Unabii wa Polepole: Corona imekwisha na Chadema imesambaratika na kuishiwa pumzi


Mkuu wewe si daktari, hata udaktari wa JF huna.
Sasa Corona imeisha kwa utafiti gani?
Hebu uweke utafiti huo hapa hadharani ili tukuamini.
 
Mnakataa kuwapokea wagonjwa, watu wanafia majumbani, na wanaofia hospitalini mnawazika kama mbwa...corona imekwisha
 
Uo ndio Ukweli. Makamanda chali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Agiza kahawa kun a wazee wanakuja hapo sasa hivi na mifuko ya kashata
 
Sijapata ona marehemu anayewapa presha walio Hai kama marehemu Chadema. Marehemu huyu ni wa pekee sana.Inaweza kuwa hajafa na hana dalili za kufa ila ninachojua mtu anapokaribia kufa hutapatapa,yawezekana hawa wanaoona wapo Hai ndo wanatapatapa sasa,mbona hawalali?usiku na mchana wao hawaishi kumtaja marehemu wao feki.Lakini sasa inadhihirisha wazi mambo Yale kuteka watu,kupiga watu risasi,kesi za ajabu ajabu ni harakati za kutamani kuona maiti ya marehemu wao feki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acheni siass za maji taka Corona imeisha Viongozi wanavaa Barakoa za nini? Shule za msingi kwanini hazijafunguliwa au mnawadanganya watanzania ili wafe?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani comrade bhana..Hivi katika maadui na matatizo yanayo wakumba watanzania na CHADEMA ipo kumbe.
 
Kuna vitu sasa hivi unaweza kujikuta unajichekea kimoyo moyo.
 
Falsafa mujarabu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…