Kuna vitu ni kweli, mfano umeanzisha shughuli fulani ya biashara, ikakua mpaka imekupa ulichonacho sasa kwenye maisha yako.Yaani ana maanisha kila kitu kinachokutokea umekianzisha wewe mwenyewe 🤔
Atueleweshe namna mtu anavyoanzisha hayo mambo
Mf: mtu aliezaliwa ni kipofu au ana ulemavu fulani huyu alinzishaje ?
Yaani kama kila kitu ni matokea nani
angeanzisha vitu negative kwake
Una kuta mtu ana henyeka na maisha
,Magonjwa , Uchumi Nk... ndio kusema huyu nae ni matokeo ya alichoanzisha 🤔
Mtoa mada Thecoder
Hebu nyoosha maelezo
Hapa mleta mada apatazame upyaSema anachokosea ni kuifanya hii kanuni ni ya lazima kwa kusema "unachopitia sasa ni matokeo ya kile ambacho ulikianzisha zamani" wakati kuna mengine unayapitia na wala hukuanzisha wewe.
Mkulima anapolima huwa anatenga mbegu bora na zile ambazo si Bora zile Bora atazipanda kwenye eneo ambalo anajua rutuba yake ipo vizuri kwa asilimia zote na zile ambazo sio bora anaenda kuziweka kwenye eneo ambalo rutuba yake ni ya pata potea ili zipambane na hali ya hapo zenyewe.Unaposema kila unachopitia sasa ni matokeo ya ulichoanzisha, unafanya Bias na Generalization, siyo kila kitu unachopitia sasa ni matokeo ya ulichokianzisha, mfano:
Ukizaliwa kwenye familia yenye utajiri, ukafundishwa biashara, ukawa tajiri, hayo ni matokeo ya ulichokianzisha au ulicho anzishiwa?
Mtu aliyezaliwa bila uwezo wa kuona au mtu aliyepata ajali, hiyo hali inaathiri maisha yake sababu aliianzisha mwenywe?
Mtu anayeishi kwenye vita akalazimika kukimbia na kuipoteza fursa nzuri ya biashara naye anapitia alichokianzisha?
Kuna watu wana saratani na hawakupanga kuwa nayo, wanachopitia kwasasa ni kitu walichokianzisha?
Niskilize, unapopanda mbegu ikiota tu unajua ukomo wa wake ni lini, kwa maana kuna mbegu za miezi mitatu, kuna mbegu za miezi sita na kuendelea, na hii counting huanza punde tu pale mbegu inapoota.Yaani ana maanisha kila kitu kinachokutokea umekianzisha wewe mwenyewe 🤔
Atueleweshe namna mtu anavyoanzisha hayo mambo
Mf: mtu aliezaliwa ni kipofu au ana ulemavu fulani huyu alinzishaje ?
Yaani kama kila kitu ni matokea nani
angeanzisha vitu negative kwake
Una kuta mtu ana henyeka na maisha
,Magonjwa , Uchumi Nk... ndio kusema huyu nae ni matokeo ya alichoanzisha 🤔
Mtoa mada Thecoder
Hebu nyoosha maelezo
Hahahahaaa pole kwa kuumwa mafua ila wewe ndio hujui kama umepanga kuzaliwa wapi kwakua huna kumbukumbu ya maisha yako ya nyuma ila hatima iliyopo ndani mwako na namna ya kwenda kuifikia uliichagua mwenyewe, huo ndio uhalisia.Ikiwa tu mtu huwezi kupanga uzaliwe au usizaliwe
na huna hata option ya kusema uzaliwe na nani masikini au tajiri
uzaliwe ulaya au africa uwe mweupe au mweusi
sasa unawezaje kuanzisha matokeo yako ya baadae?
Kicwa kinauma kwa mafua makali
Na wewe mtoa mada unataka kuhakikisha nachanganyikiwa🙌
Mbona wewe unapanda punje moja ya muhindi ila zinakuja kutoka zaidi ya moja? Universe inasheria zake za lazima na zile za hiyari moja ya sheria ya universe ni uchavushaji ni kama Dunia inavyofanya mizunguko miwili katika wakati mmoja na ndio hivyo hivyo wewe ulivyo.Huyu mtu ana mawazo ya hovyo sana. Sasa km watu wanaokufa ndio wanaorudi Duniani, ina maana toka maisha yaanze Duniani kulikuwa na idadi hiyo hiyo ya watu ndio wanaojirudia kuzaliwa. Mbona idadi ya watu Duniani inaongezeka. Hivi hawa watu wanaodai kila siku sijui kuna roho, mara zinaenda motoni au mbinguni mtu akifa mbona hawaongelei roho za wanyama zinaenda wapi wakifa? Au binadamu tunafikiri roho zetu Zina thamani sana kuliko wanyama kwa sababu gn, ufahamu tulio nao? Km ufahamu, wale binadamu wanaozaliwa wakiwa na ulemavu wa ubongo kiasi ambacho ufahamu wao wakati mwingine huzidiwa hata na ufahamu wa wanyama, roho zao huenda wapi? Huyu anayedai kila kinachokutokea ulikipanga ww zamani, wanaozaliwa utumbo nje au bila miguu walipangajr hali hiyo? Na ili upange jambo lazima uwe na umri na akili tumamu ya kuweza kuamua mambo, wanaokufa wakiwa watt wachanga walipangiwa na nani?
Nakubaliana na Kiranga. Anatakiwa athibitishe madai yake na aondoe neno "Imani" katika mafundisho yake. Tunataka kuelewa na kufahamu na siyo kuamini. Km kuamini, kuna mwingine atakuja kutuambia labda yeye ndiye anayepanga roho gani izaliwe leo na nyingine kesho. Naye ataka tumuani. Athibitishe hayo anayoyahubiri tuelewe kwa ushahidi. Hiyo roho ipo wp katika mwili wa binadamu
Umesema vizuri sana, sasa umeona hii ndio ile ambayo Dunia inajizungusha kwenye muhimili wake so matokeo yake yanaonekana papo kwa papo ila Dunia inapolizunguka jua matokeo yake huwa ni msimu hadi msimu.Kuna vitu ni kweli, mfano umeanzisha shughuli fulani ya biashara, ikakua mpaka imekupa ulichonacho sasa kwenye maisha yako.
Au mfano ulianza mazoezi gym, mpaka ulimefikia stage unabody iliyojazia vizuri hapo kweli ni matokeo ya ulichokianzisha.
Au labda pesa yako yote ilikuwa inaishia kwenye kamari ikapelekea hali yako ya maisha ya sasa kuwa ngumu, hapa kweli unakuwa responsible for your action.
Sema anachokosea ni kuifanya hii kanuni ni ya lazima kwa kusema "unachopitia sasa ni matokeo ya kile ambacho ulikianzisha zamani" wakati kuna mengine unayapitia na wala hukuanzisha wewe.
Duh aisee🙌Hahahahaaa pole kwa kuumwa mafua ila wewe ndio hujui kama umepanga kuzaliwa wapi kwakua huna kumbukumbu ya maisha yako ya nyuma ila hatima iliyopo ndani mwako na namna ya kwenda kuifikia uliichagua mwenyewe, huo ndio uhalisia.
Weka link ya uzi huoKitu ambacho hamtakiwi kusahau ni kwamba hizi vurugu zooote zinazoendelea duniani ni mapambano ya Kila mtu kuufuata mwanga ulipo mithiri ya mmea ufanyavyo.
Na katika hizo harakati za kuutafuta mwanga ulipo ndio vita inapokuja na ndio maana nikawaletea ule Uzi wa dunia ni uwanja wa vita za kihatima.
Kwasababu hatima ni uelekeo wa maisha ya Kila mtu kwa maana nyingine hatima mfano wake ni mwanga.
Na nilisema indicator moja wapo inayoweza kukuonesha mtu anazielekea njia za kihatima ni urahisi wa mambo kwenye kile anachokifanya, yaani hutumii nguvu nyingi ila unaona matokeo, so pesa ni indicator kuu.
Ndio maana kupitia hapo kuna msemo kama jasho la mtu haliendi bure kwa maana pesa imebeba hustling za kihatima za mtu, so mtu akisema jasho la mtu haliendi bure it means huwezi izulumu hatima ya mtu mwingine na ukabaki kuwa salama.
Sasa hapa haimaanishi ya kwamba utakufa au utapata madhara yanayoonekana usiku na mchana ila ni yale ya kimsimu.
Weka link ya uzi huo
UmeuaNatumai mko salama.
Kama kichwa cha habari kinavyosema kwamba dunia ni uwanja wa vita za hatima kwahiyo kila mtu ambae yuko hapa duniani anapaswa kujua kwamba yuko vitani na swala la kushinda au kushindwa ni juu ya mtu mwenyewe.
Sasa iko hivi...
Kimsingi ni kwamba kila mwanadamu ambae yuko kwenye hii dunia hayupo hapa kwa bahati mbaya na inawezekana wazazi waliomzaa mtu huyo wanaamini wamemleta huyo mtu hapa duniani kibahati mbaya ila kiroho hakuna kitu kinachoitwa bahati mbaya.
Maadam umezaliwa na uko hapa duniani basi kaa ukijua kuna mission unatakiwa uitimize na hii mission ndio...
- Thecoder
- uwanja wa vita
- Replies: 169
- Forum: Jamii Intelligence