Unaazaje kumueleza Mkeo kuwa una mtoto nje ya ndoa, Mwanamke unalipokeaje kutoka kwa Mumeo?

Unaazaje kumueleza Mkeo kuwa una mtoto nje ya ndoa, Mwanamke unalipokeaje kutoka kwa Mumeo?

GAZETI

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2011
Posts
5,286
Reaction score
6,736
Imetokea kwa baba yangu Mdogo, kwa sasa mtoto wake wa nje ya ndoa yuko mwaka wa pili
Hapo UDSM lakini mkewe hajui..............

Si jambo zuri, hakika si jambo zuri, Lakini imeshatokea unafanyaje, yaani unalifikisha
vipi kwa mkeo? Unaanzaanzaje?
Na wewe Mwanamke unalipokeaje? Uko tayari kumchukulia huyo mtoto kama mwanao?
 
Katika mambo ambayo ni magumu kwa wanawake kuelewa ni hili

Kama atakuelewa kirahisi basi huyo umri wake utakuwa umeenda sana na atakuwa hajali sana mambo ya watoto kwasababu huenda hawazi kuzaa tena au ameshachoka kurukaruka huko lakini kama ni mbichi itakuwa ngumu sana,wanawake hawakubali kirahisi kuishi na mwanaume ambae ana watoto au mtoto

Hivyo sishangai huyo baba yako mdogo kuamua kumficha mkewe kuhusiana na huyo mtoto!
 
nivigumu kueleza ukweli kwamba una mtoto nje ya ndoa lakini ukweli ni lazima amfikishie mkewe na yy aelewe mana ishatokea
 
Kama mtoto alipatikana kabla hajaingia kwenye ndoa ni jambo la kawaida kwa waelewa haina aja ya kushindwa kusema ukweli mapema, shida naona iko pale mtoto wa nje kupatikana tukiwa kwenye ndoa, na hata hivyo ikishatokea, imetokea hata moto uwake vipi ukweli hauwezi kubadilika ni kusuluhisha mambo kimya kimya maisha yanasonga.
 
GAZETI Mume wangu, Vipi ikitokea umesafiri safari ya mwaka mmoja au
Miwili ukanikuta nimezaa na mwanaume mwingine, uko Tayari kumpokea
huyo mtoto kama mwanao Pia?
Mcharuko kuna wanaume walienda vitani Dhidi ya Idi Amini waliporudi
walikuta wake zao wakiwa na watoto lakini haikuwa shida Maisha yaliendelea.
 
Inategemea umri wa mtoto "wa nje" na hao "wa ndani" pia umri wa wazazi wa pande zote!!!!!!
Pia inategemea sana vipato vya wazazi wa pande zote!!!!!
 
Inategemea umri wa mtoto "wa nje" na hao "wa ndani" pia umri wa wazazi wa pande zote!!!!!!
Pia inategemea sana vipato vya wazazi wa pande zote!!!!!

Hapo kwenye vipato sijakuelewa mkuu, sijui inategemea vipi??
 
Kwanza unamwandaa mkeo kisaikolojia kwa kumtega na vimaswali vinavyohusiana na watoto wa nje, itategemeana na majibu atakayokupa, pili unamwomba samahan kwa kosa ulotenda miaka ilopita ila hutaj ni kosa lip, unapotezea zaid ya miez 6 hiv unarudia tena kuomba msamaha, hapa lazima akubane ili umwambie ni kosa gani
 
Hapo kwenye vipato sijakuelewa mkuu, sijui inategemea vipi??

Kuna wanaoona sungura mdogo sasa ukiongeza walaji si itakuwa issue hapo!!!?????
Kama unajitosheleza kwa kipato na ukawa una mtoto nje hapo suala ni "infedility" tu ila ukiwa pangu pakavu then ukazaa nje asee lazima ukutane na "kama we kidume tunza hawa......hawa tu wanakutoa jasho halafu ukaongeze mizigo hapa!!!!!!!..na maneno kama hayo!!!!!!
 
Hakuna ustaarabu wa aina hiyo, hapo solution ni kuondoka tu.

kuondoka kisa mtoto wa nje ndo sln gani hiyo? Kweli mwanamke -------- hutawanya familia yake kwa mikono yake! Kwa mfano tayari wana watoto, yule wa nje alipatikana kabla hawajawa kwenye ndoa au hata kama wakiwa kwenye ndoa. Huyu mwanamke cha kumuondoa kwenye ndoa ni nini na wakati huo mapenzi yapo kati yao?
 
mhhhh till second year???si zaidi ya miaka 20 hyo?afanye afanyavyo heshima ya wife aendelee kuweka mbele kama tai
 
Yaani mie kama ni mtoto, niachwe hadi nifikee chuo kikuu ndio nitambulishwe? Nawakataa wote baba na familia yake siwataki tena.

Wa nini hata sina nao historia, aku nabaki na wale walle wwalionilea wananitosha kabisa.
 
Inategemea huyo mtoto alipatikana kabla au baada ya mahusiano na mkeo. Kama alipatikana kabla ina ahueni kidogo ingawa ulipaswa umpe taarifa mapema pia ila kama alipatikana baada!! Lazima uone rangi zote!
Umri wa mtoto pia unahusika sana maana kama ni mdogo itabidi mjadili malezi yake na kama akilelewa na mama yake mke anaweza ahofie idadi ya hao watoto kuongezeka!!!
Ukisubiri akikua pia ule ukaribu na nduguze unakuwa mdogo sana,wata share jina tu la baba ila ukaribu baina yao huwa haupo.
Kuzaa nje ya ndoa kunaathiri wengi hasa watoto,wanandoa tuwe makini sana hasa wanaume wanaojiona wako salama kwa sababu mimba hawabebi wao. Tufikiri kabla ya kuamua.
 
28d672f02fL.jpg
 
Yaani mie kama ni mtoto, niachwe hadi nifikee chuo kikuu ndio nitambulishwe? Nawakataa wote baba na familia yake siwataki tena.

Wa nini hata sina nao historia, aku nabaki na wale walle wwalionilea wananitosha kabisa.

Kuna mdada alizimia baada ya kufuatwa na mzee ofisini hawafahamiani wala nini baada ya salamu mzee akamwambia "mimi ndio baba yako mzazi" yule dada alikuwa amelelewa na mzee aliyemuoa marehemu mama yake baada ya wazazi kukosana yeye akiwa mdogo kabisa na mzee kutawanyika na zake !!!!!!!! Amekuwa maisha yote (akijua) yule aliyemlea ndiye baba yake despite the fact aliambiwa na mama yake just before her death kuwa yule sio biological father wake but mdada alimuambia marehemu mama yake kuwa kama kanilea na kunikubali kwa maisha yote huyu ndio baba yangu!!!!
 
Yaani mie kama ni mtoto, niachwe hadi nifikee chuo kikuu ndio nitambulishwe? Nawakataa wote baba na familia yake siwataki tena.

Wa nini hata sina nao historia, aku nabaki na wale walle wwalionilea wananitosha kabisa.
Kitufe cha like sikioni!!! Ila unaistahili.
 
Back
Top Bottom