Unadhani Mwanga ndio kitu chenye spidi ya juu kushinda kila kitu? Vipi kuhusu hili jambo?

(Unahisi kipi kina spidi zaidi, Mwanga au Fikra


  • Total voters
    50
  • Poll closed .
Eti mwanga hauna spidi????
 
Me naona speed kali iko kwenye ubongo kutafsiri kitu.. Maana chochote unachokiona hapo hapo kwenye ubongo kinatambua hicho nn.. Ndio maana hata ukiangalia maandishi tuh utashangaa umeyasoma bila hata kutaka kuyasoma
 
Na unaweza ona vitu 100 kwa pamoja na vyote ukavijua bila hata kua na habar navyo... Kwa hio speed ya kuona na kutambua kitu... Ni kubwa zaid yaan haipimiki
 
Hapa ntakuuliza swali Gravity ipi Ulikua unamaanisha??

Dunia ina yakwake

Mwezi una yakwake

Na hivyo tunategemea bodies mbalimbali kwenye universe kuwa na gravity yakwake tofauti tofauti

Ni ipi sasa ambayo ina spidi kuliko mwanga
 
Sipingani kabisa na kile unachosema wewe kwa sababu ni fact, isipokuwa najaribu kukufanulia kile ninachomaanisha mimi ambacho in essence nacho pia hakipingani na kile unachosema wewe hapa. Labda ujaribu kurejea kidogo post yangu hii hapa #81 halafu baada ya pale, labda ndiyo tuweze kuendelea tena kama kutakuwa bado kuna chochote kutoka kwako
 
Mmoja azungumzie blachole na warmhole n vitu gan?
Kama Einstein alivyopenda kusema 'Imagination is more powerful than knowledge',tutumie thought experiment kupata picha black hole ni kitu gani

kila massive body ina ukanda ambao gravitational field yake inaishia,mfano gravitational field ya jua inaishia kwenye ukanda unaoitwa Oort cloud,vuta picha kitu chochote kinachojaribu kutoka nje ya huu ukanda kitavutwa na Jua,Unless kiwe na speed inayowez kuikimbia gravitational field ya Jua ambayo ni 615000 m/sec,hii speed inaitwa Escape Velocity
Formula ya Escape velocity ni ve=(2GM/r)½
ambapo G ni gravitationa constant,M ni mass ya hicho kitu(nyota/sayari) na r ni radius kutoka kwenye centre of gravity ya hicho kitu
ukiangalia formula utagundua kadri mass ya nyota au sayari inavyokuw kubwa escape velocity yake inakuw kubwa zaid
Kumbuka speed ya light ni 299 792 458 m / s kwa hyo mwanga wa jua unawez kutoka nje ya ukanda wa jua bila ya shida yoyote...Sasa vuta picha una kitu chenye mass mara 50 ya jua maana yake escape velocity yake itakuw kubwa kuliko speed ya mwanga,kwa hyo ata mwanga wa hicho kitu utashindw kuikimbia gravitational field yake

Black hole ni region kwenye universe ambayo ina gravitational force kubwa kiasi ambacho hata mwanga hauwezi kuescape,black hole nying inaaminika zimeundwa baada ya kufa kwa nyota kubwa sana,baada ya kifo cha nyota,mabaki ya nyota hyo yatakuw compressed na gravity yake yenyew na matokeo yake ndio hii region inayoitwa Black hole

Kwenye mfano wa jua tuliona jua ina ukanda wake unaoitwa Oort Cloud,hii black hole pia inakuwa na ukanda wake unaoitwa Event horizon,mwanga unapoingia kwenye hii horizon hauwez kuescape kwa hiyo kama utafanikiw kuingia kwenye event horizon utakutana na library kubwa ya kila mwanga uliowah kuwepo kwenye universe,kuanzia big bang kwa hiyo black hole ni kama kitabu cha kumbukumbu cha historia ya Universe

Ukishavuka event horizon hutokutana na kitu chengine chochote cha hyo black hole kwa sababu ya strong gravitational force,kila kitu kilichokuw kwenye ile nyota iliyokufa kimekuw compressed kwenye particle moja inaypoitwa singularity na hata wew utakuw compressed kwend kweny ile singularity lakini huu ni upande mmoja wa imagination
Upande mwengine wa imagination ni kitu kinaitwa rotating black hole,ambapo badala ya black hole ku compress to singularity ina collapse kuwa rapidly spinning ring,ikitokea umeanguka kwenye hii ring utawez kutokea upande wa pili wa hii ring ambapo kimahesabu huu upande wa pili utakao tokea inaweza kuwa universe nyengine tofaut na hii ya kwetu,kwa hyo unawez kutengeneza hole inayo act kama daraja kati ya universe moja na nyengine kupitia hii rotating black hole,hii hole ndio inaitwa wormhole
Kama wanasayansi wataweza kutengeneza kitu kama hiki laboratory maana yake mtu anaingia kwenye hiki kitu ataweza kusafir kwenda universe nyengine,atawez kurudi nyuma au kwenda mbela ya muda
 
General relativity
 
Nnaposema elimu ya outer space and time na dunia haiendani na uhalisi nakusudi hivyo,kuwa haviendani na hali halisi hata kidogo,yaani ni vitu tafauti kabisa,hivi vitu sio rahisi kufahamu hasa baada ya kupata elimu si rahisi kuona uhalisi hata kama uhalisi upo mbele ya macho.

Jua naliona kama sote tunavyoliona na kama nlivyosema kuwa jua haliko mbali wala halipo outer space na kama jua lipo 53 million miles away tusingeliona hata liwe kubwa kiasi gani, macho yetu yana mwisho wa uwezo wa kuona,hayawezi kuona infinity kwa sababu tu kitu ni kikubwa sana au kina mwangaza mkali, kwa macho yetu 1 million miles ni zaidi ya infinity achilia mbali 53 million miles,hivi vitu sio uhalisi hata kidogo tufungue akili.

jua,mwezi,sayari, nyota vyote havipo outer space vipo karibu sana na ardhi na wala dunia siyo sayari, hayo mafunzo yote ya skuli sio uhalisi,dunia kuelea angani na gravity na vitu vyote hivyo sio uhalisi,wala sayari zote hakuna yenye ardhi au udongo kama ilivyo ardhi ya dunia, mkuu sitakwenda mbali sana ila kama nlivyosema kuwa hivi vitu si rahisi kufahamu hasa ukiwa na elimu ya skuli pekee na ufahari wa elimu ndio adui mkubwa wa ufahamu.
 
Sasa mzee utatrace vipi hio sauti wakati unaweza kuta hio energy ilishaenda hadi kwenye mkaa na nikapikia makande.

Sound imeenda kwenye electrical impulses thru masikio yangu mimi nikareact na ngumi..ikaja kifuani kwako ikaleta heat na impulses tena yani it's practically impossible kutrace sauti ya sekunde 2 tu nyuma maana sio kwamba sauti yooote inageuka kua aina moja ya energy no..inageuka kua aina tofaut tofaut na inasambaa all over
 
Ni kweli fikra ya mwanadamu ina speed kuliko mwanga, unaweza kwenda nnje ya galaxy yetu kwa hio sekunde, labda tofauti ije kwamba mwanga ni KITU, cha kuonekana kwa macho, na fikra ni HALI, isiyoonekana kwa macho
Kama ni fikra iko slow kurko mwanga,
Unaesema unaenje nje ya galaxy, utaendaje kifikra angar hujawah kufika
Pili macho yakiona ilo shati, ni mwanga umesafir mpaka jichon kwako na mpaka kwenye retina ikabadrishwa ili uwe umeme then unapita kwenye optical nerve ndo unabadrishwa tena kwenda kwenye akili then process za kutambua zianze'
Process za mwil ziko slow, sema mazoea ndo yanafanya udhan yako fasta, ukitak kujua ni dista ce yako na huyo mtu, lets say 3meters mpaka umtambue mwanga ushasafiri mara milion100, ukigawanya kupata mda ni mdogo sana kuringanisha na fikra, ata computer na processor zake zote haikarbii ata kidogo, ata chembe ya robo ya speed ya mwanga, usiongelee kuzunguka dunia ukadhan dunia ni ndogo kaka
 
Mada ilitakiwa ifungwe na jibu hili
Kuendeleza mada ni ukosefu wa adabu na ni dhuluma ya wazi ya mawazo kuntu ya mtoa jibu!
Binafsi hii mada imefika mwisho kwa jibu lako
Mwanga mwanga ndio baba lao
 
Speed ya Nerve impulse ni ndogo kuliko ya Mwanga yani ya Mwanga ni 300,000Km/s huku ya Nerve Impulse ikiwa ni 342Km/s..

Umetolea mfano wa shati na Mimi naomba nikutolee huu mfano..

*Kiwango ambacho huona ambavyo huona video inacheza kwenye Tv ni matokeo ya macho kushindwa kutofautisha picha zilizofuatana kuanzia kiwango cha speed ya picha 24 kwa sekunde yani 24fps..

Mpaka hapo utakuwa umeona vile kunatofauti kubwa Kati ya speed ya kuona ya macho na Mwanga..
 
Halaf huo mfano wako umejikita kwenye computation yani uwezo wa ubongo kuchakata.
Uko sahihi kabisa. Mimi nimeshasema tangu awali kwamba kwenye mjadala huu, watu wanachanganya kati ya "processing/processor speed" na travel speed
 
Naomba nitofautiane na ww kidg,

Kwa nnavyo elewa, unapoona kitu mfano shati la njano (kama mfano wa mdau), maanake mwanga umesafiri kutoka hilo shati au chanzo mpaka retina ya jicho. Then cell hubadilisha miale kuwa kuwa signal ambazo ubongo hutafsiri na kukupa maana kuwa Teenager umeona shati la njano.

Sasa mwanga umetoka kwenye shati mpaka kwenye jicho. Fikra zimeanza ubongo ulipopata signal na kutafsiri na kukupa maana. Kwa namna fulani yote yanahusisha kiungo cha kuchakata(kuprocess).

Ishu inakuja pale kiungo hiki kinaposhindwa kutoa jibu sahihi, basi inaweza kuathiri speed.
Mfano; kwa mfano wako mimi naona sio kwamba fikra zimesafiri muda mrefu, ila ni kwamba zimefika ila jibu halijawa tayar, hivyo ubongo umekosa mrejesho sahihi uliouhitaji(jibu la hiyo hesabu yako) na kukufanya uhisi fikra hazina speed ya kutosha. In real sense hata kutambua kuwa hesabu ni ngum kwa kupitisha macho tayari fikra zimefikisha ujumbe.
Mfano 2: Mfano wa shati la njano. Kama hyo mtu angekuwa sehem ambayo haonekani vzr either umbo au shati, mtoa hoja asingeweza kumtambua. Kwa namna fulani unaweza tafsiri mwanga umechelewa na kufikinya macho uone vzr illa kumbe ubongo ndo umeshindwa kutafsiri picha sahihi.

Swali fikirishi 1: Kama mwanga unazunguka dunia kwa muda mfupi hvyo, vipi fikra zinazoweza kunipeleka utotoni na kunirudisha palepale nnapoulizwa swali na nikamjibu bila delay? Vipi zinavyoweza kunipeleka kwenye imagination za maisha ya zaman au yajayo pale nnaposoma habari za kufikirika?

Swali fikirishi 2: Kuna utofauti gani wa nerve impulse na fikra?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…