Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Teh woteHii chikunde inatumika hadi kwa wanaume au ni wanawake tu
Acha unaweza jikuta umevimbiwaWewe unaelewa Chakula kitamu sasa
Haya mambo ya kisu na uma kama yakupa shida, we jifanye tu unajiskia kinyaa kutumia hizo kitu ambazo huna uhakika zimetumiwa na wangapi kabla yako! Ukijifanyisha, utajulikana tu kwamba huna huo utamaduni manake hata kama utaweza kula lakini staili ya ushikaji na movement ya mikono itatoa jibu kwamba wewe ni chikunde ndani ya sekunde tano tu!Siku nyingine tumekaa mezani mambo ni yale yale kikuku hiki hapa mara uma, nikajitahidi tu hivo hivo nikamuacha na nyama nyingi roho ikiniuma, kwakifupi nikiona dalili za kuwa chikunde nakataa mtoko muda ntakaoenda kutafuta wali maharage na chachandu naujua mwenyewe sitaki aibu!!!!
Eeeh. Maana unavyokula tumbo linatamani zaidi. Jana nimepita ninaponunuaga dagaa nikakuta hawajafungua roho imeniumaaa maana nilikua nshapanga kupika mchicha wa Nazi Na dagaa mchele.Acha unaweza jikuta umevimbiwa
Basi me chikunde mzee mama, kwanza kama wali sielewagi kuula na kijiko nataka niufinyange ndo unakuwa mtamuTeh wote
Hahahaha kwamba kuliarrest lisifike chini lolHaya mambo ya kisu na uma kama yakupa shida, we jifanye tu unajiskia kinyaa kutumia hizo kitu ambazo huna uhakika zimetumiwa na wangapi kabla yako! Ukijifanyisha, utajulikana tu kwamba huna huo utamaduni manake hata kama utaweza kula lakini staili ya ushikaji na movement ya mikono itatoa jibu kwamba wewe ni chikunde ndani ya sekunde tano tu!
Yote tisa, kumi ni pale ukosefu wa uzoefu utakaposababisha pande la kuku lichoropoke kutoka kwenye umma wakati lilishakaribia kabisa mdomoni na kufuatiwa na zile body movement utakazofanya kujaribu kuhakikisha pande halifiki chini wakati watoto wa kishua wakipata eksident kama hiyo huwa wanajitahidi kulikwepa lisiwachafue huku mwenzangu mimi unataka kujaribu kuli-arrest lisifike chini.
Msusa ni nini?Huwa nampenda Sana ambaye ambaye anatukuza asili yake,. Mfano Masai huwa anakuwa hajui kitu na anajivunia kuto kujua. Na siyo ujuaji ambao mbele unaumbuka. Ukweli huku bongo kwenye hizi hotels mara nyingi nikifika naona mhudumu anaanza kunieleza Mambo ya beef beef mine huwa namwambia Mimi msukuma nieleze ugali maharage , nyama, msusa mlenda matembele nk hayo ma beef subiri waje wenyewe.
Na akileta visu vyake huwa namwambia nataka maji ninawe. Nakula kikwetu.
Unajua ukiwa na hela raha huogopi na una jeuri ya kulipa. Ila ukiwa unanunuliwa lazima umuonee aibu mlipaji
Ilikua zaidi ya kula nadhani nilifakamiahaha ha ha haaaaaa....
Aisee hii ya kula sana mpaka zipu kukataa kufunga imenikosha vilivyo, umenifanya nikenue kwa saut
Msusa ni majani ya mabogaMsusa ni nini?
Sipendi miguu ya kuku,kichwa,shingo,mgongoKuna mwana siku nipo foleni dukani..nikaona kapimiwa miguu kama ndoo nzima. nikawa najiambia nikiwa nakula miguu si nitahisi nakula mkono wa binadamu.
Daah ila hongera kwao wamepewa roho nzuri ya kuingiza kila kisicho najisi.
Tunyamaze utaitwa wa kishua.Sipendi miguu ya kuku,kichwa,shingo,mgongo
Migui sitakagi hata kuiona nikiagiza kuku wanaitupa kabisa na kichwa sitaki viona
Ahahahahahah hapana aisee mi sio wa kishua lakin hivyo vimiguuu hapana,wewe je unakula?Tunyamaze utaitwa wa kishua.
Utumbo wa kuku? daah bora nipike uji.Ahahahahahah hapana aisee mi sio wa kishua lakin hivyo vimiguuu hapana,wewe je unakula?
Ahahahahah watu wa dar wana mioyooo sanaUtumbo wa kuku? daah bora nipike uji.
Anhaaa. Nikajua ni aina ya samaki Kama kule kwetu TangaMsusa ni majani ya maboga