mwanyaluke
JF-Expert Member
- Jan 22, 2015
- 704
- 2,435
Moja ya jambo linalotisha kwenye maisha ni kufilisika, ulikuwa na mali zako kidogo zinakusogeza na zinakupatia chochote, una watu wamekuzunguka unawapa kazi na unawapatia chochote japo kidogo, then inatokea hiyo hali inakata, humiliki Cha maana, mission za mjini zimekata, huonekani aisee unapauka, mahitaji ya msingi unayaona ni anasa, tabia za majungu zinakurudia, kutoka kutafuta muda saizi unawaza upotezaje muda, hali hii Huwa inatisha na kuchanganya sana.
Ninapokuwa mjini na ninapokutana na kaka zangu na watu tofauti wa hapa kwetu hasa wale walionekana miaka Ile wamebotoa au wapo njiani kutoboa halafu unakuta wamechoka, uzee huu hapa, ngozi zao hazishawishi, wamechagua kufanya kazi ndogo ndogo, mara bodaboda nk, wanakuomba pesa.
Niseme ukweli mimi binafsi nafsi yangu inangia na huzuni na hofu, huwa najiuliza wao walikosea wapi na mimi nina nini cha maana ambacho kinaweza kuwa ni ngao na uhakika.
Nikiwa kanisani nimejikuta sala yangu ni kuomba, "Mwenyezi MUNGU mwingi wa upendo, azibariki siku zangu, aniondolee siku za mateso, aniepushe na mikosi, laana na mabalaa," kwani Sioni what so special nilichonacho, je wewe unafanyaje ili usikae nje ya mstari wa maisha?