Acha kabisa aiseee.
Maisha ya uswazi ukiwa na buku 2 siku imepita.
Unanunua fungu moja la dagaa mchele unaligawa mara mbili, nusu unakula mchana nusu nyingine unamalizia jioni.
Ukiona vipi kama appetite imekata unaongezea na kachumbali silingi 400 tu inatosha,
Unanunua nyanya za mia 2 na kitunguu cha mia 1 na karoti moja ya 100 siku imepita.
Nimeyamisi sana hayo maisha aiseeee.
Niliwahi pia kukaa kule kinondoni shamba, nilikula sana utumbo wa kuku.
Jioni tunayoosha miguu kuelekea msasani kule kuosha macho kwa kuangalia machangu wakijiuza, ukichoka unarudi kulala geto.
Maisha ya uswazi safi sana.