Swali zuri sana, tena linahitaji hoja za msingi.
Unajua kuna vitu vinatokea tunavichukulia kirahisi sana au pengine ndio tunaona ni maendeleo ya technolojia nianze hivi:
Miaka ya nyuma jamii ilitunza maadili sana na jambo moja lililotiwa mkazo ni tendo la ndoa baada ya ndoa, na mabinti walikuwa makini na wakali sana juu ya hili, hiyo ilimlazimu mwanaume kuoa ili apate tendo la ndoa ambalo kwake ni hitaji muhimu sana, na hii ilifanya taasisi ya ndoa na familia kwa ujumla kupata heshima kubwa na kuwa jambo la muhimu katika maisha ya mwanadamu.
Siku hizi kuna vita kubwa sana juu ya hii taasisi ya ndoa pamoja na familia, ndio maana kuna makundi haramu yameibuka, Kataa ndoa, superwoman, haya makundi yako kimkakati kabisa kuhakikisha hii taasisi kuonekana haina maana, upatikanaji wa tendo lenyewe nje ya ndoa umerahisishwa mno, kiasi kwamba hakuna umuhimu wa kuoa ndio upate tendo la ndoa, Lakini pia ibilisi ameachilia roho ya uharibifu na mafarakano ndani ya hizo ndoa ili kusiwe na maelewano, lengo ikiwa ni kuisambaratisha hiyo ndoa na umuhimu wa ndoa yenyewe usionekane, ndio maana utashangaa binti amestrugle apate ndoa halafu anapata anaanza kumnyima mwenzake, mara anaanza mawasiliano na maex, mwisho wa siku ndoa inajifia kibudu.
Nini kifanyike?
1. Lazima turudi kwenye msingi wa kuelewa ndoa ni nini? na ni nini kusudio la kuwepo kwa ndoa ili tuwe na familia zilizo salama kwa vizazi vijavyo.
2. Lazima ijulikane kuwa ndoa ni mpango wa Mungu sio matakwa ya mwanadamu, na huo mpango unapigwa vita vikali lengo ni kuondoa upendo unaojengwa kupitia hizo ndoa, kama likiachwa kama lilivyo itafika kipindi binti kulala na baba yake, au kijana kumlala mama yake litaonekana jambo la kawaida.
3. Lazima hatua za madhubuti zichukuliwe, hasa kwa watumishi wa Mungu, ambao nao wamejikita katika kuhubiri pesa, mafanikio tu huku wakiacha mambo ya msingi, ukigeuka huku sadaka, ukigeuka huku sadaka. Yale mambo ya msingi yameachwa.
4. Jamii lazima ikubali kuwa kwenye hili tumeteleza, wametengenezwa wanawake ambao ni material oriented, jinsia ya mwanaume inapigwa vita maeneo yote, angalia hata maofisini utakuta idadi ya wanawake ni kubwa kuliko wanaume, halafu wanaume vijana hawana ajira, huyu mwanamke majukumu ya ndoa hawezi kuyabeba, tunaona mifano huku kwa maandiko mbali mbali mwanamke akipata nafasi ya cheo na kipato ndoa hakuna hapo, ila nje atagawa kipapa bila shida kwa kisingizio cha haniridhishi.