Unadhani ni Kitu gani kimembadili ghafla Profesa Shivji na sasa hana Uharaka wa Katiba Mpya huku akisema ni Jambo la Kimjadala zaidi?

Kwa vyovyote vile,iwe usiku ama mchana.Jamhuri yetu ya leo,sio ile ya miaka ya 80-95.

Anaumri gani kwa sasa,na elimu yake ameipatia katika mazingira gani.Hatutaki ujima sisi Tanzania ya leo.
Ajiulize tangu amepata huo uprofeseli ni miaka mingapi imepita.
Wazee wakae kimya,maana kwa upande wao wameshindwa kulisaidia Taifa kwenye mambo mhimu.
Siasa ni nzuri kama umeitumia vizuri,pia ni mbaya ukiitumia visivyo.Hatuna taasisi imara tangu na tangu Bali tuna taasisi sujudu kiongozi.
Hitaji LA katiba haliepukiki kwa mkitadha wa sasa.

Nijue tu,ana ndugu zake wangapi serikalini?.
 
Amehongwa na ccm huyo gabachori kafulia mbaya baada ya kustaafu udsm,hata project yake ya kigoda cha mwalimu haina wafadhili siku hizi na imekosa mvuto,kule ndio alikuwa anapata ulaji,chamber yake ya sheria ,shivji and company advocate in kesi saba tu,tumuhurumie huyu mzee njaa haina baunsa
 

Aina hii ya mtazamo ndio shida kubwa ya nchi hii. Sitazungumzia hizo shutuma nyingine unazotoa, huenda una taarifa sahihi na kamili kuhusu unayoyasema.

Kwa swala la Katiba, Chadema ni sehemu ya raia wa nchi hii. Wana wajibu kisheria kuzungumzia jambo jambo hili sawa sawa na wale wasiolitaka wanavolizungumzia. Shida yako ni kudhani si swala la Chadema bila kuonesha ni swala la nani - huku hata CCM wanaosema sio muda wake ukiona hawatanufaika na kubaki kwa katiba?

Ni nani ana jukumu hilo basi?? Na njia za kukishughulikia au kutolishughulikia ziko wapi?? Kwa mbwiga kama wewe - huwezi kujua hii point pekee inatosha kuwa sababu ya kuiandika Katiba yetu upya ili njia, sababu za kutaka mabadiliko ya Katiba zijulikane wazi!!
 
Anaenda na mdundo wa ngoma, hakuna jingine......ni sawasawa na tume ya korona. Unasikilizia ngoma inapigwa namna gani na wewe unademka kufuatisha mdundo wa ngoma.....
 
Huyu ni Mhindi hivyo apuuzwe tu,siyo mzawa hivyo hayajui machungu yetu yatokanayo na utawala huu wa mabavu uliosimikwa kwa mtutu wa bunduki.
 
Hoja muflisi hizi,mnzirudia kila siku. Tumeshawapuuza.
 
Hata mchakato wa katiba ulioisha prof Shivji alisema tusiwe na haraka tuwe na MUAFAKA WA KITAIFA kwanza ndo twende kwenye mchakato wenyewe. Nilifatilila mihadhara yake yoote alisisitiza juu ya MUAFAKA. Tukampuuza lakini mwisho wa siku tukaumbuka
 
Huu msemo wa wananchi wanataka katiba mpya, ni wananchi gani hao??,maana huku mtaani kilio ni hali ya maisha, na hata vijiweni ni nadra kusikia watu wakisema wana shida sana na katiba mpya.
 
Ndugu hili Andiko lako lingekuwa ni Bidhaa iliyoko Dukani kwa Mauzo ningeinunua kwa Gharama yoyote ile na hata kama ingenibidi Kukopa Pesa mahala ningefanya hivyo.

Umesema Ukweli mtupu na Heko sana.

Ile post namba moja ni kama ulikuwa unapima upepo, ila kwa post hii umeonyesha upande halisi uliopo. Ni hivi, katiba mpya ni lazima , hivyo badilisheni mapambio tu lakini habari ndio hiyo.
 
Kwa akili yako unadhani kuna wana CCM watapaza sauti kuomba katiba mpya au mnajitoa akili?
 
Kwa maoni yangu suala la katiba ni la muhimu lakini si la kukurupuka nalo.Kuanzia utawala wa awamu ya tano,kifo cha JPM na kuchukua madaraka kwa mama,kuna maswali mengi ambayo katiba ya sasa haiwezi kujibu lakini sio suala la kiuanaharakati.Kuna mambo mengi ya msingi,asikuambie mtu unaweza ukawa na nguo nzuri lakini ukavaa na usipendeze.
 
Uzoefu aliojifunza kwenye nchi zilizofanya hivyo kama Kenya,South Afrika nk hakuna cha maana kimebadilika.

Pili kuna watu Wana ajenda zao za Siri wanataka kupitia mgongo wa Katiba mpya,wamemsitua Maza..

Eti Katiba mpya ili kuwezesha chadema kuingia ikulu kwa kuungwa mkono na wahuni fulani kutoka ughaibuni,hakuna kitu kama hiyo..Tzn hii bado kufikia stability ya kuhitaji Katiba mpya.

Huko kitaa ukiuliza mtu Katiba mpya ndio takwa lako hana habari sembuse kumwambia faida ya Katiba hajui chochote .
 
Nyie wananchi mnaanza lini? Maana hakuna aliyewazuia mpaka sasa. Au ni mpaka cdm na ccm wawaachie ndio muanze?
Nickname ni tatizo!! Hawa ndio maana Ontario aliwapiga hela ni wajinga sana yani!!

Sisi tuongee kwa mfano watatukumbuka mbeleni
 
Walio wengi wakina nani? Katiba mpya itakuletea pesa mezani?
 
Toa source ya taarifa yako au clip.
 
Napata wasiwasi sana na vijana wa sasa!! Hivi Katiba ya warioba ilikuja kuchukuwa maoni kwa kila sehemu, umeshindwa vipi kutoa maoni?

Yani umeshindwa hata kujiuliza kwanini mikataba ya nchi yako ni siri wakati ni mali yako. Then unaongelea katiba wakati ipo wazi tu tunaweza kusema toa hiki weka hiki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…