waandishi wa habari.

Waandishi wa habari wanaojinasibu ni magwiji wa habari, huku magazetin kwao wakijaza habari za wasaniii wa bongo fleva.

Waandishi wasoandika kuhusu Tunu zetu hizi!

Waandishi wanaoandika juu ya umuhim wakuendelea kuenzi Tamaduni zetu hizi!
 
Hawa jamaa ni wajinga kweli.

Hivi kweli Mwenge na Uhuru, wapi wanatumia Pesa zzetu Hovyo?

Et Mwenge unaenda kuzifungua miradi ambayo ingeweza zinduliwa na Mkuu wa wilaya? Mwenge ambao umechangia ongezeko la Maambukizi ya VVU

Unaahirisha Shere za UHURU KWELI? UHURU WA NCHI?
 
Halafu in kama unafanya watu watoto wa dogo- na by the way Serikali inatuchukulia hivyo yani hiyo statement no sawa na kichota maji kwenye bwawa na kuyapeleka ziwani.
 
What is there to celebrate? Hata hiyo Muungano nayo nadhani hizi sherehe ziwe zina adhimishwa in decades..or half a decade at least, miaka 65 ..70.. 80. Binafsi kama mzaliwa wa miaka ya baada ya uhuru, after grasping the whole concept of uhuru wa bendera tuliopata toka kwa muingereza naona kama taifa bado tuna mambo jadidifu ya kuconcentrate nayo na kuyashupalia kimustakabali kuliko sherehe na mbwembwe za Kila mwaka.

Sent from my Nokia C30 using JamiiForums mobile app
 
Then kesho anaenda kukopa na kugawa huo mkopo na wakwao kisha deni tulipe watanganyika[emoji24]
Huku wanaingia ikulu kwao mtanganyika ht ajira ya kufagia hupewi, laana gani hii ya kukumbatia laana? [emoji848]
 
Kwahiyo hizo sherehe zikishafanyika ndio Tz tutakuwa huru kweli??, Kuna Mambo yakupigania sio haya matamasha ya CCM ebooh!!
 
Hizo sherehe za uhuru zitamsaidia nini mwanchi was kawaida,hiyo midahalo na makongamano mbona yanatosha Kwa wananchi was kawaida kuliko kuharibu pesa Kwa masherehe na magwaride hizo shule zitakazofaidika na pesa hizo Kwa matengezo hayo zitasaidia sana wananchi katika elimu za watoto wao kuliko kuharibu pesa zote hizo kwa sherehe zisizokuwa na faida yoyote Kwa jamii.
 
Hizo sherehe za uhuru zitamsaidia nini mwanchi was kawaida, hiyo midahalo na makongamano mbona yanatosha Kwa wananchi wa kawaida kuliko kuharibu pesa Kwa masherehe na magwaride hizo shule zitakazofaidika na pesa hizo Kwa matengezo hayo zitasaidia sana wananchi katika elimu za watoto wao kuliko kuharibu pesa zote hizo kwa sherehe zisizokuwa na faida yoyote Kwa jamii.

Siku hizi aliyesoma hana tofauti na asiyesoma. Hizo shule zao hazina faida yoyote.
 
Kuna muda watanganyika tunakuwa mafala sana kwenye mambo Fulani Fulani.

BringBackTanganyika.

Ingetokea nakuwa Rais wa hii nchi paaap!!! Nairudishs Tanganyika kwanza.

Tanganyika imekufa na Zanzibar bado Iko.

Ujinga mtupu.
 
Embu imagine waandishi wetu wa Faisal anaenda azam. Unategemea abali kweli. Baasha baba ni shida
 
Hizo sherehe za uhuru zitamsaidia nini mwanchi was kawaida,hiyo midahalo na makongamano mbona yanatosha Kwa wananchi was kawaida kuliko kuharibu pesa Kwa masherehe na magwaride hizo shule zitakazofaidika na pesa hizo Kwa matengezo hayo zitasaidia sana wananchi katika elimu za watoto wao kuliko kuharibu pesa zote hizo kwa sherehe zisizokuwa na faida yoyote Kwa jamii.
Hizo pesa zinaenda kweli huko wanapodai wanazipeleka ?
 
Huwez sikia mapinduzi day imeahirishwa hata siku moja, Ni sherehe ambayo inafanyika January Ila shamra shamra zake zinaanza mwez wa 12 Ni sherehe kubwa Sana kwa wazanzibar Ila Uhuru wa Tanganyika unaonekana hauna maana
 
Huwez sikia mapinduzi day imeahirishwa hata siku moja, Ni sherehe ambaya inafanyika February Ila shamra shamra zake zinaanza mwez wa 12 Ni sherehe kubwa Sana kwa wazanzibar Ila Uhuru wa Tanganyika unaonekana hauna maana
Ndio maana tunataka katiba mpya
 
Back
Top Bottom