Unadhani ni kwanini watu wengi wanaogopa kuwa Mashahidi Mahakamani?

realMamy

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2024
Posts
3,925
Reaction score
8,853
Hili limekuwa ni tatizo sugu kwa kuwa watu hawataki kuwa mashahidi wa kitu walichokishuhudia.

Shahidi ndiye anayesababisha kesi iweze kumalizika kwa haraka.

Lakini watu wanaogopa.

Lakini baada ya kufanya utafuti wangu mdogo wengi wao wanasema wanaweza kupata matatizo endapo watu aliowatolea ushahidi watashinda kesi.

Wewe unadhani sababu ni nini?
 
Kama ulishaangalia movies za kihindi jibu unalo ile miamba ukiitolea ushahidi ikitoka inatetekeza familia nzima

Na kabla haijateketeza inabaka kwanza female members wote kwenye familia
 
ILIANZIA KWA PETRO ALIPO KUWA ANAMKANA BWANA YESU KRISTO MARA TATU

NI ROHO CHAFU ILIYO BEBA HOFU INAHITAJIKA MAOMBI

In our nation we need serious intercessors for this situation
 
Fumba macho, kesi nyingine unaweza kulogwa bure.
 
ILIANZIA KWA PETRO ALIPO KUWA ANAMKANA BWANA YESU KRISTO MARA TATU

NI ROHO CHAFU ILIYO BEBA HOFU INAHITAJIKA MAOMBI

In our nation we need serious intercessors for this situation
Kabisa
 
Guilty versus innocence.

Kumsamehe MTU ni bora zaidi na kutojihusisha na migogoro ni bora zaidi Sana.
 
Kila ikifika siku ya kutoa ushahidi unaumwa na kulazwa, ugonjwa hauonekani na muda wa mahakama ukiisha unapona.
Daaaa! πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…
 
Nipo Nps hapa natakiwa nitoe ushahidi mahakamani alafu nakutana na huu uzi
 
Kila ikifika siku ya kutoa ushahidi unaumwa na kulazwa, ugonjwa hauonekani na muda wa mahakama ukiisha unapona.
Haha kuna kesi hapa natakiwa nitoe ushahidi mi ndo shahidi wa mwisho hii kesi imehairishwa Mara nyingi sana kila nikiitwa kwenye ushahidi nakuta hakimu anaesikiliza kesi ni mgonjwa naishia kuonywa na kupangiwa tarehe nyingine sijui anapigwa misumari.
 
Watu wanaogopa usalama wao basi.kama mtoa ushahidi unahakikishiwa usalama wake,itakuwa ni rahisi kutoka ushahidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…