Unachukuliaje tabia ya watu kubeba vyakula au vinywaji toka kwenye masherehe na kurudi navyo nyumbani

Unachukuliaje tabia ya watu kubeba vyakula au vinywaji toka kwenye masherehe na kurudi navyo nyumbani

Umaskin
Nyumbani umeacha watoto hawajala unawabebea nao wale maana nyumban havipo
 
huwezi kuona vitu kama hivyo katika nchi za wenzetu kwani kwa kufanya hivyo wao wanaona ni kutokustaharabika.
Haha we jamaa unachekesha sana nchi zipi hizo za wenzetu??? Ni jambo la kawaida kabisa duniani kote watu wanakula viporo bila shida..
Au kwa kuwa nchi za wenzetu wanaita leftovers????

Kama ulikuwa haujui hata ukienda kwenye restaurant kubwa , mtu anakula /buffet akibakisha anaomuomba pick up boy amfungie chakula chake vizuri huwa wanaondoka navyo!
 
Umaskin
Nyumbani umeacha watoto hawajala unawabebea nao wale maana nyumban havipo
Huo sio umasikini ni upendo! Kwenye sherehe nyingi mara nyingi mavyakula ni yale yale!!

Ila mnapokula kwa kushare inanoga
 
Ni kukosa ustaarabu tu.
Kifupi ni tabia mbaya sana.
Acha uchoyo wewe, mc kasha tangaza jamani chakula kimebaki huko tunaomba ...mrudie..

Pombe mnakomaa nazo kwa fujo, kwanini usibebe chakula? Ustaarabu ni kukimwaga?
 
Chakula chenyewe chakula gani ubebe sasa,ni yale yale tu mapilau nyama hayana kipaja kuku,njegere, ikizidi sana vifinyango vya nyama na kachumbari kama kanuni vile.
Mi nikienda naenda kuzitwanga monde tu hata huo msosi naweza nisiguse kabsaa
 
Ni kukosa ustaarabu tu.
Kifupi ni tabia mbaya sana.
Vyote vilivyoandaliwa ni kwa ajili ya waalikwa wote. Vikibaki anayejisikia kubeba anaruhusiwa na isiyoshe amechangia kama alikuwa aje na mwenza lakini alishindwa pia haki yake. Mnamwachia mwenye shughuli hahitaji ashajiwekea vyake.
Wewe kama hubebi waachie wenye nazo.
 
Kama utambulisho unavyoeleza, hii tabia imeonekana kuzoeleka na hata kuonekana ni jambo la kawaida kwa jamii nyingi za kiafrika na huwezi kuona vitu kama hivyo katika nchi za wenzetu kwani kwa kufanya hivyo wao wanaona ni kutokustaharabika.

Je, kwako binafsi inauchukuliaje tabia hii?
Je, ulishawahi kubeba chakula au kinywaji toka kwenye sherehe nini sababu?

Tushee maoni yetu wadau.
Kuna watu hawatumii nyama, hawatumii pombe hawatumiii vitu vyene sukari na hakuna option halafu wamechanga sawa na wanywaji wa pombe, soda, je inadhuru nini wakichukua vitu hivyo kuwapelekea ndugu zao kama nia ni njema? Hata hao wa nchi zingine wakilielewa hili siyo dhambi wakiiga
 
Tunafosi kufananisha Maisha ya Africa na Wazungu na hapa moja kati ya sababu za kufeli.Africa by nature huwa tunaishi Kibinadam, yaani namaanisha hii tabia ya kushift misosi haiko kwenye sherehe tu ndo asili yetu Sasa mwafrika kujibagua kwa kujifananisha na Wazungu huo ni uboya.Embu tuwe na fikra za kuishi Kiafrika labda tutakuja kuwa free from Neo colonialism jamani.. Divide and rule yaani Mzungu kafanikiwa kututenganisha kututawala hadi kwenye chakula.
 
Kama utambulisho unavyoeleza, hii tabia imeonekana kuzoeleka na hata kuonekana ni jambo la kawaida kwa jamii nyingi za kiafrika na huwezi kuona vitu kama hivyo katika nchi za wenzetu kwani kwa kufanya hivyo wao wanaona ni kutokustaharabika.

Je, kwako binafsi inauchukuliaje tabia hii?
Je, ulishawahi kubeba chakula au kinywaji toka kwenye sherehe nini sababu?

Tushee maoni yetu wadau.
Take away, tatizo linakuja wanavyoanza kupaki kabla Wageni hawajamaliza kula
 
Nchi za wenzetu ata hawachangishani michango.

Sasa mzee vyakula vibaki si vitaharibika tu hivyo?
Hii ni kawaida nchi ninayoishi, kukiwa na sherehe, watu (sio wote), huleta chochote, iwe amepika au amenunua. Na mwisho wa sherehe, anayetaka hufungasha chochote. Ni kuzuia uharibifu au utupaji wa vyakula hovyo.
 
Back
Top Bottom