Unachukuliaje tabia ya watu kubeba vyakula au vinywaji toka kwenye masherehe na kurudi navyo nyumbani

I am Groot

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2018
Posts
3,929
Reaction score
10,747
Kama utambulisho unavyoeleza, hii tabia imeonekana kuzoeleka na hata kuonekana ni jambo la kawaida kwa jamii nyingi za kiafrika na huwezi kuona vitu kama hivyo katika nchi za wenzetu kwani kwa kufanya hivyo wao wanaona ni kutokustaharabika.

Je, kwako binafsi inauchukuliaje tabia hii?
Je, ulishawahi kubeba chakula au kinywaji toka kwenye sherehe nini sababu?

Tushee maoni yetu wadau.
 
Poa tu mbona mkuu,,, na jana tu kulikuwa na mwanangu ana shughuli yake nimebeba msosi mpaka vinywaji,, au we unatuchukuliaje mana umetufungulia na uzi kabisa
 
Sioni tatizo

Wengi wetu tumetokea familia za Msiba kwa Jirani, Mama usipike
 
Ni kukosa ustaarabu tu.
Kifupi ni tabia mbaya sana.
 
Kama utambulisho unavyoeleza, hii tabia imeonekana kuzoeleka na hata kuonekana ni jambo la kawaida kwa jamii nyingi za kiafrika na huwezi kuona vitu kama hivyo katika nchi za wenzetu kwani kwa kufanya hivyo wao wanaona ni kutokustaharabika.

Je, kwako binafsi inauchukuliaje tabia hii?
Je, ulishawahi kubeba chakula au kinywaji toka kwenye sherehe nini sababu?

Tushee maoni yetu wadau.
1. ulafi na kutokuwa na chembe ya aibu hasa kwa wale ambao nyumbani vyakula wanavyo.

2. uchungu wa kupigwa pesa ndefu ya mchango hasa kwenye maharusi na alichokula anaona hakitoshi hela aliotoa.

3. wengine wanakumbuka familia, anajua alichowaachia watoto nyumbani sicho kile alichokula pale kwenye sherehe sasa anataka watoto wakale kile alichokula.ni upendo t u.
 
Umenikumbusha yule bibie alivyomwaga kande kwenye daladala aibu ilioje na vijora vyao
 
Wale wa ukumbi wa ubungo Plaza kila weekend kunakuwaga na harusi kwa hiyo kubeba chakula ni kawaida si nimetoa hela
 
Yaani wewe mtoa huduma unataka vikibaki uende navyo kwenye kijiwe chako ukawauzie watu tena? Huu nao ni uroho!
 
Back
Top Bottom