Unaelewa nini unaposikia Mtu akisema yeye anasomea Computer?

Unaelewa nini unaposikia Mtu akisema yeye anasomea Computer?

Huo ni mjadala mpana,kwanza fani kama computer sceince ni pana sana,ni ngumu kwa chuo chochote duniani kutoa graduate ambaye atakuwa ameiva kwenye kila kona ya computer science....kama graduate hajaiva hata kona moja ya computer science hilo linaweza kuwa tatizo la graduate mwenyewe binafsi kwa sababu chuo kwa fani za computer ni kama platform tu kwamba umepewa access ya library,ya lectures na labs
kuna kona za computer science kama programming,system administration graduate anaweza akafunikwa na mtu alie mtaani kwa sababu zenyewe haziitaji sana hizo access ili mtu awe competent,the bad of story ni kwamba hizo kona ndio zina soko zaidi kwa sasa kwenye nchi kama Tanzania
Sio kweli kaka, angalia walio soma nje hii fani ndio wanaofanya makubwa..

Hapa nchini, vyuo vina IT department lakini website na mifumo yao wananunua kwa gharama kubwa kutoka nje hii sio serikali wala kampuni binafsi hao maIT kazi yao ni kwenda kusoma hii mifumo inavyofanya kazi then nao wanakuja kuwafundisha wagazi au wahasibu pale wanapohitaji msaada, Kwa serikali sasa imejipambanua kuja na taasisi ya serikali mtandao (EGA) kwa ajili ya kutengeneza website na baadhi ya mifumo ya serikali lakini vijana wengi wanaoajiriwa pale kwenye fani za IT baada ya mda hupelekwa nje ili wakasome maeneo mahsusi ili wakirudi wafanye kazi kwa ufanisi.

Na hili lipo kwenye taasisi zote muhimu kama TCRA, TPDC na BOT, hili halina ubishi kwenye masuala ya technolojia vyuo vyetu havina huo ufanisi wa kutoa hiyo kozi.

Fani kama IT, COMPUTER science, Telecom engineerin, software engineering ni fani ambazo mtu akiiva huna haja ya kuajiriwa inatakiwa kampuni zikufuate wewe, leo angalia hapa nchini vijana wa fani hizo wako mtaani kama njugu na ni wengi sana nadhani wanaongoza kwa wingi wakiendana na procurement..

Chuo kikiwa na chumba kimoja tu cha lab ya computer wanatoa kozi ya IT, angalia chuo cha utumishi wa umma(tpsc) wanatoa kozi hii kwa matawai yao yote kuanzia certificate, CBE MATAWI yao yote, Udom kuanzia certificate , SUA kuanzia certificate, Udsm kuanzia cetificate, DIT, MUST,ATC,NIT zote hizo kuanzia ngazi ya cheti..Kuna chuo cha uhasibu Arusha(IAA) MATAWAI YOTE wanatoa kuanzia certificate, IFM matawi yote kuanzia certificate, SAUT, Mzumbe, Sekomu,kuna chuo kule tanga kiko kange pale nadhani kinaitwa Ecknford Tanga university hakina hata sifa nacho kilikuwa kinatoa kuanzia certificate,TEKU, chuo cha kodi, chuo cha ustawii wa jamii, sijui kilimanjaro institute of technologr, MUSE, MUCCOBS, MWENGE university, Setfano memorial university..

Karibia vyuo vyote hapa nchini wanatoa hizi kozi hapa nchini kuanzia cetificate, matokea yake wanazalisha watu wengi ambao ni sawasawa na User wa kawaida, hawana tofauti hata kidogo ikiwa hata hawezi kufanya troubleshooting ya tatizo dogo la computer au kutengeneza hata mifumo ya kiteknology itakayomuwezesha kujiajiri..

Hii ni fani nzuri sana kwa dunia ya sasa ila kwa vyuo vya hapa nchini bado sana
 
Back
Top Bottom