Unaepuka vipi kuwa "Chikunde" ukiwa unadate na mtu mambo safi?

Unaepuka vipi kuwa "Chikunde" ukiwa unadate na mtu mambo safi?

Kuna mtu fudenge alikuwa ananiita Chikundeee.... my Chikundeee twende samaki samaki leo..... Nami namjibu okee baby Chikundeee. Hehehehehhee Chikundeee.
 
Bila shaka chikunde mnamjua, kile kidada kinatolewa out na jamaa, kinajifanya sehemu nzuri ndo maeneo yangu kumbe ki asha ngedere hakijui kitu...Ulishawahi kudate na mtu mambo safi kiasi cha kuogopa kukaa nae mahali ukihofia kuaibika? Labda akikuuliza unatumia ketchup unajibu hapana halafu unamuita mhudumu alete tomato?😛

Mimi nilichokua nafanya ni kukataa tu najifanya nmeshiba kumbe tumboni ni empty, tumbo linaunguruma tu gruuu gruuu akisema tupite sijui burger point sijui pizza hut namwambia thanks much nimeshapata msosi am okay kumbeee minyoo imechachamaa tumboni, atakaponiacha lazma nikimbie fasta kula, nlikua nawaza labda nitakutana na menu siijui niishie kuabika. Nawaza mambo ya kula na uma na kisu naona tabu, mi napenda nikila samaki nimvuruge vuruge yani nisagesage mifupa ukiikuta mifupa usijue ni ya kiumbe gani. Kama ni kuku hivo hivo sasa nikiwa na huyo mambo safi si nitajitia aibu.

Siku moja nlikua so down nikaenda pale tilapia hotel kupunga tu upepo, nimeorder chips kuku uma na kisu pembeni. Sijui ndo kujali mteja jamaa kasimama pembeni nikashika ile uma na kisu nazuga zuga pale huku nikijiona chikunde, ikawa sasa nakula kwa kuvizia utadhani naiba akigeuka nakamata kuku kwa mkono kahkakah vunja vunja mifupa then nashika kisu utadhani nimekitumia nlipataje tabu!!!nashukuru aliondoka nikala kwa raha.

Siku nyingine tumekaa mezani mambo ni yale yale kikuku hiki hapa mara uma, nikajitahidi tu hivo hivo nikamuacha na nyama nyingi roho ikiniuma, kwakifupi nikiona dalili za kuwa chikunde nakataa mtoko muda ntakaoenda kutafuta wali maharage na chachandu naujua mwenyewe sitaki aibu!!!!
daah nimecheka sana
 
Ndio nilikua nakaa maeneo hayo karibu na kanisa pale mbele kidogo kuna bar nimeisahau jina hahaha aisee ni noma sana ila saizi niko zangu mbezi beach huku napunga upepo
He he he he
Mkuu na wewe wa tungi??

Unapajua mwembe radu??
 
Story yako imenikumbusha mbali sana ..
Nilikuwa nasimamia harusi ya jamaa yangu ... walifunga ndoa Dar then wakaleta harusi nyumbani ... wakanambia niwatafutie sehemu ya kupumzika .. nikawachukulia chumba Hill Front hotel .. jioni wakaomba wapelekwe sehemu yenye samaki wa ukweli tukaenda villa park; huko tulikaa wanne tukipanga namna ya kwenda kijijini kesho yake kwa ajili ya sherehe.
Alikuwepo mdada ambaye alikuwa ameandaliwa kwa ajili ya kuwa mpambe wa bibi harusi, huku mimi nikiwa mpambe wa bwana harusi ...
Huyo dada alikuwa mrembo kweli kweli hadi nilikuwa nasita kumsemesha .. lakini baada ya kumaliza kula samaki wa kuchoma .. akaomba maji ya kunawa .. dah! nilimshangaa kitendo cha kujifuta maji kwenye nguo!
 
Back
Top Bottom