Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Haha we jamaa unachekesha sana nchi zipi hizo za wenzetu??? Ni jambo la kawaida kabisa duniani kote watu wanakula viporo bila shida..huwezi kuona vitu kama hivyo katika nchi za wenzetu kwani kwa kufanya hivyo wao wanaona ni kutokustaharabika.
Huo sio umasikini ni upendo! Kwenye sherehe nyingi mara nyingi mavyakula ni yale yale!!Umaskin
Nyumbani umeacha watoto hawajala unawabebea nao wale maana nyumban havipo
Acha uchoyo wewe, mc kasha tangaza jamani chakula kimebaki huko tunaomba ...mrudie..Ni kukosa ustaarabu tu.
Kifupi ni tabia mbaya sana.
Vyote vilivyoandaliwa ni kwa ajili ya waalikwa wote. Vikibaki anayejisikia kubeba anaruhusiwa na isiyoshe amechangia kama alikuwa aje na mwenza lakini alishindwa pia haki yake. Mnamwachia mwenye shughuli hahitaji ashajiwekea vyake.Ni kukosa ustaarabu tu.
Kifupi ni tabia mbaya sana.
Kuna watu hawatumii nyama, hawatumii pombe hawatumiii vitu vyene sukari na hakuna option halafu wamechanga sawa na wanywaji wa pombe, soda, je inadhuru nini wakichukua vitu hivyo kuwapelekea ndugu zao kama nia ni njema? Hata hao wa nchi zingine wakilielewa hili siyo dhambi wakiigaKama utambulisho unavyoeleza, hii tabia imeonekana kuzoeleka na hata kuonekana ni jambo la kawaida kwa jamii nyingi za kiafrika na huwezi kuona vitu kama hivyo katika nchi za wenzetu kwani kwa kufanya hivyo wao wanaona ni kutokustaharabika.
Je, kwako binafsi inauchukuliaje tabia hii?
Je, ulishawahi kubeba chakula au kinywaji toka kwenye sherehe nini sababu?
Tushee maoni yetu wadau.
Take away, tatizo linakuja wanavyoanza kupaki kabla Wageni hawajamaliza kulaKama utambulisho unavyoeleza, hii tabia imeonekana kuzoeleka na hata kuonekana ni jambo la kawaida kwa jamii nyingi za kiafrika na huwezi kuona vitu kama hivyo katika nchi za wenzetu kwani kwa kufanya hivyo wao wanaona ni kutokustaharabika.
Je, kwako binafsi inauchukuliaje tabia hii?
Je, ulishawahi kubeba chakula au kinywaji toka kwenye sherehe nini sababu?
Tushee maoni yetu wadau.
Hii ni kawaida nchi ninayoishi, kukiwa na sherehe, watu (sio wote), huleta chochote, iwe amepika au amenunua. Na mwisho wa sherehe, anayetaka hufungasha chochote. Ni kuzuia uharibifu au utupaji wa vyakula hovyo.Nchi za wenzetu ata hawachangishani michango.
Sasa mzee vyakula vibaki si vitaharibika tu hivyo?