Mmoja azungumzie blachole na warmhole n vitu gan?
Kama Einstein alivyopenda kusema 'Imagination is more powerful than knowledge',tutumie thought experiment kupata picha black hole ni kitu gani
kila massive body ina ukanda ambao gravitational field yake inaishia,mfano gravitational field ya jua inaishia kwenye ukanda unaoitwa Oort cloud,vuta picha kitu chochote kinachojaribu kutoka nje ya huu ukanda kitavutwa na Jua,Unless kiwe na speed inayowez kuikimbia gravitational field ya Jua ambayo ni 615000 m/sec,hii speed inaitwa Escape Velocity
Formula ya Escape velocity ni ve=(2GM/r)½
ambapo G ni gravitationa constant,M ni mass ya hicho kitu(nyota/sayari) na r ni radius kutoka kwenye centre of gravity ya hicho kitu
ukiangalia formula utagundua kadri mass ya nyota au sayari inavyokuw kubwa escape velocity yake inakuw kubwa zaid
Kumbuka speed ya light ni 299 792 458 m / s kwa hyo mwanga wa jua unawez kutoka nje ya ukanda wa jua bila ya shida yoyote...Sasa vuta picha una kitu chenye mass mara 50 ya jua maana yake escape velocity yake itakuw kubwa kuliko speed ya mwanga,kwa hyo ata mwanga wa hicho kitu utashindw kuikimbia gravitational field yake
Black hole ni region kwenye universe ambayo ina gravitational force kubwa kiasi ambacho hata mwanga hauwezi kuescape,black hole nying inaaminika zimeundwa baada ya kufa kwa nyota kubwa sana,baada ya kifo cha nyota,mabaki ya nyota hyo yatakuw compressed na gravity yake yenyew na matokeo yake ndio hii region inayoitwa Black hole
Kwenye mfano wa jua tuliona jua ina ukanda wake unaoitwa Oort Cloud,hii black hole pia inakuwa na ukanda wake unaoitwa Event horizon,mwanga unapoingia kwenye hii horizon hauwez kuescape kwa hiyo kama utafanikiw kuingia kwenye event horizon utakutana na library kubwa ya kila mwanga uliowah kuwepo kwenye universe,kuanzia big bang kwa hiyo black hole ni kama kitabu cha kumbukumbu cha historia ya Universe
Ukishavuka event horizon hutokutana na kitu chengine chochote cha hyo black hole kwa sababu ya strong gravitational force,kila kitu kilichokuw kwenye ile nyota iliyokufa kimekuw compressed kwenye particle moja inaypoitwa singularity na hata wew utakuw compressed kwend kweny ile singularity lakini huu ni upande mmoja wa imagination
Upande mwengine wa imagination ni kitu kinaitwa rotating black hole,ambapo badala ya black hole ku compress to singularity ina collapse kuwa rapidly spinning ring,ikitokea umeanguka kwenye hii ring utawez kutokea upande wa pili wa hii ring ambapo kimahesabu huu upande wa pili utakao tokea inaweza kuwa universe nyengine tofaut na hii ya kwetu,kwa hyo unawez kutengeneza hole inayo act kama daraja kati ya universe moja na nyengine kupitia hii rotating black hole,hii hole ndio inaitwa wormhole
Kama wanasayansi wataweza kutengeneza kitu kama hiki laboratory maana yake mtu anaingia kwenye hiki kitu ataweza kusafir kwenda universe nyengine,atawez kurudi nyuma au kwenda mbela ya muda