Unadhani ni kwanini uhuru na haki ya kikatiba ya kuandamana kenya inawaangamiza gen z wenyewe?

Unadhani ni kwanini uhuru na haki ya kikatiba ya kuandamana kenya inawaangamiza gen z wenyewe?

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
51,453
Reaction score
41,274
Ni kwasababu hawajui wanachotaka, hawamjui aduai yao au hawaelewi namna bora ya kudai mabadiliko wanayohitaji na badala yake wanajikita kwenye uharibifu wa samani za umma ambazo baadae zitakarabatiwa kwa kodi zao wenyewe?

Wasipojitahimini kwa kina na kutumia hekima na busara kuwasilisha na kudai mabadiliko wanayopendelea,
wanaweza kuishia kung'oana meno, kutoana macho wao kwa wao, kwasababu kinachoonekana sasa ni mgawanyiko wa wazi baina ya waandamanaji amboa wote wana haki na uhuru sawa wa kuandamana kwa mujibu wa katiba.

Kitendo cha waandamanaji wanaotaka mabadiliko kwa kuharibu maduka ya watu na miundombinu, kukutana wanja moja na waandamanaji wasiotaka makelele na waporaji, kutasababisha uharibifu na maafa zaidi miongoni mwa gen z na matokeo yake asiwepo wa kufaidika nayo.

Huenda maandamano ya kudai bei ya unga ishushwe chini huku wakiwa na masufuria kichwani yakashuhudiwa tena kuanzia mwezi September, kwasababu muda mwingi wakenya wanautumia kuandamana na sio kulima.

Mungu Ibariki East Africa.
 
Back
Top Bottom