Unaepuka vipi kuwa "Chikunde" ukiwa unadate na mtu mambo safi?

He he he he

Kuna mademu huwa wanazuga wa kishua sana kumbe tunakaa nao tu huku Tungi kigamboni.
Nimewahi kumuona mmoja yaani alikuwa anamhemyesha kibosile wa watu mpaka aibu.

Ajabu akitoka kudanga jioni tunabanana kwenye magenge yetu kutafuta dagaa mchele zile, analumangia na ugali mkavu siku inapita.

Ila nilienjoi sana kula chabo, maana alikuwa jamvi la wageni balaa na alikuwa hana hiyana.
Ukimuomba huduma anatoa, hata kwa mkopo.

Ila akikutana na mjinga mjinga anamshika masikio, jamaa lazima aamini ameopoa kitu kumbe yaliyomo hayamo.
 
Dagaa mchele na miguu ya kuku
 
Dagaa mchele na miguu ya kuku
Acha kabisa aiseee.

Maisha ya uswazi ukiwa na buku 2 siku imepita.

Unanunua fungu moja la dagaa mchele unaligawa mara mbili, nusu unakula mchana nusu nyingine unamalizia jioni.
Ukiona vipi kama appetite imekata unaongezea na kachumbali silingi 400 tu inatosha,
Unanunua nyanya za mia 2 na kitunguu cha mia 1 na karoti moja ya 100 siku imepita.

Nimeyamisi sana hayo maisha aiseeee.

Niliwahi pia kukaa kule kinondoni shamba, nilikula sana utumbo wa kuku.
Jioni tunayoosha miguu kuelekea msasani kule kuosha macho kwa kuangalia machangu wakijiuza, ukichoka unarudi kulala geto.

Maisha ya uswazi safi sana.
 
Ngoja nikatafute mwendelezo [emoji23][emoji23][emoji23].

Mimi kitu kilichonishinda ni kujivunga. Ukinitoa out sehemu za heshima sijui za uma, vijiti, visu, na nini sijui[emoji23][emoji23] naweka kando!!!!

Sema Mimi Baby mwelewa wakati mwingine ananishauri tuu "usitumie hivyo tutaaibika" na pia huwa ananifasiria menu [emoji23][emoji23][emoji23]maana sishindwi kuagiza uji nikijua kitu cha maana.[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mkuu sio dharau wala nini na mimi nimekulia uswahilini pia.

Ila utumbo wa kuku? kamguu ka kuku na vichwa vya kuku daah unavila! huwa nashangaa saana.
Mkuu vinaliwa tena sana tu.

Ikifika mida ya jioni unaona watu wanapita na masinia yamejaa miguu, utumbo na vipapatio kutokea Kisutu huko.

Hio ndio misosi yetu, ukipata na tembele ukakazia na maji ya Kandoro ya kutosha kinachofuata ni kuvua tu shati na kulala kibarazani kupata upepo safi kabisa huku unahemea juuu juu.
 
Kuna mwana siku nipo foleni dukani..nikaona kapimiwa miguu kama ndoo nzima. nikawa najiambia nikiwa nakula miguu si nitahisi nakula mkono wa binadamu.

Daah ila hongera kwao wamepewa roho nzuri ya kuingiza kila kisicho najisi.
 

Kuna mtu ukikaa nae safi tu, mzee mwenzangu enzi zetu nlikua fresh tu sioni noma niliwahi kula msosi mwingi zipu ya gauni ikakataa kufunga nashukuru ilikua usiku tukarudi home mbavu zipo nje.
Ishu ukutane na yule mtu unajivunga eti paja haumalizi japo ndo tatizo teh
 
Mimi na roho ngumu walai kwenye mambo ya msosi nimwone mtu aibu? Big no.

Mimi nilisha enda mahali ugenini, kwenye kahotel, mhudumu kajaza vijiko na kisu msosi wenyewe unaushika na mkono mmoja unaujaza kwenye viganja vya mkono vile vikorokocho vyote nikamwambia aviondoe nibakize kijiko tu,

Kuna sehemu nyingine ukiwa siriazi unaumbuka
 
Hahahahaha eti hadi zipu ikakataa kufunga.

Halafu hata vyakula vya hotelini vya mauma uma vitiji , visu vijiko huwa hata si vitamu.[emoji23][emoji23][emoji23]

Kama ni mtu wa kujivunga dawa ni kuagiza ma pizza tuu. Na sambusa
 
😀😀
 
Hahaha mkui hapo mchawi mbu na joto la usiku tu ila tumbo liko fresh kabisa mkuu umenikumbusha tungi aisee ni noma sana
 
Bidada mmoja aliingiwa na ushamba hoteli za watu akaangukia kuagiza pilipili
Meza ya pili kuna mzungu kaagiza sahani ya makuku
Alipomaliza akaita mhudumu akimwambia Kwa sauti The same
Ikaletwa sahani ya Kuku tena
Sasa bidada akasikia the same
Akaita mhudumu akimwambia the same
Akimaanisha sahani ya Kuku
Kumbe laja bakuli la pilipili tena
Bidada akaona aibu sana
 




Hahaha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…