KUBADILIKA
Katika maisha ya mwandamu hapa ulimwenguni vitu viwili daima hawezi kuvibadlisha na vitabadilika vyenyewe milele.
1. Muda
Hatuwezi kuzuia muda usiende mbele ambapo sekunde, dakika, masaa, siku, tarehe miezi miaka kila kukicha itakuwa inasonga mbele, hivyo hata umri wetu siku zote utakuwa ukienda mbele hivyo hatua zetu zitabaki kwenda kuanzia utoto, ujana, uzee kisha mauti.
rejea kitabu kimoja kimeandika "kwa kila jambo kuna majira yake, na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu. wakati wa kuzaliwa na wakati wa kufa"
2. Mabadiliko (Change)
nagusia mada husika.
Mabadiliko katika maisha ya mwanadamu nilazima yatokee, na hii ni nature katika ulimwengu huu, na tabia ya nature siku zote huwa inatabia yakufanya replacement kila inapotokea mabadiliko.
AINA ZA MABADILIKO
Kuna aina mbili za mabadiliko ambazo ni Mabadiliko Chanya na mabadiliko Hasi ambapo kwenye uzi huu nitagusia mabadiliko hasi ikijumuisha mada tajwa hapo juu ya kufilisika.
YANAPOTOKEA MABADILIKO
Yanapotokea mabadiliko katika maisha ya mwanadamu huwa kuna athari kuu mbili
i. Kukubali mabadiliko ambapo nature huwa ina -reward positively kwa mtu anayekubaliana na mabadiliko
ii. Kukataa mabadiliko ambapo nature huwa ina -reward negatively kwa mtu anayekataa mabadiliko.
SABABU KUU ZA MABADILIKO HASI
katika maisha ya mwanadamu huwa zipo kuu katika makundi mawili
i. Internal forces ambapo hizi ni sababu zinazosababishwa na sisi wenyewe na kiasi kikubwa zikihusishwa na tabia hasi za maisha kama kupenda starehe kwa kiwango kilichopitiliza, kutopanga bajeti, kuiga maisha, kuishi katika show off, dear gambe, maadui, wanafiki nk
ii. External forces ambapo mabadiliko huja bila kutarajia wala kujipanga mfano majanga, magonjwa, vita, Ukame, Kiama, Mdororo wa kiuchumi, Mipango ya Mungu nk
NAMNA YA KUKABILIANA NA MABADILIKO HASI
i. Usimuombe Mungu akuepushe na mabadiliko bali muombe akupe hekima ya kuweza kukabiliana na mabadiliko maana baadhi ya mabadiliko tena hasi huyapanga yeye katika maisha ya mwanadamu kwa Utukufu wake mfano Ayubu na mfalme Nebukadereza.
Pia yeye kasema Kunawakati wa kutafuta na wakati wa kupoteza, wakati wa kulia na wakati wa kucheka, wakati wa kuweka na wakati wa kutupa, wakati wa kuomboleza na wakati wa kucheza, zipo nyakati nyingi kaziandika.
ii. Siku zote fahamu kuwa mabadiliko lazima yatokee katika maisha yetu mfano kuwa tajiri au kufirisika, kupigika na baadae kuwa tajiri.
hivyo tunapaswa kujiandaa kila siku kwa hilo na linapotokea tuwe tayari kuyapokea na kukubaliana nayo na kutafuta njia sahihi ya kufanya baada ya hapo (kukabiliana) nb fanya vitu vya msingi unapopata pesa nk
iii. Tujifunze kila siku kwa kusoma vitabu, kusikiliza Wenye hekima, kumtegemea Mungu na kutowaamini sana wanadamu.
mafano wa vitabu vizuri vya kusoma ili kujiandaa na mabasiliko, kwa waajiriwa soma Who Moved my cheese by Spencer Jonson, Wafanya biashara za kawaida soma Peak and Valley by Spencer Jonson, Trump Never give up by Donald J. Trump, mnaofanya biashara za online trading na investment on soft moneysoma Soros on Soros by George Soros pia mnaopenda kusikiliza seminar unaweza tafuta utube somo linaitwa 7 pliciple of planning and change by Dr Mayles Manroe lina video 5 ziko poa sana.
iv. Ukipata usibweteke waza zaidi ya hapo, wekeza zaidi kila siku, unapofanya biashara A waza siku utaigwa wekeza akili mpya kwenye mbinu mpya au biashara mpya, ukipata weka akiba na usitumie yote.
v. Punguza tamaa ya vitu vya hapa duniani, mfano kulala na wanawake/wanaume wengi nikujiletea mikosi na mabalaa yasiyo na sababu juzi nimemsikiliza shehe mmoja akihutubia vijana anasema Unapozini na mwanamke/mwanaume ambaye sio wako kuna majini na mashtwaini yanahudhulia hapo ili kukukwamisha katika mambo yako.
Pia kuna msemo unaosema Mwanaume aliyevuka tamaa ya ngono amesolve nusu ya matatizo yake hapa ulimwenguni.
vi. Usithubutu kutofautiana na taasisi nne zifuatazo
1. Mungu,
Hii ni mamalaka kubwa kupita mamlaka zote duniani na Mbinguni, usiingilie anga hii, usikejeli wala kuweka midahalo na mtu aliyesimama vema na Mungu mfano Mchungaji, Shehe, Padri hata muumini wa kawaida, usitafute umaarufu hapa wala kukosoa, anasema ''Mimi ni Mungu mwneye Wivu''
2. Serikali
Mungu mwenyewe anasema ''Kila mmoja na aitiii mamlaka iliyo kuu, kwa maana hakuna malaka isiyotoka kwa Mungu na ile iliyopoumeamriwa na Mungu" Hivyo serikali pia ni moja y mamlaka ya Mungu hivyo ni vema kuitii pamoja na maagizo yake
3. Wazazi
Hii pia ni mamalaka lakini katika sheria za Mungu ameagiza tuwaheshimu, usimesapu na wazazi wako kwa namna yoyote ile maana hapa unaweza pata tabu sana na kufupishwa siku zako za kuishi hapa duniani au kama sio kuishi kwa tabu kubwa.
4. Umma
Watu wanaotuzunguka ni muhimu sana kwa mstakabali wa maisha yetu ni vema sana kuishi nao kwa kuwaheshimu na kuthamini sana mchango wao kwa ujumla, tunmaishi kwa kusaidiana tusiwadharau wengine no matter what, lakini kuwasaidiakadili tunavyoweza au kutowaumiza.
Aristotle once said the society is accuracy as a thermometer, hapa alimanisha pokea pia mrejesho juu ya nini watu wanasema juu yako kama ni hasi jirekebishe, ogopa sana siku jamii ikisema ni huyu... afu huyu akawa ni wewe umekwisha.
vi. Ishi maisha yako na punguza mashindano, Muhimu hapa kula vizuri (sio gharama bali vyakula vyenye virutubisho muhimu), vaa kawaida (nadhifu), fanya kazi kwa bidii bila mashindano, ishi sehemu safi na salama, saidia wengine kwa kadri ya uwezo wako, punguza misifa na show off people come people go, kuwa na marafiki kiasi.
mwanasaikolojia mmoja wa kimarekani alifanya tafita akasema watu wengi wakifikisha miaka 40 ndipo hugundua kuwa hakuna mtu alikuwa anajali sana kuhusu maisha yao waliokuwa wakipambania waonekane.
Yapo mengi sana cha muhimu hapa Duniani tunajifunza kila uchwao, muhimu nikujua tu hakuna mtu anaweza kuzuia muda na kuzuia mabadiliko, hata awe nani katika ulimwengu huu maana hayayote ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu kwa ajili ya Utukufu wake, Asante.