Unabii umeanza kutimia kuhusu Uchaguzi kenya

Truths

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2017
Posts
1,494
Reaction score
1,504
Mgombea Urais wa Kenya anaeungwa mkono na ngome ya NASA, Raila Odinga amepinga matokeo yanayoendelea kutangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi ya nchi hiyo (IEBC).

Odinga ameeleza kuwa kutokana na kutokuwepo fomu hizo ni vigumu kubaini matokeo yanayotangazwa na IEBC yanatoka wapi.

“Mfumo umeachwa na sasa ni mitambo ndio inayopiga kura. IEBC wamesema kwamba hakuna chama chochote kilichopinga matokeo. Lakini vyama vitapingaje matokeo bila kujua asili yake? Ni fomu namba 34A pekee inazoonesha chanzo cha matokeo,” amesema Odinga.

“Kwa hivyo, tunakataa matokeo yote yaliyotangazwa kwa sasa na kuitaka tume ya IEBC itoe fomu 34A za kila kituo kabla ya matokeo zaidi kutangazwa,” aliongeza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani kuna haja ya kutoa maana ya "demokrasia ya vyama vingi, "
Ila ninavyoona sio demokrasia ambayo ni lazima vyama vya upinzani vishinde pekee lakini pia vionekana vinashiriki katika huo mchakato wa kushindwa.
Eventually, free and fair elections are too abstract in these undeveloping countries.
 
Nilifundishwa shule kuwa mfumo wa vyama vingi africa ulilazimishwa na woldi benki haukuwa utashi wetu
 
Unaandaa uchaguzi wewe. Muhimili wako umejikita mita 800 chini ya usawa wa bahari na ulipa salary na allowance za watu wa Tume ya Ulanguzi. Una jeshi, usalama wa Taifa na the so called intelijensia. Unaanzaje kushindwa kwa mfano?
 
Wazichape kama ile 2007 Sie tutawapokea huku kama refugees[emoji41] [emoji41] [emoji41] [emoji41]
 
Nilifundishwa shule kuwa mfumo wa vyama vingi africa ulilazimishwa na woldi benki haukuwa utashi wetu

Je kwako tatizo kwako ni mfumo au tabia zetu waafrika kulazimisha madaraka? Mbona nchi hizohizo ndio zilitulazimisha elimu ya darasani na hatuoni ni shida?
 
Aisee kumbe wakina jecha ni wengi sana afrika mashariki
 
Mgombea Urais wa Kenya anaeungwa mkono na ngome ya NASA, Raila Odinga amepinga matokeo yanayoendelea kutangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi ya nchi hiyo (IEBC).

Odinga ameeleza kuwa kutokana na kutokuwepo fomu hizo ni vigumu kubaini matokeo yanayotangazwa na IEBC yanatoka wapi.

“Mfumo umeachwa na sasa ni mitambo ndio inayopiga kura. IEBC wamesema kwamba hakuna chama chochote kilichopinga matokeo. Lakini vyama vitapingaje matokeo bila kujua asili yake? Ni fomu namba 34A pekee inazoonesha chanzo cha matokeo,” amesema Odinga.

“Kwa hivyo, tunakataa matokeo yote yaliyotangazwa kwa sasa na kuitaka tume ya IEBC itoe fomu 34A za kila kituo kabla ya matokeo zaidi kutangazwa,” aliongeza.

Sent using Jamii Forums mobile app

???? 2015. ????

Sent using Jamii Forums mobile app
2020

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahaaa ndiyo cdm wanalazimisha tume huru ya uchaguzi kumbe ni tume binafsi ya chama tawala cha aliyeko madarakani hapa ni janja janja tu hiyo tume Kenyatta anaithibiti mwenyewe hakuna cha tume huru
 
Dhana ya "demokrasia" kwa Africa ni ubatili mtupu, tuendelee kudanganywa kuwa kuna demokrasia ili walioshika kwenye mpini waendelee kula.
 
kwani huu mfumo kwao ni mpya...? si walishaupitia na kujua namna unavyofanyakazi....? huo ni uchochezi
 
Back
Top Bottom