Unadhani ni nini kimesababisha mpaka dereva wa semi trela kuchora?

Unadhani ni nini kimesababisha mpaka dereva wa semi trela kuchora?

Benjamin10

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2016
Posts
409
Reaction score
598
Tazama hii video mpaka mwisho!! Unadhani ni nini kimesababisha mpaka dereva wa semi trela kuchora 7??

Kama huyu dereva mwenye gari inayorecord video angekua na speed up to 100kmph nini kingetokea?

 
Duuh si mchezo.

Nadhani mwenye kosa ni huyo mwenye basi ali overtake bila kuchukua taadhari, ukiangalia ameovertake wakati gari yenye dash cam haipo umbali mrefu kuliko alipo yeye, so nadhani baada ya hilo basi kuona gari ya mbele ipo karibu ndio ikabidi amchomekee huyo jamaa wa Scania ili asikutane uso kwa uso na huyo mwenye gari ya camera, jamaa wa Scania ikabidi ndio atoke nje ya barabara ili kukwepa kuligonga basi kwa nyuma na alivotoka nje ya rami upande wa kushoto nadhani akashindwa ku control vizuri gari ikarudi barabarani tena na kuchora 7.

Huyo jamaa mwenye gari yenye dash cam angekua nduki huo mzinga hapo ungekua sio wa kitoto, angekula trailer hiyo.

Mungu atulinde aise, humu barabarani madereva wengine ni vichaa.
 
alifeli breki hiyo yaani malori haya mengi yashatupwa na wazungu huko kwao hayawafa ndio wanayaleta huku spana juu
Kuna bus lilimuovertake wakati mbele kuna hiyo gari yenye camera, dereva wa bus akarudi upande wake ghafla baada ya kuona asingeweza kuovertake gari la pili mbele yake matokeo ndiyo huyo mwenye semi akajinusuru kutoligonga bus kwa nyuma
 
Huyo amechomekewa na hilo bus
Yeah ni sahihi na alikua mwendo mkali.. akatanua... nadhani tera likawa linamvuta nje ya barabara na kukwepa kuligonga bus kwa nyuma..
 
Kuna bus lilimuovertake wakati mbele kuna hiyo gari yenye camera, dereva wa bus akarudi upande wake ghafla baada ya kuona asingeweza kuovertake gari la pili mbele yake matokeo ndiyo huyo mwenye semi akajinusuru kutoligonga bus kwa nyuma
Lakn amejihatarishia zaidi mi naona maana kama huyu anaerecod angekua kasi
 
Hii inairwa jacknife , na hapo bahati nzuri haijamaliza , worst case scenario ni kuwa hicho kichwa huwa kinazunguka na kujibamiza kwenye trailer , mara nyingi haponi mtu.

Hutokea kwenye gari ambazo hazina Abs, na husababishwa na breki kali wakati matairi hayapo kwenye surface moja , kama hapo huyo wa semi alimpisha basi ,tairi za kushoto zikawa nje ya lami , alipokuja kukanyaga breki hizi za kwenye lami zika lock wakati zile za kushoto zinasota , ndo lori ikazunguka.

Gari zenye Abs huwezi kuta zinafanya hivyo
 
Alifeli breki hiyo yaani malori haya mengi yashatupwa na wazungu huko kwao hayawafai ndio wanayaleta huku spana juu
Mkuu
Hakuna gai inayotupwa ulaya !! Kitu pekee kinafanywa hizi lori zije Afrika ni kwa sababu ya tight emmissiin requirements, europe kwa mfano sasa wapo euro 6 , maana yake ni kuwa hata zile scania au benzi mpya za hapo vingunguti haziwezi kutembea london. .
 
Back
Top Bottom